Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-18 18:44:10    
Dunia yatangaza vita dhidi ya umaskini

cri

Tarehe 17 mwezi Oktoba ni siku ya kutokomeza umaskini duniani. Makao makuu ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa lililoko mjini New York, Marekani yalifanya shughuli za maadhimisho alasiri ya siku hiyo.

sauti uliyoisikia ni maonesho yaliyofanywa na wasanii kutoka New Zealand kwenye sherehe ya maadhimisho iliyofanyika katika kiwanja cha kaskazini cha makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Huku kukiwa na sauti ya muziki, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alipiga picha pamoja na wajumbe wa umma wa nchi mbalimbali waliokwenda huko kushiriki kwenye shughuli za maadhimisho, ambao wengi wao walitoka kwenye nchi zilizo nyuma kabisa kiuchumi duniani.

Mwaka huu miaka 20 imetimia tangu ianzishwe harakati za kupambana na umaskini. Katika siku ya tarehe 17 mwezi Oktoba miaka 20 iliyopita, maelfu ya watu walikusanyika mjini Paris, mji mkuu wa Ufaransa, walitoa wito wa kupambana na umaskini. Kwenye sherehe iliyofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alitoa hotuba fupi, akisema,

"Wakati inapowadia siku ya 20 ya kupambana na umaskini duniani, tusimame, tuoneshe nia yetu ya kisiasa na tujitahidi kutokomeza kabisa umaskini wa binadamu."

Katika hotuba yake Bw. Ban Ki-moon alisema pia, wakati ilipoanza milenia mpya, viongozi wa nchi mbalimbali duniani walitoa ahadi kwa makini na ujasiri kwa watu maskini duniani: kuwa watajenga dunia ambayo kila mtoto anaweza kumaliza masomo ya shule ya msingi, kila mtu anapata maji ya kunywa yaliyo safi na salama, na kila familia inaweza kuepukana na balaa la ugonjwa wa malaria, na watajitahidi kupunguza utoaji hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani. Jambo muhimu zaidi ni kuwa viongozi wetu waliahidi kujenga dunia moja, ambayo hakuna mtu atakayepata shida kutokana na hali mbaya ya umaskini.

Kabla ya hapo Bw. Ban Ki-moon alitoa hotuba iliyoandikwa kwa ajili ya siku ya kutokomeza umaskini duniani ikisema, watu maskini wanatamani kutokomeza umaskini kuliko mtu yeyote mwingine, lakini mara kwa mara wanakosa maelekezo, vyombo na nafasi za kazi. Jukumu la jumuiya ya kimataifa ni kutoa msaada katika upande huo. Hivyo kauli-mbiu ya siku ya kutokomeza umaskini duniani ya mwaka huu ni "watu maskini wanamageuzi".

Lengo muhimu la maendeleo ya milenia la Umoja wa Mataifa ni kupunguza nusu ya idadi ya watu maskini ifikapo mwaka 2015. Kuhusu suala hilo Bw. Ban Ki-moon alisema, kufuatana na hali ya maendeleo ya hivi sasa, lengo hilo linaweza kutimizwa kwa wakati huo. Lakini maendeleo ya dunia hayana uwiano, baadhi ya sehemu hususan sehemu ya Afrika kusini mwa Sahara, bado zinakabiliwa na changamoto kali. Alitoa wito wa kutaka jumuiya ya kimataifa lazima ifuatilie na kuweka raslimali katika sehemu zilizo nyuma kimaendeleo pamoja na watu wake. Ofisa wa Umoja wa Mataifa Bw. Rachel Miahnja kwa niaba ya naibu katibu mkuu anayeshughulikia mambo ya uchumi na jamii Bw. Sha Zukang, alitoa hotuba, akisema,

"Tunakabiliwa na jukumu kubwa na gumu, ingawa hivi sasa tumefanya juhudi kubwa, lakini bado kuna mtu mmoja kati ya kila watu watano, ambaye anahangaika kutokana na umaskini."

Ili kuhimiza jitihada za kupunguza idadi ya watu maskini duniani, Umoja wa Mataifa umethibitisha kipindi cha kutoka mwaka 1997 hadi mwaka 2006 kuwa ni miaka kumi ya kwanza ya kutokomeza umaskini duniani. Na kuamua tarehe 17 mwezi Oktoba kuwa ni "siku ya kutokomeza umaskini duniani".

Wakati Umoja wa Mataifa unapofanya shughuli za maadhimisho, uwanja ulioko katikati ya mji wa New York na miji ya nchi nyingine pia ilifanya shughuli za maadhimisho.