Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-22 15:30:29    
Sehemu ya mazingira ya asili yenye thamani ya Shennongjia

cri

Shennongjia iliyoko kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya mkoa wa Hubei, katikati ya China, ni sehemu ya misitu minene ya asili yenye mimea aina zaidi ya 3,700 na wanakoishi wanyama zaidi ya aina 1,000. Sehemu hiyo inasifiwa kama ni ghala pekee lililohifadhi vizuri Jini(gene) za wanyama na mimea.

Jina la Shennongjia linatokana na hadithi moja ya kale. Katika kipindi cha jamii ya asili, maambukizi ya maradhi na njaa yaliwasumbua binadamu. Ili kuwaokoa watu, mfalme yandi Shen Nongshi alionja mimea ya aina mbalimbali, na kuchagua mbegu na kuzipanda. Alipofika kwenye msitu mnene na mlima mkubwa ya mkoani Hubei, alizuiliwa na magenge yaliyochongoka sana. Hivyo Shen nongshi alijenga ngazi 36, na alifaulu kupanda juu. Tokea wakati ule, mahali hapo paliitwa Shennongjia. Hapo baadaye iliota miti mingi na kuwa msitu mnene.

Eneo la Shennongjia ni zaidi ya kilomita 3,200, na karibu 70% yake ni msitu, mzee Lei Jinguang ana umri karibu miaka 70, alipokuwa na umri wa miaka 20 alikwenda kufanya kazi ya kukata miti kwenye sehemu ya Shennongjia. Alipoeleza hali ya hapo awali ya Shennongjia, alisema,

"Wakati ule Shennongjia ilikuwa ni sehemu yenye msitu wa asili wenye wanyama wengi wakiwemo chui na dubu weupe"

Mandhari ya milima na misitu ya Shennongjia ni nzuri sana, na ni raslimali kubwa ya utalii. Mandhari nzuri ya Shennongjia inatokana na mambo matatu: Kwanza ni miti mikubwa ya asili iliyohifadhiwa vizuri, ambapo ndege wa aina nyingi wanaishi, na watu wanaweza kusikia milio yao ya kuburudisha. Pili, katika hadithi Shennongjia, ni mahali ambapo Shennongshi alijenga ngazi na kuchimba dawa za miti-shamba. Na tatu, Shennongjia ina mambo mengi yasiyofahamika, inasemekana kuwa huko wanaishi 'binadamu pori'.

Kutokana na kuathiriwa na upepo wa kusini mashariki unaoleta unyevunyevu mwingi, milima mikubwa na misitu minene, hali ya hewa ya huko ni joto, wala siyo baridi sana katika majira ya baridi. Aidha sehemu ya Shennongjia ina mfumo mzuri wa kupatana kwa viumbe kwenye misitu minene. Mfumo mzuri wa viumbe, aina nyingi za mimea na wanyama, hali ya hewa isiyo ya baridi, hivyo inasifiwa kuwa "ni ghala la kijani" na "hifadhi ya asili ya wanyama na mimea".

Kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu wanachukuliwa kuwa ni (gene) jini kwenye sehemu ya Shennongjia, na ni wanyama walio kwenye hatari ya kutoweka hapa duniani, ambao wanaishi katika mazingira machache tu yanayoweza kutimiza matakwa yao. Katika miaka ya hivi karibuni, mazingira ya viumbe ya sehemu ya Shennongjia imekuwa inaboreshwa siku hadi siku, idadi ya kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 1,200 kwa hivi sasa, kutoka zaidi ya 600 tu ya wakati idadi ya kima hao ilipungua kwa kiwango kikubwa, na kuwa wanyama wanaowavutia watalii zaidi kwenye sehemu hiyo. Kila mara Bw. Qian Yuankun, ambaye ni ofisa wa serikali ya huko, anaposikia milio ya kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu, anafurahi sana akisema,

"Baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi kuwa kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu wanaokaribia kutoweka kwenye sehemu ya Shennongjia, wanashindwa kuishi kwenye sehemu hiyo, na Shennongjia vilevile itazorota hadi kutoweka, sasa tunaweza kusema, China imeihifadhi ipasavyo sehemu ya Shennongjia, na idadi ya kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu inaongezeka kwa mfululizo, maeneo ya shughuli za maisha yao yanapanuka hatua kwa hatua, katika siku za baadaye Shennongjia itakuwa maskani yenye mazingira mazuri na ya kupatana kati ya binadamu na maumbile ya asili."

Mwanzoni mwa miaka ya 90, wakati serikali ya sehemu ya misitu ya Shennongjia ilipotoa kipaumbele katika hifadhi ya Shennongjia, iliendeleza ipasavyo sekta ya utalii wa viumbe. Hivi sasa sehemu ya misitu imeendelezwa kuwa sehemu nne zenye mandhari nzuri, ambazo zinapokea watalii zaidi ya laki 6 kwa mwaka. Maendeleo ya utalii yanahimiza maendeleo ya sekta husika. Mfanyakazi wa idara ya misitu Bw. Li Shikai amejenga nyumba ya wageni, katika majira ya joto huwa anapata wateja wengi, Bw. Li alisema,

"Tangu tulipoanza kuendeleza utalii wa viumbe, hali ya Shennongjia inakuwa nzuri siku hadi siku, watalii wengi wanaitembelea sehemu hiyo katika majira ya joto, kwa hiyo niliomba mkopo na kujenga nyumba ya wageni, katika miaka ya hivi karibuni pato letu liliongezeka kwa mfululizo."

Ustawishaji wa utalii unaleta pato kubwa kwa wakazi wa sehemu ya misitu, lakini pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watalii, mazingira ya viumbe ya sehemu ya misitu yanakabiliwa na shinikizo kubwa. Ofisa wa serikali ya huko Bw. Qian Yuankun alisema,

"Wakati tunapokuza maendeleo ya uchumi na jamii ya Shennongjia, tumekuwa tukitoa kipaumbele katika hifadhi ya mazingira ya viumbe, na kutatua vizuri mgongano kati ya maendeleo ya uchumi na hifadhi ya mazingira ya asili."

Bw. Qian Yuankun alisema, shughuli za utalii zilisimamishwa kwa mara ya kwanza kwa muda wa miezi 3 mwanzoni mwa mwaka 2006. Lengo letu lilikuwa ni kutoa muda wa mapumziko na marekebisho kwa wanyama zaidi ya aina 1,000 wa huko, na kurejea kwenye hali nzuri kwa mazingira ya kupatana kwa viumbe kwenye sehemu hiyo, ambayo inasifiwa kuwa ni "ghala la (gene)jini za mbegu za viumbe la nchini China".

Mradi wa hifadhi ya misitu ya asili ya Shennongjia ulizinduliwa miaka mingi iliyopita, miti ya sehemu hiyo inapigwa marufuku kukatwa ili kuhifadhi sehemu ya Shennongjia, ambayo inaitwa na wanasanayasi kuwa ni "ghala la kijani", na "ghala la jini za mbegu za viumbe ya duniani". Sasa mazingira ya viumbe ya Shennongjia yanaanza kurejea katika hali nzuri polepole. Mlinzi wa misitu Bibi Jiang Lingling alisema,

"Tangu mradi wa hifadhi ya misitu ya asili mwaka 2000 uanze kutekelezwa, baadhi ya wanyama wakiwemo kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu, kuku wenye manyoya ya rangi nyekundu sehemu ya kifuani na mbuzi mwitu, wameonekana, sasa maji yamebadilika kuwa maangavu na milima imebadilika kuwa na rangi ya kijani."

Idhaa ya kiswahili 2007-10-22