Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-24 20:10:07    
Mapishi ya supu ya matango ya baharini na pilipili manga

cri

Mahitaji

Matango gramu 750, pilipili manga gramu 3, vipande vya vitunguu maji gramu 25, mvinyo wa kupikia gramu 15, chumvi gramu 4, chembechembe za kukoleza ladha gramu 5, tangawizi gramu 10, kiasi kidogo cha giligilani, mafuta ya ufuta na mchuzi wa sosi.

Njia

1. osha matango , halafu uyakate yawe vipande vipande. Chemsha maji, halafu weka vipande vya matango kwenye maji ya moto.

2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria halafu tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, mimina maji, mvinyo wa kupikia, chembechembe cha kukoleza ladha, mchuzi wa sosi, chumvi na pilipili manga, korogakoroga, halafu tia vipande vya matango korogakoroga. Baada ya kuchemka ipakue kwenye bakuli. Mimina mafuta ya ufuta, weka vipande vya vitunguu maji na giligilani. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari.