Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-25 16:19:41    
Idadi ya watoto wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria yapungua

cri

Ugonjwa wa malaria ni ugonjwa unaosababisha vifo vya watu wengi barani Afrika. Takwimu kutoka Shirika la Afya duniani WHO zinasema kila mwaka watu zaidi ya milioni moja duniani wanakufa kwa ugonjwa wa malaria, wengi kati yao wako katika nchi zilizoko kusini mwa Sahara. Ugonjwa huo unasababisha vifo vingi vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kuliko watu wengine. Msumbiji ni nchi yenye watoto wengi zaidi wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria duniani. Lakini kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali za nchi mbalimbali za Afrika na jumuiya ya kimataifa, hali hii imebadilika. Idadi ya watoto wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria inapungua.

Ofisa husika wa kituo cha utafiti wa afya cha Msumbiji hivi karibuni alisema, majaribio yao ya kutumia chanjo ya ugonjwa wa malaria kwa watoto yamepata mafanikio na matokeo husika ya utafiti yametangazwa kwenye gazeti moja la Uingereza.

Habari zinasema Profesa Pedro Alonso wa kituo hicho alisema, wataalamu walifanya majaribio ya kutumia chanjo hiyo kwa watoto wa Msumbiji wenye umri wa miezi 8 hadi miezi 16, na usalama wa chanjo hii unafuatiliwa sana na wataalamu hao.

Profesa Alonso alisema watoto wote waliopata chanjo hiyo hawakupata magonjwa mengine na kiasi cha watoto kuambukizwa ugonjwa wa malaria kimepungua kwa asilimia 65. Lakini watoto hao si kama tu walitumia chanjo hiyo kupambana na malaria, bali pia walitumia vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu. Wataalamu walisema hata kama chanjo ya malaria itafanikiwa, inapaswa kutumia vyandarua, dawa ya mbu na njia nyingine za kukinga ugonjwa wa malaria kwa wakati mmoja.

Habari nyingine zinasema serikali ya Kenya ilitoa takwimu ikionesha kuwa, kutokana na matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu, kiasi cha watoto wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria wenye umri chini ya miaka mitano kimepungua kwa asilimia 44 kuliko miaka mitano iliyopita.

Taarifa kutoka wizara ya afya ya Kenya zinasema, kuanzia mwaka 2002 serikali ya Kenya imetoa vyandarua milioni 13.4 vyenye dawa ya kuua mbu, kwa watoto na wajawazito nchini Kenya. Taarifa zinasema matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu yanasaidia kuzuia vifo vya watoto 7 kutokana na ugonjwa wa malaria.

Shirika la UNICEF na shirika la "wenzi wa kupambana na malaria" yalitoa ripoti kwa pamoja kuwa, kutokana na nchi nyingine za Afrika kutumia vyandarua vyenye dawa ya mbu na kueneza dawa mpya za kutibu malaria, katika miaka ya hivi karibuni operesheni ya kinga na tiba ya malaria katika nchi za Afrika imepata maendeleo.

Ripoti zinasema kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2006 idadi ya uzalishaji wa vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu imeongezeka na kuwa milioni 63 kutoka milioni 30. Katika miaka miwili iliyopita, idadi ya vyandarua vilivyotolewa na mashirika mbalimbali duniani pia iliongezeka. Mwaka 2006 shirika la UNICEF lilitoa vyandarua milioni 25 ambavyo ni mara tatu ya vile vya mwaka 2004.

Ripoti hiyo pia inasema katika nchi 20 zilizoko kusini mwa Sahara, nchi 16 zimetoa vyandarua zaidi ya mara 3 ya idadi ya mwaka 2000. Aidha, karibu nusu ya nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara zimeanza kutumia dawa ya Cotexin badala ya dawa zenye ufanisi mdogo.

Katika mkutano wa Beijing wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana, rais Hu Jintao wa China alitangaza kuwa China itazisaidia nchi za Afrika kujenga hospitali 30, na kutoa Yuan zaidi ya milioni 300 kuzisaidia nchi za Afrika kukinga na kutibu ugonjwa wa malaria, kutoa dawa za Cotexin na kuanzisha vituo 30 vya kinga na tiba ya malaria.

Hivi sasa China imefanya semina ya kwanza ya wataalamu wa China kuhusu ugonjwa wa malaria watakwenda Afrika, na wataalam 60 watakwenda kwenye nchi mbalimbali za Afrika kuzisaidia kujenga vituo vya kinga na kutibu malaria na kuwaandaa watu wa Afrika wenye ujuzi wa kinga na tiba ya malaria ndani ya mwaka huu.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-25