Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-30 16:13:44    
Mkutano wa Doha kuhusu matumizi ya gesi wahimiza maendeleo ya nishati safi

cri

Mkutano wa sita kuhusu matumizi ya gesi ulifunguliwa tarehe 29 mjini Doha, maofisa na wataalamu karibu elfu moja kutoka sekta mbalimbali walihudhuria mkutano huo. Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Gesi--nishati ya karne ya 21", mkutano huo unasisitiza umuhimu wa matumizi ya nishati safi katika siku za baadaye.

Washiriki wa mkutano huo wa siku nne wana matumaini kuwa wataafikiana katika maoni mengi, ili kuleta nafasi kubwa ya maendeleo na matumizi ya gesi. Washiriki wanaona kuwa matumizi ya gesi ni njia pekee ya kuhakikisha mazingira safi. Mtaalamu wa matumizi ya gesi kutoka Algeria Bw. Salman Fikry alisema,

"Sote tunafahamu kwamba gesi ni nishati safi, ni rahisi kusafirisha kati ya mataifa na bei yake ni ya chini. Ni sawa kusema kwamba gesi itakuwa nishati muhimu siku baada ya siku kadiri muda unavyopita katika karne ya 21, na maendeleo ya viwanda vya gesi siyo tu yatasaidia kuleta mazingira safi bali pia yatakuwa nguvu kubwa ya kusukuma mbele uchumi duniani."

Gesi ni nishati isiyo na rangi wala na sumu, na joto lake ni kubwa na haina uchafuzi, sifa yake kubwa ni safi na haichafui mazingira, wakati nchi zote zinapotilia mkazo mazingira safi, nishati hiyo inafuatiliwa sana. Katika miaka ya hivi karibuni, bei ya mafuta imekuwa inapanda kwa kasi na sasa imezidi dola za Kimarekani 93 kwa pipa. Hali hiyo inazipasa nchi zinazotumia nishati kwa wingi kutafuta nishati mbadala, kwa hiyo nishati ya gesi ambayo bei yake iko chini na inaweza kukidhi mahitaji ya mazingira safi, imekuwa nishati muhimu inayotumainiwa na nchi zote. Hali hiyo imeiletea gesi nafasi kubwa ya maendeleo. Bw. Salman Fikry aliendelea kusema,

"Nchi nyingi zimepanga gesi kwenye ratiba ya maendeleo au matumizi ya gesi na kutunga mkakati na zimekuwa tayari kuendeleza mradi wa maendeleo na biashara ya gesi. Mkutano huu unawashirikisha wasimamizi na wataalamu wengi wa gesi, na kujadiliana mkakati wa maendeleo ya gesi, naamini kuwa mustakabali wa matumizi ya gesi duniani utakuwa mzuri."

Pamoja na kuwa na matumaini na mustakabali mzuri wa matumizi ya gesi duniani, wataalamu wa nchi mbalimbali walijadiliana kwa kina kuhusu maendeleo ya viwanda vya gesi, wanaona kuwa ikilinganishwa na matumizi ya mafuta, maendeleo ya gesi na kiwango chake cha soko duniani vinatakiwa kuendelezwa zaidi. Bw. Ibrahim Al-Ibrahim, mshauri wa kiuchumi wa rais wa Qatar alipozungumzia maendeleo ya viwanda vya gesi alisema,

"Maendeleo ya biashara ya kimataifa ya mafuta yanatokana na sifa ya mafuta, biashara ya gesi inakwenda polepole kutokana na dosari mbalimbali za sokoni, kwa hiyo kuna ni haja kufanya juhudi ili kukamilisha soko hilo na kuendeleza biashara hiyo."

Rais wa Qatar, nchi mwenyeji wa mkutano huo, Bw. Sheikh Hamad Bin Khalifa Al Thani alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo, alisisitiza kuwa katika miongo kadhaa iliyopita yametokea mabadiliko makubwa katika sekta ya nishati, watu wanatakiwa kufikiria upya athari ya matumizi ya makaa ya mawe na kuifanya gesi iwe nishati muhimu. Alisema Qatar itafanya juhudi kubwa kuendeleza gesi na kuiuza nchi za nje. Alisema,

"Kwa makadirio yetu, mwaka huu tani milioni 31 za gesi ya Qatar zitasafirishwa nje. Kuanzia mwaka 2010 idadi hiyo itafikia hadi tani milioni 77, na idadi hiyo ni theluthi moja ya matumizi yote ya gesi duniani. Qatar ikiwa ni nchi inayozalisha gesi kwa wingi itaendeleza nishati hiyo kwa mujibu wa mahitaji ya soko la kimataifa."