Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-31 16:41:54    
Mapishi ya kuchemsha doufu pamoja na sosi ya pilipili hoho

cri

Mahitaji:

Doufu gramu 100, viazi gramu 20, sosi ya pilipili hoho gramu 5, chumvi gramu 2, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, pilipili manga gramu 2, vitunguu maji gramu 15, tangawizi gramu 15.

Njia:

1. kata doufu iwe vipande vipande, na kata viazi viwe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi korogakoroga, tia sosi ya pilipili hoho korogakoroga halafu tia vipande vya doufu korogakoroga mimina maji na tia vipande vya viazi, baada ya kuchemsha kwa dakika 5, tia chumvi, pilipili manga, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.