Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-05 18:44:01    
Ushirikiano kati ya China na Afrika waongeza uchangamfu wa shughuli za mawasiliano ya habari barani Afrika

cri

Mmkutano wa wakuu wa "kuunganisha Afrika" ulioandaliwa na mashirikisho kadhaa likiwemo Shirikisho la Mawasiliano ya Habari Duniani (ITU) lilifungwa hivi karibuni huko Kigali, Rwanda. Lengo la mkutano huo ni kustawisha shughuli za mawasiliano ya habari barani Afrika, kuondoa pengo katika mawasiliano ya kitarakimu, na kuboresha mazingira ya uwekezaji. Naibu katibu mkuu wa Shirikisho la Mawasiliano ya Habari Duniani Bw. Zhao Houlin alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, mkutano huo ulipata mafanikio makubwa, na nchi za Afrika zimeonesha matumaini makubwa ya kushirikiana, kujitegemea na kupata maendeleo ya pamoja. Alisema,

"Nchi za Afrika zina matumaini makubwa ya kujiendeleza, na zinatumai kujiendeleza kwa kujitegemea, wala siyo kusubiri uhisani na kufanya kazi kwa mujibu wa maslahi ya wahisani. Zilisema hazipendi uhisani, zinataka kushirikiana na kupata maendeleo ya pamoja. China imefanya vizuri katika jambo hilo. Mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mjini Beijing mwaka jana umefanya kazi kubwa katika kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika, kuzisaidia nchi za Afrika zishirikiane, na kuboresha mazingira ya uwekezaji barani Afrika."

takwimu zinaonesha kuwa, bara la Afrika ni sehemu ambayo shughuli za mawasiliano ya habari ziko nyuma zaidi duniani. Hivi sasa asilimia 70 ya watu wanatumia mtandao wa Interent kupitia waya ya simu, chini ya asilimia 1 ya watu wanatumia Broadband. Ili kubadilisha hali hiyo, Shirikisho la Mawasiliano ya Habari Duniani limetunga mpango wa "kuunganisha Afrika", ambao unalenga kuvisaidia vijiji vyote vya Afrika viweze kutumia mtandao wa Internet ifikapo mwaka 2015. Bw. Zhao Houlin alisema makampuni ya China imefanya kazi kubwa kwa maendeleo ya shughuli za mawasiliano ya habari barani Afrika. Kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya China na Afrika bila shaka kutasukuma mbele maendeleo ya Afrika.

Mwishoni mwa miaka ya 90 karne iliyopita, makampuni ya vyombo vya upashanaji habari ya China ilianza kuingia soko la Afrika. Hivi sasa kampuni ya Huawei na kampuni ya ZTE ambayo ni makampuni makubwa mawili ya vyombo vya upashanaji habari ya China yameanzisha shughuli zao katika nchi 35 za Afrika, kujenga ofisi zaidi ya 20 barani Afrika, na kubwa makampuni muhimu ya utengenezaji wa vyombo vya upashanaji habari katika nchi kadhaa. Bw. Zhao Houlin alisema alipowasiliana na watu wa Afrika, alifahamu kuwa mafanikio ya makampuni ya China barani Afrika yanatokana na sifa nzuri ya China na sera za China kuhusu Afrika. Alisema,

"Nchi za Afrika zinaona kuwa, China inaisaidia Afrika kama ni marafiki na ndugu, ambayo ni tofauti na Marekani na Ulaya; tena China inatoa misaada bila ya malengo ya kibiashara, lakini Marekani na Ulaya zinatoa misaada yenye masharti mengi kutokana na malengo ya kibiashara. Pia China inafuta madeni ya nchi za Afrika na kupunguza mzigo wao mara kwa mara."

Bw. Zhao Houlin anaona kuwa, bidhaa za makampuni ya China zina uwezo mkubwa wa ushindani masokoni, urafiki na kuwajibika kwa wafanyakazi wa China kumeyapatia makampuni ya China sifa nzuri. Alisema,

"Sifa za bidhaa zinazotengenzwa na makampuni ya China ni sawa na bidhaa za nchi nyingine, lakini bei za bidhaa za China ni nafuu zaidi, hivyo nchi za Afrika zinapenda kutumia bidhaa za China. Marafiki wa Afrika waliwahi kuniambia, wahandisi wa China wanazisaidia nchi za Afrika kwa udhati, wana hamu kubwa ya kujibu maswali ya Waafrika."