"Mwaka wa China" uliofanyika nchini Russia kwa mwaka mzima ulimalizika tarehe 6, hadi kufikia hapo miaka miwili ya taifa ya China na Russia imemalizika. Siku hiyo waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao na waziri mkuu wa Russia Bw. Viktor Zubkov walihudhuria sherehe ya kufungwa kwa mwaka huo wa China kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow.
Mwezi Novemba ingawa Moscow imeingia katika majira ya baridi, lakini joto la ushirikiano na maingiliano kati ya China na Russia ni kubwa, tarehe 6 ukumbi wa ikulu ya Kremlin ulijaa urafiki mkubwa. Jioni saa moja waziri mkuu wa China Bw Wen Jiabao na waziri mkuu wa Russia Bw. Viktor Zubkov walifika ukumbini pamoja kuhudhuria sherehe ya kufungwa kwa mwaka wa China nchini Russia huku muziki ukipigwa.
Kwenye sherehe kwanza Bw. Wen Jiabao alitoa hotuba akisema, "mwaka wa taifa" umeimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili kwa kina, umehimiza zaidi ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Russia na umetimiza lengo la kuinua kiwango cha kuaminiana kisiasa na ushirikiano halisi kati ya nchi hizo. Alisema,
"China na Russia kuwa na mwaka wa taifa kwa kila upande, ni hatua muhimu za nchi mbili kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimkakati na wa kiwenzi, ni jambo jipya kabisa katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili."
Bw. Wen Jiabao alisema China na Russia ni nchi kubwa jirani, ni wenzi wa kimkakati katika dhiki na faraja, kuendeleza kwa dhati uhusiano wa kimkakati na wa kiwenzi na kuimarisha urafiki, ushirikiano wa kunufaishana na ujirani mwema ni matumaini ya watu wote wa nchi hizo mbili. Alisema ingawa "mwaka wa taifa" wa China na wa Russia umemalizika, lakini moyo wa "kuendelea na urafiki na kusonga mbele kwa kushikana mikono" utarithishwa kizazi hadi kizazi, aina hiyo mpya ya kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili itakuwa mali kubwa katika uhusiano wa China na Russia. Bw. Wen Jiabao alipomaliza hotuba yake alinukuu maneno aliyosema mwanafasihi mkubwa duniani kuonesha matumaini yake kuhusu uhusiano kati ya China na Russia. Alisema,
"'Urafiki unaleta furaha, ustaarabu unaleta mapatano'. Ushirikiano unasukuma mbele maendeleo. Tushikane mikono, tuaminiane, tuungane na tushirikiane, tujitahidi kwa pamoja kupata mustakabali mzuri wa urafiki na ujirani mwema kati ya China na Russia".
Na waziri mkuu wa Russia Bw. Viktor Zubkov alisema,
"Shughuli za mwaka wa taifa zimeandika ukurasa mzuri katika historia ndefu kati ya China na Russia. Leo ni siku ya kumalizika kwa mwaka wa China nchini Russia, tumefunga ukurasa huo wa kihistoria, lakini tunapomaliza ukurasa huo tuna nia ya kufungua ukurasa unaong'ara zaidi katika uhusiano kati ya nchi zetu mbili".
Baada ya hotuba mawaziri hao wawili wakiwa pamoja na watu zaidi ya 5000 kutoka fani mbalimbali waliburudika na muziki uliopigwa na Kundi la Simfoni la China.
Mwaka wa taifa uliofanywa nchini China na Russia ulipendekezwa na viongozi wa nchi mbili. Kwa mujibu wa hesabu, katika muda wa mwaka wa taifa, pande mbili zilifanya shughuli zaidi ya 500 zikihusu mambo ya siasa, biashara na utamaduni. Mtaalamu wa Taasisi ya Sayansi ya Kijamii Bw. Jiang Yi alisema,
"Ingawa 'mwaka wa taifa' uliongozwa na serikali, lakini shughuli za mwaka huo ni za mashirika ya kiraia na maingiliano ya kiraia kati ya nchi mbili.
|