Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-07 20:05:31    
Kuimarisha ujirani mwema na urafiki na kuhimiza ushirikiano halisi

cri

Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao amerudi Beijing tarehe 7 asubuhi baada ya kumaliza ziara yake katika nchi 4 za Ulaya na Asia. Wakati wa kumaliza ziara yake katika nchi hizo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi ambaye alifuatana na waziri mkuu katika ziara yake hiyo alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, ziara ya waziri mkuu Bw. Wen Jiabao imeimarisha uhusiano wa ujirani mwema na urafiki kati ya China na Uzbekistan, Turkmenistan, Belarus na Russia.

Wakati wa ziara yake, waziri mkuu Wen Jiabao alipohudhuria Mkutano wa 6 wa mawaziri wakuu wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai, alitoa mapendekezo halisi kuhusu kuzidisha na kupanua ushirikiano kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo, akishauri kuimarisha uratibu wa sheria na sera za nchi wanachama, kuboresha siku hadi siku mazingira ya biashara na uwekezaji, kuanzisha na kukamilisha utaratibu wa ushirikiano wa kiuchumi. Aidha alisisitiza kuwa nchi wanachama zinapaswa kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za uchumi na biashara, kilimo, nishati, mawasiliano, na mawasiliano ya habari, kuhamasisha kampuni za kila upande kuwekeza kwenye nchi wanachama na kufanya ushirikiano, kufanya juhudi kubwa za kuhimiza maingiliano na ushirikiano kwenye sekta za sayansi na teknolojia, elimu na uhifadhi wa mazingira. Hasa alitoa mwito wa kuzitaka nchi wanachama zitekeleze makubaliano na maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati yao katika miaka ya hivi karibuni.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Yang Jiechi amesema, mapendekezo mbalimbali aliyotoa Bw. Wen Jiabao yamehimiza ushirikiano halisi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai, ambayo yamekubaliwa na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria Mkutano huo, ambao wameeleza kwa kauli moja kuwa, kuendeleza kwa kina ushirikiano halisi na kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja ni matumaini ya pamoja ya nchi zote wanachama, pia ni kazi muhimu ya kudumisha nguvu ya uhai ya Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai.

Waziri Yang amesema, wakati wa ziara yake nchini Russia, viongozi wa China na Russia wamefikia maoni ya pamoja kuhusu kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Russia, na wamesaini nyaraka mbalimbali kuhusu ushirikiano. Alipokutana na viongozi wa Russia, Bw. Wen Jiabao alisisitiza kuwa, upande wa China utatekeleza kwa kina wazo la amani na maendeleo ili wananchi wa China na Russia wawe na urafiki kizazi baada ya kizazi na kusonga mbele kwa pamoja, kuimarisha msingi wa kisiasa wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha msingi wa kimali wa ushirikiano huo, na kuimarisha msingi wa jamii wa ushirikiano huo, kuufanya msingi wa usalama wa ushirikiano huo uwe imara zaidi, na kuongeza uratibu zaidi katika mambo ya kimataifa ili kuimarisha ushirikiano wa kimkakati. Upande wa Russia pia umesisitiza kuwa, Russia itaendelea kufanya juhudi katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Russia na China, kufanya ushirikiano wa muda mrefu na wa utulivu kati yake na China. Aidha, pande mbili pia zimefikia maoni ya pamoja kuhusu kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za uchumi na biashara, ili ushirikiano huo uendelezwe kwa uwiano kwenye kiwango cha juu zaidi.

Kutokana na maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati ya viongozi wakuu wa China na Russia, shughuli za "Mwaka wa Russia" nchini China na "Mwaka wa China" nchini Russia zilifanyika tokea mwaka 2006, shughuli hizo zimehimiza maingiliano na ushirikiano kati yao kwenye sekta mbalimbali. Katika ziara yake ya safari hii nchini Russia, mawaziri wakuu na China na Russia walihudhuria ufungaji wa shughuli za "Mwaka wa China" nchini Russia, pande hizo mbili zilisifu sana matokeo kemkem na umuhimu mkubwa wa shughuli za "Mwaka wa China" nchini Russian na "Mwaka wa Russia" nchini China, na kuamua kuweka taratibu mbalimbali za kufanya shughuli mbalimbali zinazowafurahisha wananchi wa nchi hizo mbili kila baada ya muda fulani.

Waziri Yang Jiechi amesema, nchi tatu za Uzbekistan, Turkmenistan na Belarus zote zimetilia maanani sana ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao, ambapo China na nchi hizo tatu zimesaini nyaraka mbalimbali za ushirikiano wa pande mbili mbili. Bw. Wen Jiabao alipokutana na kuwa na mazungumzo na viongozi wa nchi hizo tatu, alisisitiza kuwa China inaheshimu njia ya maendeleo waliyochagua wananchi wa nchi hizo tatu, na kuunga mkono juhudi zao. Pia amependekeza kuinua kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi hizo tatu.