Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-07 20:12:02    
Mapishi ya samaki kwa moshi

cri

Mahitaji:

Samaki mmoja, chumvi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, vitunguu maji na vitunguu saumu kila gramu 5, chai kijiko kimoja, mchele vijiko viwili, pilipili manga gramu 5, sukari vijiko viwili, asali vijiko viwili.

Njia?

1. Kata samaki awe vipande vipande, ondoa kichwa na mkia wake. Koroga pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, vipande vya vitunguu maji na vitunguu saumu.

2. washa moto , tia mafuta kwenye sufuria, tia pilipili manga kwenye sufuria, ikaange, halafu ipakue. Mpaka mafuta yawe na joto la nyuzi 70, tia vipande vya samaki kwenye sufuria, vikaange, halafu vipakue. Mpaka mafuta yawe joto la nyuzi 100, tia vipande vya samaki kwenye sufuria tena, vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi vipakue. Halafu tia asali kwenye vipande vya samaki. Weka kwenye sahani.

3. osha sufuria, washa moto kiasi tia majani ya chai, mchele, pilipili manga na sukari, korogakoroga, mpaka moshi utokee, weka sahani kwenye sufuria, endelea kukoroga chai, mchele, pilipili manga na sukari, halafu zima moto na funika kifuniko. Baada ya dakika 5 vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.