Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-08 19:40:28    
Mkoa wa Sichuan waanzisha mradi wa kutoa mafunzo kwa wakulima wanawake vijijini

cri

 kutokana na kutokuwepo kwa uwiano kwenye maendeleo ya uchumi na jamii nchini China, sehemu za vijijini nchini China zinakabiliwa na matatizo mengi kama vile mazingira mabaya ya shule na kiwango cha chini cha ufundishaji kwa walimu wa vijijini. Ili kuwafanya watoto wa vijijini waweze kupata elimu sawa na wanafunzi wa mijini, idara za elimu za China zinawatia moyo walimu wenye kiwango cha juu cha ufundishaji kwenda vijijini, na kutoa mafunzo mbalimbali kwa walimu wa vijijini.

Wasikilizaji wapendwa, mliowasikia ni walimu wanawake zaidi ya 30 kutoka shule za vijijini mkoani Sichuan ambao walikuwa wanafundishwa lugha ya kiingereza na mtaalamu kutoka nje. Mradi huo wa kuwaandaa walimu wanawake vijijini ulianzishwa mwaka 2003. Kila mwaka walimu wanawake 30 kutoka sehemu zenye matatizo ya kiuchumi walipata mafunzo ya mwaka mmoja bila malipo. Wataalamu wa nchini na nchi za nje waliwaandaa kwa makini, masomo hayo ni pamoja na Kiingereza, kompyuta, mbinu za ufundishaji, saikolojia ya elimu, falsafa n.k.. Hadi sasa walimu wanawake zaidi mia moja wa vijijini wamepata mafunzo hayo.

Ingawa semina hiyo ni ya mwaka mmoja tu, lakini kiwango cha ufundishaji cha walimu waliopata mafunzo kimeinuka sana. Bibi. Kemucuo ni mwalimu wa shule ya msingi ya kikabila katika tarafa inayojiendesha ya kabila la watibet ya Ganzi mkoani Sichuan. Kabla ya kushiriki kwenye semina hiyo, alikuwa hawezi kuongea vizuri Kichina, sembuse kujua herufi za Kiingereza. Lakini baada ya nusu mwaka, Bibi. Kemucuo anaweza kuzungumza kwa Kiingereza na mwalimu wake. Alisema:

"mwanzoni mimi nilikuwa nyuma vibaya zaidi kuliko wanafunzi wengine, lakini sasa ninaweza kutumia Kingereza rahisi kuwasiliana na mwalimu wangu."

Siyo tu bibi Kemucuo anapata maendeleo. Mwalimu wa semina hiyo Bibi Li Wei anakumbuka kuwa, katika semina ya kwanza ya mwaka 2003, hakukuwa na mwanafunzi hata mmoja aliyeweza kusoma kwa kufuatana naye, wengi kati ya wanafunzi hao hawakuwezi kuelewa Kiingereza hata kidogo. Lakini baada ya wiki kadhaa, wanafunzi hao walianza kuelewa maneno ya kawaida darasani, na baada ya nusu mwaka waliweza kusoma makala ya Kiingereza, hata baadhi yao waliweza kuandika makala kwa Kiingereza.

Mwalimu Peng Anying alituambia kuwa, zamani shule yake haikuwa na somo la Kiingereza, baada ya kupata mafunzo alirudi kwenye shule yake na kuanzisha somo la lugha ya Kiingereza, watoto wanapenda sana. Alisema:

"sehemu yetu ni moja ya sehemu zilizoko nyuma kiuchumi. Watoto hao walikuwa hawajifunzi Kiingereza. Nilianzisha somo la Kiingereza, watoto hao wanapenda sana na kujifunza kwa makini."

Akiwa mwandaaji wa mradi huo Bw. Qin Guangya aliridhika na mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo. Alisema mradi huo ni majaribio ya aina mpya, pia ni maonesho ya kuhimiza usawa kupewa wa elimu. Mradi huo unatoa mchango katika kuboresha hali ya elimu katika sehemu zenye matatizo ya kiuchumi mkoani Sichuan.

Bw. Qin Guangya alifikiri kuwa kila mwalimu anayepata mafunzo anaweza kuwafundisha wanafunzi mia 5. Hivyo baada ya miaka kadhaa, kiwango cha ufundishaji wa sehemu zenye matatizo ya kiuchumi mkoani Sichuan kitainuka sana.