Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-13 21:08:29    
Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zajitahidi kufanikisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati

cri

Waziri wa mambo ya nje wa Misri tarehe 12 alisema Misri itajitahidi kufanikisha mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati. Siku hiyo katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Amr Moussa pia alisisitiza kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ina matumaini kuwa mkutano huo kuhusu amani ya Mashariki ya Kati, unaweza kufanyika na kupata matokeo yanayotarajiwa katika muda uliowekwa, ili kuufanya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati upate maendeleo ya kweli. Yote hayo yameonesha kuwa Misri na nchi za Kiarabu zina nia sana ya kuona amani ya Mashariki ya Kati.

Awali Rais George Bush wa Marekani alipendekeza mkutano huo wa kimataifa ufanyike tarehe 26 Novemba, lakini kutokana na kuwa nchi za Kiarabu zilikuwa na maoni tofauti kuhusu ajenda za mkutano huo, hadi sasa tarehe ya kufanyika kwa mkutano huo bado haijabainika. Sababu za Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuwa na matumaini makubwa juu ya mkutano huo ni kama zifuatazo.

Kwanza, Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zinataka kuvunja hali ya kukwama kwa mkutano huo, ili mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati uendelee. Baada ya mazungumzo ya faragha kati ya Rais Hosni Mubarak na Mfalme wa Saudi Arabia Abdullah Bin Abdul-Aziz, msemaji wa Rais wa Misri Bw. Sulaiman Awad tarehe 10 alisema, Misri na Saudi Arabia zina matumaini makubwa ya kuona mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati unafanyika na kuvunja hali ya kukwama kwa miaka mingi, ili kuleta utulivu na amani katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Pili, Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zote zina matumaini ya kuwa nchi za Kiarabu ziwe na msimamo wa namna moja kuhusu suala la amani ya Mashariki ya Kati, ili kuiwezesha Palestina iwe nchi kamili na kuufanya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati upate maendeleo ya pande mbalimbali. Katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Amr Moussa alisema, pendekezo la amani la nchi za Kiarabu ni lazima liwe msingi wa mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, kwani lengo la nchi za Kiarabu kushiriki kwenye mkutano huo ni kwa ajili ya amani ya Mashariki ya Kati kwa pande zote, wala sio tu amani kati ya Palestina na Israel na kupuuza mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Bw. Moussa alisema mkutano wa waziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu utakaofanyika, utajadili mambo yote muhimu yatakayokuwa kwenye ajenda ya mkutano huo na kusawazisha msimamo yao, kwa sababu kushiriki kwenye mkutano huo sio uamuzi wa nchi moja fulani bali ni uamuzi wa pamoja. Syria mpaka sasa bado haijatangaza kama itashiriki kwenye mkutano huo au la. Waziri wa habari wa Syria Bw. Mohsen Bilal tarehe 10 alisema, mikutano yoyote ya kimataifa haitafanikiwa kama suala la ardhi ya milima ya Golan halitawekwa kwenye meza ya mazungumzo, au kama Syria haitaalikwa kushiriki kwenye mikutano hiyo. Kwa hiyo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice tarehe 12 kwenye mazungumzo na waandishi wa habari yaliyotangazwa kwenye televisheni alisema, Marekani itaialika Syria kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati. Waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Ahmed Abul Gheit tarehe 12 pia alisema, kama mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati ukiweza kufikia makubaliano ya kuijenga Palestina iwe nchi kamili, pande zote zitajitahidi kufanikisha lengo hilo. Msemaji wa Rais wa Misri Bw. Sulaiman Awad tarehe 10 alisisitiza kuwa, Rais Hosni Mubarak ana matumaini kuwa mkutano huo unaweza kukidhi matakwa ya watu wa Palestina na Israel , na matumaini yao ya amani yenye haki na ya kudumu.

Tatu, nchi za kiarabu zina matumaini kwamba jumuiya ya kimataifa itaishinikiza Israel ichukue hatua katika kutimiza mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Nchi za Kiarabu zinasema nchi ambayo haina nia ya kweli ya kutimiza amani ya Mashariki ya Kati, ni Israel.