Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-14 16:25:40    
Mapishi ya slesi ya ngisi

cri

Mahitaji:

Ngisi gramu 250, nyama ya nguruwe gramu 100, machipukizi ya mianzi gramu 80, chumvi gramu 5, mchuzi wa sosi gramu 2, mvinyo wa kupikia gramu 6, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, mafuta ya ufuta gramu 2.

Njia:

1. mkate ngisi awe slesi, halafu washa kwa maji na uikaushe.

2. kata nyama ya nguruwe na mianzi ya vichipukizi iwe vipande vipande, halafu chemsha maji, tia vipande vya machipukizi ya mianzi kwenye maji, korogakoroga vipakue.

3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia slesi ya ngisi, korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia korogakoroga, tia vipande vya nyama ya nguruwe na machipukizi ya mianzi korogakoroga, tia chumvi, mchuzi wa sosi, korogakoroga, tia chembechembe za kukoleza ladha, mimina mafuta ya ufuta korogakoroga. Ipakue mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.