Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-14 16:42:29    
Rekodi ya dunia ya kampuni ya Viwanda vizito ya Sany

cri

Kama tunavyojua, gari lenye mashine ya kusukuma zege ni kifaa cha kisasa cha kinachotumika katika ujenzi ambacho kinaweza kupeleka zege kila mahali kwenye sehemu ya ujenzi kwa kutumia mkono wake. Mkono huo ukikuwa mrefu zaidi, eneo linaloweza kufikika litakuwa kubwa zaidi. Ujenzi wa majenga makubwa na ya juu ya kisasa hakiwezi kuendelea bila kifaa hicho. Hivi karibuni, kampuni ya viwanda vizito ya Sany ambayo ni kampuni maarufa ya kutengeneza vifaa vya ujenzi ya China imeweka rekodi moja ya dunia ya urefu wa mkono wa gari la kusukuma zege.

Tarehe 20 Septemba, katika kiwanda kikubwa cha kampuni ya Sany mjini Changsha mkoani Hunan, watu wengi walikuwa wanatazama gari moja la kusukuma zege lenye mkono wa mita 66, ambalo ni gari la aina hiyo lenye mkono mrefu kabisa kote duniani. Mhandisi mwandamizi wa kampuni hiyo Bi. Zhu Hong alisema, si kazi rahisi kuongeza urefu wa mkono wa gari la kusukuma zege, mkono wake ukirefushwa, shinikio la gari zima pia linaongezeka, uwiano na uwezo wa gari wa kukabiliana na hali ya kuyumbayumba pia utaathiriwa. Nidyo maana kuna msemo unaojulikana katika sekta ya kutengeneza gari la aina hiyo kuwa 'kurefusha mkono kwa mita moja ni ni sawa na kujaribu kunyoosha mkono kwenda mbinguni'. Kwa hivyo kabla ya mwaka 1998, asilimia 80 hadi 90 ya magari ya aina hiyo yalikuwa yameagizwa kutoka nchi za nje, hata magari ya aina hiyo yaliyoundwa nchini China yalikuwa yanatumia mikono ya nchi za nje. Bi. Zhu Hong alisema:

"zamani China haikuwa na kampuni zenye teknolojia ya kutengeneza mkono mrefu, lakini sasa tunaitengeneza, ndiyo kama hivyo tutaweza kuvumba chapa yetu ya kiwango cha juu."

Zamani mkono mrefu kabisa wa gari la aina hiyo lililoagizwa kutoka nchi za nje ulikuwa na mita 36. baada ya kufanya utafiti kwa makini, kampuni ya viwanda vizito ya Sany iliamua kusanifu na kutengeneza gari la kusukuma zege lenye hakimiliki. Hivi sasa mkono mrefu kabisa wa gari la aina hiyo duniani una mita 56, na kutolewa kwa gari lenye mkono wa mita 66 kumeongeza rekodi hiyo kwa mita 10.

Mkurungezi mtendaji wa bodi ya kampuni ya Sany Bw. Yi Xiaogang alisema, gari hilo lenye mkono mrefu kabisa duniani lina teknolojia 15 muhimu za kisasa, zikiwemo teknolojia ya kupunguza hali ya kuyumba kwa mkono ambayo imerefusha kwa kiasi kikubwa muda wa matumizi ya mkono huo; teknolojia ya kisasa ya mfumo wa kujilinda imeinua kiwango cha utulivu na usalama kwa gari hilo likiwa kazini; teknolojia ya kupunguza matumizi ya nishati inapunguza kwa ufanisi utoaji wa hewa chafu na kuhifadhi mazingira, aidha, teknolojia ya kisasa ya mfumo wa udhibiti wa mkono inaweza kudhibiti vitendo vya mkono kutoka mbali (remote controller), aidha, kutokana na gari hilo linatumia chombo kikubwa cha kusukuma zege, imeongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kupeleka zege.

Katika sekta ya utengeneza wa mashine za ujenzi, mkono huo mwenye urefu wa mita 66 umetambuliwa kuwa mrefu kabisa duniani. Hivi karibuni, kampuni ya viwanda vizoto ya Sany imepokea hati ya utambulizi iliyotolewa na makao makuu ya rekodi za dunia ya Guinness.

Katibu mkuu wa shirikisho la mashine za ujenzi la China Bw. Shi Laide alipozungumzia gari hilo alisema:

"kutolewa kwa gari hilo lenye mkono wa mita 66 na kampuni ya Sany ni alama kuwa China imeanza kufanya uvumbuzi wa kujitegemea katika utengenezaji wa mashine za ujenzi."

Uvumbuzi wa bidhaa za teknolojia zenye hakimiliki umeiletea faida kubwa kwa kampuni ya Sany. Mwaka 2006, kampuni hiyo imetimiza pato la yuan bilioni 4.5, likiwa ni ongezeko zaidi ya asilimi 80 kuliko mwaka 2005 wakati kama huo. Katika miaka 13 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo, imedumisha ongezeko la zaidi ya ailimia 50 kila mwaka, shughuli zake katika ng'ambo zimefunika nchi mbalimbali kote duniani. Naibu mkurugenzi wa bodi ya kampuni hiyo Bw. He Zhenlin alisema:

"maendeleo hayo ya kasi yanatokana na kushikilia uvumbuzi na uwekezaji mkubwa katika utafiti wa teknolojia, uwekezaji mkubwa hakika utavutia wataalamu wengi kushiriki kwenye kampuni yetu, mkusanyiko wa wataalamu pia utahimiza zaidi uvumbuzi. Kuendelea kutolewa kwa matokeo ya uvumbuzi, kumeimarisha zaidi ulinzi wa hakimiliki, hatimaye kumeinua umaarufu wa chapa yetu. Mzunguko huo mzuri umepanua zaidi njia ya maendeleo ya kampuni yetu."

Imefahamika kuwa, gari hilo lenye mkono wa mita 66 litaoneshwa katika miji 9 nchini China ikiwemo Guangzhou, Nanjing, Shanghai, Hangzhou na Beijing, baadaye litakwenda nje na kuoneshwa katika nchi za Marekani, Ujerumani, Hispania na Saudi Arabia. Mhandisi mwandamizi wa kampuni ya Sany Bi. Zhu Hong alisema, gari hilo ni mwanzo mpya kwake na kwa kampuni hiyo. Hivi sasa Bi. Zhou Hong atashiriki kwenye miradi 2 au 3 mikubwa ya utafiti, kuendelea kufanya uvumbuzi kumekuwa imani ya pamoja yake na kampuni ya Sany.

Idhaa ya kiswahili 2007-11-14