Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-15 18:51:47    
Mfuko wa Song Qingling wa China

cri

Kati ya wananchi wa China zaidi ya bilioni 1.3, kuna watu wasio wazima zaidi ya milioni 300. Watoto nchini China siku zote wanafuatiliwa sana, serikali ya China ilitunga sheria ya kuwalinda watoto ili kulinda haki na maslahi yao, pia kuna idara maalumu zinazoshughulikia mambo ya watoto. Jumuiya mbalimbali za jamii zinasaidia serikali kuhimiza maendeleo ya watoto. Leo tutawaletea maelezo kuhusu mfuko wa Song Qingling wa China ambao umekuwa unafuatilia maendeleo ya watoto nchini China katika miaka 25 iliyopita.

Bibi. Song Qingling alikuwa mmoja kati ya viongozi wazee wa China waliofariki dunia, aliwahi kutoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa taifa na maisha mazuri ya wananchi wa China. Alifariki mwaka 1981 ambapo alikuwa rais wa heshima wa nchi.

Katika maisha yake, alifuatilia sana maendeleo ya watoto, alichukulia shughuli zinazohusu watoto kuwa ni shughuli zinazohusiana na siku za usoni za taifa. Katika miaka miwili baada ya yeye kufariki dunia, mfuko wa Song Qingling wa China ulianzishwa. Hadi sasa thamani ya jumla ya mfuko huo imefikia Renminbi milioni 100.

Katibu mkuu wa sasa wa mfuko huo Bw. Li Ning alisema katika miaka 25 iliyopita, mfuko huo ulifuata matumaini ya marehemu Song Qingling, kuweka lengo la mfuko huo kwa kuendeleza shughuli za watoto, kufuatilia ukuaji mzuri wa watoto na maendeleo ya pande zote ya watoto, na kufanya shughuli mbalimbali kuhusu maendeleo ya watoto na ukuaji mzuri wa watoto alisema:

"tulifanya shughuli kadhaa ili kuinua sifa ya watoto na mafunzo kuhusu maadili ya watoto, kama vile kutoa tuzo ya uvumbuzi wa watoto na tuzo ya fasihi ya watoto ya Song Qingling. Katika sehemu zenye matatizo ya kiuchumi, tulisaidia watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi warudi tena shuleni, kuboresha mazingira ya ufundishaji shuleni, kuweka mradi wa kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu, na kufanya shughuli zinazohusu matibabu na afya ya mama na watoto."

Watoto wengi walinufaika kutokana na shughuli hizo.

Chen Xi ni mwanafunzi wa shule ya msingi mjini Changsha mkoani Hunan. Muda mfupi uliopita, alipata tuzo ya shahada ya uvumbuzi ya watoto ya Song Qingling. Tuzo hii imempa moyo, yeye anapenda zaidi kutengeneza vitu. Hivi karibuni, yeye ana mpango wa kutengeneza mashine ya kuzalisha umeme kwa kutumia sauti ya kelele. Alisema :

"Nilitengeneza vitu mimi mwenyewe, vitu hivyo vinahusiana na ujuzi wa sayansi na teknolojia ya pande mbalimbali. Nikiongeza ujuzi wangu, uwezo wangu wa kutengeneza vitu pia utaongezeka."

Tuzo ya uvumbuzi wa watoto ya Song Qingling ni tuzo moja kati ya tuzo zilizowekwa na mfuko wa Song Qingling, na watoto zaidi ya laki moja wa sehemu mbalimbali nchini China wanashiriki kwenye shughuli hizo. Watoto zaidi ya elfu moja wamewahi kupata tuzo hiyo, na uvumbuzi wao unahusiana na pande mbalimbali za maisha. Naibu mkurugenzi wa kamati ya tuzo ya uvumbuzi ya watoto ya Song Qingling Bw. Lu Shan alisema:

"Lengo la shughuli hizo ni kuwaandaa watoto wawe na uwezo wa uvumbuzi na utekelezaji. Maendeleo ya taifa yanategemea sayansi na teknolojia, sayansi na teknolojia zinategemea watu wenye ujuzi, tunapaswa kuwaandaa watu wenye ujuzi kuanzia utotoni."

Idhaa ya kiswahili 2007-11-15