Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-15 20:14:31    
Nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zataka kuunda umoja wao wa usalama

cri

Mkutano wa pili wa mawaziri wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulianza tarehe 14 huko Singapore. Kwenye mkutano huo mawaziri wa ulinzi wa nchi kumi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki walisisitiza kuwa, nchi zote za umoja huo zitajitahidi kuimarisha ushirikiano wa amani na usalama wa sehemu hiyo, ili kutimiza lengo la ushirikiano kwenye Usalama la Umoja wa Asia ya kusini mashariki ifikapo mwaka 2015.

Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulianzishwa mwaka 1967. Baada ya kuendelezwa kwa miaka mingi, nguvu za umoja huo katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni, inaimarishwa kwa mfululizo, na unatoa mchango mkubwa katika shughuli za sehemu hiyo. Lakini maendeleo ya maeneo mbalimbali ya umoja huo bado yanakabiliwa changamoto ya usalama.

Kama inavyojulikana, mlango wa bahari wa Malacca, ambao ni kiungo cha bahari ya Pasifiki na bahari ya Hindi, uko kwenye sehemu ya Asia ya kusini mashariki, lakini katika miaka mingi iliyopita, shughuli za maharamia walioko kwenye sehemu hiyo, zimeathiri sana maendeleo ya uchukuzi wa baharini na maendeleo ya sehemu hiyo. Baada ya kutokea tukio la tukio la "Tarehe 11 Septemba", sehemu ya Asia ya kusini mashariki inakabiliwa na tishio jipya linalohatarisha usalama wake, ambalo ni pamoja na ugaidi, biashara ya magendo ya mihadarati na biashara ya watu. Licha ya hayo, nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki zinatambua kuwa kutokuwepo kwa mazungumzo kuhusu usalama wao hakunufaishi maendeleo ya maslahi ya nchi zote za Asia ya kusini mashariki.

Nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki ziliafikiana kuwa zitamaliza kazi ya kuunda "idara za nchi za Asia ya kusini mashariki" mnamo mwaka 2020. Idara hizo mpya ni pamoja na nguzo tatu za umoja wa uchumi, umoja wa usalama pamoja na umoja wa jamii na utamaduni. Mkutano wa kwanza wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa Asia ya kusini mashariki ulifanyika mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. Hayo ni maendeleo muhimu ya utaratibu wa mazungumzo kuhusu suala la usalama la Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Mawaziri wa ulinzi walioshiriki kwenye mkutano huo, walikubali kuanzishwa kwa umoja wa usalama kabla ya mwaka 2020 ili kuinua uwezo wa nchi za umoja wa Asia ya kusini mashariki katika kupambana na wahalifu wa kimataifa na magaidi, na kuimarisha usalama wa baharini na uwezo wa kutoa msaada kwa watu waliokumbwa na maafa. Mkutano wa wakuu wa nchi wa umoja wa Asia ya kusini mashariki uliofanyika mjini Cebu mwezi januari mwaka 2007, uliamua kutimiza lengo la kuunda jumuiya ya nchi za Asia ya kusini mashariki katika mwaka 2015.

Kwenye mkutano wa pili wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa Asia ya kusini mashariki, mawaziri wa ulinzi walitoa maelezo kuhusu suala la usalama wa nchi zao na kufanya majadiliano kuhusu masuala ya usalama ya duniani na ya sehemu hiyo pamoja na mustakabali wa maendeleo ya sehemu hiyo. Hatimaye walisaini "Azimio la mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa Asia ya kusini mashariki" pamoja na nyaraka tatu, ili kuimarisha maelewano, kuaminiana na ushirikiano kati yao.

Hususan "Azimio la Pamoja" lilifanya uchambuzi kuhusu maendeleo ya ushirikiano ya sehemu hiyo, ambao umeweka wigo kwa ushirikiano wa ulinzi na usalama wa umoja huo katika siku za baadaye. Nyaraka hizo tatu ni "mapatano kuhusu wazo la mkutano wa mawaziri wa ulinzi", "mpango wa kazi wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi katika miaka mitatu ijayo" na "makubaliano kuhusu wazo la mkutano wa upanuzi wa mawaziri wa ulinzi". Waraka ule wa "makubaliano kuhusu wazo la mkutano wa mawaziri wa ulinzi" umeweka kanuni za utaratibu kuhusu mazungumzo, mashauriano na uamuzi wa sera za ulinzi. "Mpango wa utekelezaji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi katika miaka mitatu ijayo" umetoa malengo ya miradi ya ushirikiano katika mambo ya ulinzi. Na waraka wa "makubaliano kuhusu wazo la mkutano wa upanuzi wa mawaziri wa ulinzi" umeeleza kanuni na njia za mawasiliano kati ya umoja wa Asia ya kusini mashariki na nchi nyingine za sehemu ya kusini mashariki.