Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohamed El Baradei tarehe 15 aliwasilisha ripoti mpya kuhusu suala la nyuklia la Iran kwa nchi 35 wajumbe wa baraza la shirika hilo, kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini Vienna. Ripoti hiyo inasema Iran imefanya ushirikiano wa kutosha na shirika hilo katika kufafanua mpango wake wa nyuklia na imefanya juhudi kutokana na matakwa ya shirika hilo, lakini haikufanya juhudi ipasavyo kwenye ushirikiano huo.
Kwenye ripoti hiyo Bw. Baradei alisema Iran ililiruhusu Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki lifanye ukaguzi kuhusu zana zake za nyuklia, na aliisifu Iran kwa kujibu maswali ya shirika hilo kwa wakati na kushirikiana na shirika hilo kwenye suala la mashine za kusafisha uranium. Lakini Bw. Baradei amesema hajaridhika na vitendo vya Iran kuhusu masuala ambayo bado hajatatuliwa ya mpango wa nyuklia. Ripoti hiyo inasema Iran inaendelea kupuuza maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kutosimamisha shughuli za kusafisha Uranium. Iran imefanya juhudi kuimarisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na kuongeza uwazi wa mpango wake wa nyuklia kutokana na makubaliano husika kati yake na shirika hilo. Hivyo Iran inatoa ushirikiano kutokana na matakwa ya shirika hilo badala ya kufanya juhudi ipasavyo.
Iran na nchi za Magharibi zikiwemo Marekani na Uingereza ziliitikia ripoti hiyo kwa njia tofauti. Tarehe 15 mwakilishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo ya nyuklia ambaye pia ni katibu wa kamati kuu ya usalama wa taifa ya Iran Bw. Saeed jalili aliifurahia ripoti hiyo, na alisema ripoti hiyo inathibitisha kuwa maneno yote kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ni kwa ajili ya malengo la kijeshi ni uwongo.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Bw. Jalili alisema, ripoti hiyo inaonesha kuwa maneno yote yanayosemwa kuwa mpango wa nyuklia wa Iran ni kwa ajili ya lengo la kijeshi ni uwongo, ripoti hiyo imethibitisha lengo letu la amani. Iran Imejibu maswali yote ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili umepata maendeleo. Aliilaani jumuiya ya kimataifa kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, alisema ripoti hiyo imevunja msingi wa kuwasilisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Siku hiyo serikali ya Marekani ilisema Iran inaendelea kupuuza jumuiya ya kimataifa, na kutotoa majibu kamili kuhusu masuala yasiyotatuliwa ya mpango wa nyuklia wa Iran. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi. Dana Pereno alisema kutokana na Iran kukataa kusimamisha shughuli za kusafisha Uranium, Marekani itaendelea kushirikiana na Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, China na Russia, ili kutekeleza mpango wa tatu wa kuiwekea vikwazo Iran. Serikali ya Uingereza imesema wakati Iran inapohimizwa kufafanua mambo yote, inaona ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki inaonesha kuwa, Iran haijajibu maswali kadhaa muhimu. Serikali ya Uingereza ilisema, kabla ya kupata matokeo mazuri kwa ripoti nyingine kuhusu suala la nyuklia la Iran itakayotolewa mwezi huu na mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za usalama Bw. Javier Solana, Uingereza italiomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya waiwekee Iran vikwazo vipya.
|