Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-16 19:20:27    
Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ni mfano wa ushirikiano kati ya kusini na kusini

cri

Wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ufanyike mwaka jana hapa Beijing, balozi wa Cameroon nchini China ambaye pia ni kiongozi wa kundi la mabalozi wa nchi za Afrika nchini China, Bw. Etien alizipongeza China na Afrika, akisema Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya kusini na kusini duniani.

Bw. Etien alifafanua kutoka upande wa siasa, akisema mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana Beijing ulitoa mwelekeo wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika siku za baadaye. Miezi miwili baada ya kumalizika kwa mkutano huo, rais Hu Jintao wa China alifanya ziara katika nchi nane barani Afrika, hii ilipanua zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika. Wakati huo huo viongozi wa nchi nyingi za Afrika pia walifanya ziara nchini China, na kufanya juhudi kwa kutekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo. Bw. Etien alisema mkutano huo pia ulionesha msimamo wa China, kuhusu kuhimiza amani na maendeleo ya Afrika, hasa kwenye suala la Darfur, sio tu China ilikuwa inaendelea kutoa misaada mingi kwa sehemu ya Darfur, bali pia ilimteua mjumbe maalumu wa serikali anayeshughulikia suala la Darfur, na kufanya juhudi za kuhimiza kampeni ya kulinda amani kwenye sehemu hiyo na mchakato wa amani ya sehemu hiyo.

Kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana hapa Beijing, serikali ya China ilitangaza kufuta na pia kupunguza madeni ya nchi za Afrika. Bw. Etien alisema hatua hiyo ilipunguza mzigo wa maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika. Na kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya China na Afrika kulihamasisha viwanda vya China viwekeze barani Afrika, na kuonesha umuhimu wa kuhakikisha maendeleo ya uchumi barani Afrika. Kwenye upande wa teknolojia, China ilizisaidia nchi nyingi za Afrika kuwaandaa watu wengi wenye ujuzi wa kilimo, na kutoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya kilimo na kuhakikisha kujitosheleza kwa chakula barani Afrika.

Bw. Etien hasa alieleza umuhimu mkubwa wa mfuko wa maendeleo ya China na Afrika na mradi wa ujenzi wa kituo cha mikutano cha Umoja wa Afrika. Alisema mfuko wa maendeleo ya China na Afrika unaonesha umuhimu mkubwa, serikali ya China inahimiza viwanda vya China vyenye nguvu halisi na sifa nzuri viwekeze barani Afrika, na kuanzisha miradi inayosaidia kuinua kiwango cha teknolojia cha nchi za Afrika, kuongeza nafasi za ajira na kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii za huko. Bw. Etien alisema China ilisaidia kujenga kituo cha mikutano cha Umoja wa Afrika, hii imeonesha kuwa serikali ya China inaunga mkono nchi za Afrika kushirikiana, kujitegemea, na kuharakisha ujenzi wa utandawazi wa uchumi barani Afrika. Alisema kituo hicho kitakuwa ni alama ya urafiki kati ya China na Afrika.

Alipozungumzia namna ya kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika, Bw. Etien alisema hivi sasa China na Afrika zimepata mafanikio makubwa kwenye mawasiliano ya utamaduni kati yao. Wanafunzi wengi kutoka barani Afrika wamepewa udhamini wa masomo nchini China, wanafunzi hao wamejenga daraja la mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika. Bw. Etien alisema hivi sasa vyombo vya habari vya bara la Afrika vinataka sana kuifahamu China na wananchi wake, hivyo China na Afrika zinapaswa kuhimiza na kupanua mawasiliano kati ya vyombo vya habari, ili kuhimiza maelewano kati ya pande hizo mbili.

Bw. Etien alisema hatua nane zilizotolewa na China kwa ajili ya kuhimiza uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwaka jana, zitahimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye eneo kubwa zaidi na kwenye ngazi ya juu zaidi, na zitafungua ukurasa mpya wa uhusiano huo.

************************************************

katika mwaka mmoja uliopita, China na Afrika zilifanya juhudi kutekeleza hatua zilizotolewa kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana hapa Beijing, kuhimiza uhusiano wa aina mpya kati yao ulio wa kiwenzi na kimkakati, na kufungua ukurasa mpya wa urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika.

Wakuu wa China na nchi za Afrika walitembeleana mara kwa mara, mazungumzo ya kisiasa ya aina mbalimbali yaliongezeka, na maelewano na uaminifu kati ya China na Afrika uliimarishwa. Rais Hu Jintao wa China, spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo, na mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Jia Qinglin walifanya ziara kwenye nchi 13 za Afrika, na wakuu watano wa nchi za Afrika walifanya ziara rasmi nchini China. China na nchi zaidi ya kumi za Afrika zilifanya mikutano ya kamati ya pande mbili mbili na mazungumzo ya kisiasa kati ya wizara za mambo ya nje. Mawasiliano kati ya mabunge, vyama vya siasa, na ujumbe wa sehemu mbalimbali za pande hizo mbili yameongezeka siku hadi siku. China iliimarisha ushirikiano na mawasiliano na Umoja wa Afrika na mashirika ya kikanda barani Afrika, na kuunga mkono Umoja wa Afrika kuonesha umuhimu wa uongozi katika utatuzi wa masuala ya Afrika. Hadi kufika sasa China imeshiriki kwenye operesheni saba za kulinda amani za Umoja wa Mataifa barani Afrika, na idadi ya askari wa kulinda amani wa China imefikia elfu 1.3, na kutoa mchango mkubwa katika kuunga mkono Afrika kulinda amani na utulivu.

Serikali ya China ilitimiza ahadi zake kuhusu kuongeza misaada kwa Afrika, kusamehe madeni na kufuta ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa, pia ilianzisha mfuko wa maendeleo ya China na Afrika, na kuhimiza ujenzi wa sehemu za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara barani Afrika. Thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliendelea kuongezeka, ushirikiano kati ya viwanda vya China na Afrika uliimarishwa siku hadi siku. Wanakampuni zaidi ya 500 wa China walishiriki kwenye mkutano mkubwa wa ushirikiano kati ya viwanda vya China na Afrika uliofanyika nchini Misri mwezi Mei mwaka huu. Ushirikiano wa kifedha kati ya China na Afrika pia uliimarishwa siku hadi siku, mkutano wa mwaka wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya maendeleo ya Afrika ulifanyika kwa mafanikio mjini Shanghai. China ilirusha satellite ya kwanza ya mawasiliano ya Nigeria. Safari nne za ndege za moja kwa moja kati ya China na Afrika zilianzishwa, na kurahisisha mawasiliano ya watu. Ushirikiano kati ya China kwenye ujenzi wa miundo mbinu na raslimali ya nishati pia unaendelea vizuri.