Waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong alasiri ya tarehe 18 mwezi Novemba alikuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa China Bw. Wen jiabao, ambaye hivi sasa yuko ziarani nchini Singapore. Pande hizo mbili zilifikia makubaliano kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kusaini makubaliano kati ya serikali za nchi hizo mbili kuhusu kuujenga mji wa Tianjin wa China uwe mji wenye mapatano na mazingira ya viumbe. Katika mazungumzo yao, kuhimiza mazungumzo ya kuanzisha eneo la soko huria, kujenga mfumo wa mazungumzo kuhusu sera za ulinzi na kuendeleza soko katika upande wa tatu yalikuwa masuala yaliyotiliwa mkazo zaidi. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mazungumzo hayo, Bw. Lee Hsien Loong alieleza maoni yake kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili, akisema:
"Uhusiano kati ya nchi hizi mbili ni wenye mapana, marefu na nguvu, hii ni kwa sababu uhusiano wetu umejengwa kwenye msingi wa kuwa na maoni ya kimkakati ya namna moja kuhusu maendeleo ya ukanda na Asia na kuinuka kiamani kwa China. Tumekuwa na ushirikiano mkubwa juu ya msingi wa usawa, kuheshimiana na kunufaishana."
Suala la Taiwan pia lilikuwa moja ya masuala muhimu yaliyozungumziwa. Kwa niaba ya serikali ya Singapore Bw. Lee Hsien Loong alisisitiza msimamo kuhusu kupinga Taiwan kujitenga na China, Bw. Wen Jiabao alipongeza msimamo huo, akisema:
"Tulifanya majadiliano pia kuhusu uhusiano wa kando mbili za mlango bahari wa Taiwan. Mimi nilieleza msimamo wa serikali ya Singapore kuhusu suala hilo. Msimamo huo haubadiliki, yaani kuendelea kufuata sera ya kuweko kwa China moja duniani na kupinga Taiwan kujitenga na China."
"tunamshukuru sana waziri mkuu Lee Hsien Loong kwa kueleza wazi tena kuendelea kufuata sera za kuweko kwa China moja, na kuiunga mkono China kutimiza muungano wa taifa."
Mbali na uhusiano wa pande mbili, mawaziri wakuu wa nchi mbili walibadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda yanayoyafuatiliwa na nchi zao, likiwemo suala nyeti la Myanmar. Waziri mkuu Wen Jiabao naye pia aliwaeleza waandishi wa habari kuhusu msimamo wa China kuhusu suala la Myanmar, akisema.
"Mazungumzo yetu yanahusu masuala ya kikanda na kimataifa yanayofuatiliwa na pande zetu mbili, hususan suala la Myanmar, tunaona kwa pamoja kuwa maafikiano ya kitaifa yangerejeshwa mapema iwezekanavyo, kutimiza amani, utulivu na kuleta maendeleo ya Myanmar kutokana na usuluhisho wa Umoja wa Mataifa, hasa jitihada za wananchi wa Myanmar."
Baada ya mazungumzo yao, mawaziri wakuu wa nchi mbili walisaini makubaliano ya kanuni za kujenga kwa ushirikiano mji wa Tianjin uwe mji wa mapatano na mazingira ya viumbe. Mawaziri wakuu hao wawili wana matarajio makubwa kuhusu mradi huo mpya wa ushirikiano. Bw. Lee Hsien Loong alisema, sekta mbalimbali za Singapore zinaunga mkono kwa juhudi mradi huo mpya.
"Pande na sekta mbalimbali nchini Singapore zinauunga mkono kwa nguvu mradi huo, ninaamini kuwa serikali kuu ya China na serikali ya mji wa Tianjin pia zitauunga mkono kwa nguvu mradi huo, na kuuendeleza mradi huo kuwa alama nyingine ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Singapore."
Bw. Wen Jiabao aliona uvumbuzi wa ushirikiano wa nchi hizo mbili kutokana na ujenzi wa mji wa kuhifadhi mazingira ya viumbe, tena anatarajia kuwa mradi wa mji wa Ecology kuwa alama mpya ya urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili."
Aidha mawaziri wakuu hao walizindua ubao wa shaba wenye maandishi wa jengo la mfuko wa fedha wa elimu wa Singapore na China. Habari zinasema mfuko huo wa fedha utatoa msaada wa mafunzo ya kuandaa watumishi wa serikali wa nchi hizo mbili.
|