Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-20 10:39:47    
Maendeleo yenye masikilizano ya mji wa Xuzhou

cri

   

Mji wa Xuzhou uko kaskazini magharibi mwa mkoa wa Jiangsu, ambao ni sehemu ya eneo la uchumi la mto Huai-Hai linaloundwa na mikoa ya Jiangsu, Shandong, Henan na Anhui. Reli kutoka Beijing hadi Shanghai na Reli inayotoka mkoa wa Gansu hadi mkoa wa Jiangsu zinakutana mjini humo. Mji wa Xuzhou pia unazalisha maliasili na nishati nyingi, na ni kituo pekee cha uzalishaji wa makaa ya mawe mkoani Jiangsu. Nishati ya kutosha imeharakisha mchakato wa maendeleo ya viwanda mjini humo, lakini pia imeathiri mazingira ya kimaumbile ya mji huo. Kuhusu suala la kushughulikia uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya uchumi, katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China wa mji wa Xuzhou Bw. Xu Ming alimwambia mwandishi wa habari kuwa,

"Bila Shaka tutahifadhi mazingira."

Bw. Xu Ming alisema hayo, na anawaongoza wakazi wa mji huo kufanya hivyo. Serikali ya mji huo imechukua hatua nyingi ili kuboresha mazingira ya mji huo. Alisema,

"Mji wa Xuzhou ni mji unaozalisha makaa ya mawe, pia ni kituo muhimu cha mawasiliano. Zamani watu walisema ukiingia mjini Xuzhou utavuta hewa yenye vumbi yenye gram 100. Katika miaka miwili iliyopita, tulifunga matanuri yote yanayotumia makaa ya mawe, tulianza kutumia nishati zisizosababisha uchafuzi kwa wingi zikiwemo gesi ya asilia na gesi ya makaa ya mawe badala ya makaa ya mawe. Licha ya kufunga matanuri yanayotumia makaa ya mawe, pia tulivihamisha viwanda vya kemikali ili kuboresha mazingira ya mji wetu."

Habari zinasema kwa jumla mji wa Xuzhou ulifunga viwanda vidogo 47 vya saruji, viwanda vidogo 117 vya karatasi, kupiga marufuku matumizi ya migodi midogo ya makaa ya mawe, kubomoa matanuri 646 na dohari 740 zilizokuwa katikati ya mji huo. Baada ya kuchukua hatua kadha wa kadha, sifa ya hewa mjini humo inaboreshwa mwaka hadi mwaka. Katika asilimia 83.4 ya siku za mwaka huu hali ya hewa mjini humo imefikia kigezo cha pili cha hali nzuri ya hewa. Idara kuu ya uhifadhi wa mazingira ya China imesema mji wa Xuzhou ni mmoja kati ya miji ambayo siku zenye hali nzuri ya hewa zinaongezeka haraka zaidi nchini China. hivi sasa mji huo umetimiza hali nzuri ya mazingira.

Mradi wa kusafirisha maji kutoka sehemu ya kusini hadi sehemu ya kaskazini ya China ni mmoja kati ya miradi mikubwa zaidi nchini China ambayo ni pamoja na miradi ya Magenge matatu ya Mto Changjiang na reli ya Qinghai-Tibet. Mji wa Xuzhou ni kituo muhimu kwenye mradi huo, hivyo China inatilia maanani mazingira ya miji inayohusika na ujenzi wa mradi huo, hasa mji wa Xuzhou. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo umeongeza nguvu kutekeleza mradi wa kuleta maji safi, kuhimiza utekelezaji wa vigezo vya utoaji wa maji taka, kujenga bomba la maji taka lenye urefu wa kilomita 51.4, viwanda vikubwa 9 vya kushughulikia maji taka, na mfumo wa kusimamia sifa ya maji ya kunywa, ili wakazi wa mji huo waweze kupata maji safi ya kutegemewa.

Bw. Xu Ming anaona kuwa, mazingira mazuri ya mji yanatokana na maji safi na kuwa na miti mingi. Katika miaka miwili iliyopita, licha ya kufanya kazi kubwa ili kuboresha sifa ya maji, mji wa Xuzhou pia umeongeza nguvu kubwa ya kupanda miti mjini humo. Hivi sasa wastani wa eneo la miti kwa mtu ni karibu mita 8 za mraba, na asilimia 23 ya eneo limefunikwa na miti mjini humo, ambalo linachukua nafasi ya kwanza mkoani Jiangsu.

   

Kuboreshwa kwa mazingira kumeongeza nguvu ya jumla ya mji wa Xuzhou. Tangu mwaka 2004, mji huo umewahi kuwekwa mara mbili kwenye orodha ya miji mizuri zaidi ya biashara ya China bara na gazeti la Forbes, pia ulisifiwa kwa miaka miwili mfululizo na shirikisho la mashine za umeme na elektroniki la Taiwan kuwa mji mzuri zaidi kwa uwekezaji. Mwaka 2005 mji huo ulipata sifa ya mji wenye chapa nyingi maarufu za bidhaa, na uliwekwa kwenye orodha ya miji 100 yenye nguvu kubwa zaidi nchini China. Mwaka 2006 mji wa Xuzhou uliwekwa kwenye orodha ya miji 200 yenye sifa za kipekee inayowavutia watu nchini China, pia uliwekwa kwenye orodha ya miji yenye maendeleo makbuwa ya kiuchumi na wenye mazingira mazuri ya viumbe yanayowavutia watu zaidi nchini China. Sifa hizo zimeufanya mji wa Xuzhou kwa mji mzuri wa uwekezaji kwa wafanyabiashara wa nchi za nje.

Bw. Xu Ming anapozungumzia kazi ya kuvutia wafanyabiashara na uwekezaji, alisema mji huo unawakaribisha wafanyabiashara wa nchini na nchi za nje kufanya uwekezaji mjini humo, lakini pia alitoa matakwa kuhusu makampuni na miradi, alisema,

"Kwanza tunayakaribisha zaidi makampuni yanayofikia kiwango fulani cha teknolojia kadhaa ambayo hayatoi uchafuzi mwingi. Pili tunayakaribisha makampuni yanayoweza kuongeza nafasi za ajira. Tatu tunayakaribisha makampuni ya teknolojia za kisasa, ambayo tunatekeleza sera ya upendeleo kwa makampuni hayo. Tumerahisishia njia ya uwekezaji kwa kujenga kituo cha utawala kwa wawekezaji wa nchini na kutoka nchi za nje, wawekezaji wanaotaka kuwekeza mjini Xuzhou wanaweza kushughulikia mambo yote kwenye kituo hicho."

Mazingira mazuri ya uchumi na uwekezaji yanausaidia mji wa Xuzhou kuvuta mitaji mingi kutoka nje. Hadi hivi sasa makampuni 13 kati ya makampuni 500 yenye nguvu kubwa zaidi duniani yamewekeza kwenye miradi 13 mjini humo, na thamani ya uwekezaji ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 600. Mitaji mingi kutoka nchi za nje na utaratibu wa kisasa wa usimamizi wa uzalishaji umeongeza nguvu ya kichumi ya mji huo.

Historia ndefu, utamaduni unaong'ara, mazingira mazuri ya kimaumbile, mji wenye hali ya masikilizano, na maendeleo makubwa ya uchumi yameufanya mji wa Xuzhou uwe mji wenye uchangamfu ambao unavutia.