Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-21 15:51:02    
Familia ya kabila la Watibet kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet

cri

Bw. Kharsicer mwenye umri wa miaka 57 ni mfugaji mmoja wa kawaida anayeishi kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet. Nyumba yake iko kwenye mbuga ya heri kando ya ziwa Qinghai, na ina vyumba tisa. Kutokana na kuwa kwenye uwanda wa juu, vyumba hivyo vilifungwa vizuri kwa vioo ili kuzuia baridi. Kwenye sebule kubwa ya nyumba hiyo, kuna vifaa vizuri vya umeme na samani za kisasa, na vyakula vitamu viliandaliwa mezani. Hali hiyo iliwafanya waandishi wetu wa habari waone kama wako mjini. Alipozungumzia mabadiliko makubwa yaliyotokea katika familia yake, alisema,

"Tulianza kuweka makazi yetu hapa mwaka 1989. Zamali tulikuwa tunakaa kambini na kuhama hama ili kutafuta malisho kwa mifugo, hivyo awali hatukuweza kuzoea maisha ya kutoahama hama, lakini sasa tunafurahia sana maisha haya yenye manufaa zaidi. Baada ya kuwa na makazi ya kudumu, maisha yameboreshwa kwa kasi , na hata chakula chetu kimebadilika, zamani tulikuwa tunakula nyama tu, tambi za kukaangwa na tsampa ambacho ni chakula maalumu cha kabila la Watibet, lakini sasa aina za chakula chetu zimeongezeka sana."

Kutokana na hali mbaya ya hewa kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, ni vigumu kwa watu wanaoishi kwenye uwanda huo hasa wanavijiji kupata chakula cha mboga mbichi. Kwa mujibu wa desturi ya chakula cha kabila la Watibet, wenyeji wanapaswa kuandaa vipande vikubwa vya nyama ya ng'ombe na mbuzi, lakini siku hiyo waandishi wetu wa habari waliandaliwa mboga mbichi. Kwa kuwa nyumba ya Bw. Kharsicer iko mbali na mji, mboga hizo mbichi zilipatikana wapi? Bw. Kharsicer aliwaambia kuwa katika majira ya joto, mifugo yake inahamishiwa kwenye shamba la nyasi, na zizi la kioo la kulaza mifugo linabaki wazi, ili kuondoa tatizo la kupata mboga mbichi, alipanda mboga za aina mbalimbali kwenye zizi hilo.

Mboga zinazooteshwa kwenye zizi la vioo haziwezi kukidhi tu mahitaji ya familia ya Bw. Kharsicer, bali pia zinatolewa kwa majirani zake. Bw. Kharscier alisema kutokana na mabadiliko ya desturi ya kula chakula na vitendo vingine katika maisha, magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa tumbo na viungo yaliyokuwa yanawakumba wafugaji kwa urahisi sasa yamepungua sana. Mke wa mtoto wake Bibi Lhamotso mwenye umri wa miaka 30 alisema,

"Katika miaka ya hivi karibuni, maisha ya wafugaji yamebadilika sana. Ingawa sasa tunaishi milimani na tuko mbali na miji, lakini kutokana na misaada ya serikali na jitihada zetu wenyewe, familia zote za wafugaji zina makazi ya kudumu. Mwaka jana serikali ilitusaidia kupata umeme na kutuwekea maji ya bomba."

Kama alivyosema Bibi Lhamotso, katika miongo kadhaa iliyopita, kutokana na hali mbaya ya hewa na wafugaji kuhamahama, hakukuwa na umeme wala maji ya bomba kwenye makazi yao, na maisha ya wafugaji hao yalikuwa magumu sana hata wengine hawakuweza kupata chakula na nguo za kutosha. Hivi sasa wafugaji hao wamebadilisha desturi yao ya maisha, na wamekuwa na makazi ya kudumu, na maisha yao yameboreshwa sana kutokana na misaada ya serikali.

Bw. Kharsicer aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, sasa ana mbuzi zaidi ya 1,200 na ng'ombe zaidi ya 170, mwaka jana mapato yake yaliyotokana namauzo ya mbuzi na ng'ombe yalifikia zaidi ya yuan elfu 60, na alimnunulia mwanaye nyumba mjini kwa kwa kutumia zaidi ya yuan elfu 80. Ili kujionea wafugaji wanavyoishi kwenye mji, kwa kuandamana na Bw. Kharsicer waandishi wetu wa habari walitembelea nyumba ya mwanaye iliyoko mjini.

Nyumba iliyonunuliwa na Bw. Kharsicer mjini ina eneo la zaidi ya mita 80 za mraba, vyombo vya umeme, samani na vitu vingine vilivyowekwa kwenye nyumbani hiyo ni kama vile vya nyumba za kawaida za mijini, inaweza kutambuliwa kuwa ni nyumba ya watu wa kabila la Watibet kwa kupita tangkas iliyo juu ya ukutani ambayo ni picha maalumu ya kabila la Watibet na sanamu za dini ya kibudha. Mke wa Bw. Kharsicer bibi Harmo alisema,

"Zamani wanawake katika familia ya wafugaji wa kabila la Watibet walikuwa wanachoka zaidi, hawakuwa na makazi ya kudumu, walikuwa wanahudumia mifugo mingi na kupika chakula, kuleza watoto na kutunza waume, hivyo walipatwa na magonjwa ya aina mbalimbail. Lakini sasa hali imebadilika, nina kaa nyumba nzuri, na kuweza kutumia vyombo vya kisasa vya umeme. Zamani sikuthubutu kutarajia maisha hayo mazuri hata nilipoota ndoto."

Maisha mazuri huleta furaha kubwa moyoni. Bibi Harmo aliimba wimbo ya kabila la Watibet.

Baada ya kupata maisha mazuri, wafugaji wameanza kujiendeleza katika utamaduni. Mtoto mkubwa na mume wa binti wa Bw. Kharscier walijiunga na kikundi cha wapanda farasi cha mji, na mara kwa mara wanakwenda kuonesha ustadi wao wa kupanda farasi kwa wageni. Binti na mke wa mtoto wa Bw. Kharscier wamejifunza kupiga ala ya muziki, wakiwa na nafasi, wanakusanyika kupiga muziki, na hata mjukuu wake mwenye umri wa miaka mitano anapenda kushirika kwenye mchezo wao.

Idhaa ya kiswahili 2007-11-21