Uturuki na Iran tarehe 20 zilisaini mkataba wa ushirikiano wa kuzalisha umeme huko Ankara. Huu ni mkataba wa pili wa ushirikiano wa kinishati tokea mwezi Julai. Wachambuzi wanaona kuwa wakati Marekani inapotaka kuiwekea Iran vikwazo vipya, Uturuki na Iran bado zinaendelea na ushirikiano wa kinishati, hakika hii ni nia ya kila upande.
Kwa mujibu wa mkataba huo, nchi hizo mbili zitajenga vituo viwili vya kuzalisha umeme nchini Iran, kila kimoja kina uwezo wa kuzalisha megawati elfu mbili kwa moto na kingine kina uwezo wa kuzalisha megawati elfu kumi kwa nishati ya maji. Nchini Uturuki pia kitajengwa kituo kimoja chenye uwezo wa megawati elfu mbili kwa nishati ya moto. Waziri wa nishati wa Iran Parviz Fattah kwenye sherehe ya kusaini makubaliano alisema, ingawa mkataba huu unazichukiza baadhi ya nchi, lakini Iran na Uturuki ni nchi huru, mkataba huo umesainiwa kwa kanuni za kunufaishana.
Ushirikiano wa kinishati kati ya Uturuki na Iran ulianza katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita. Tarehe 13 Julai nchi hizo mbili zilisaini mkataba wa ushirikiano wa kinishati. Kwa mujibu wa mkataba huo, Uturuki inaruhusiwa kushiriki kwenye uchimbaji wa gesi kwenye sehemu ya kusini ya Fars bila kupitia zabuni, na gesi inayochimbwa itauzwa kwa Iran. Zaidi ya hayo, kuanzia mwaka 2008 Iran na Turkmenistan kila mwaka zinasafirisha gesi mita za ujazo bilioni 30 hadi Ulaya kupitia Uturuki. Wachambuzi wanaona kuwa mbele ya upinzani mkali wa Marekani nchi hizo mbili zinaendelea na ushirikiano hakina zina sababu nyingi.
Kwanza ni mahitaji ya kiuchumi. Iran ni nchi yenye utajiri mkubwa wa nishati, akiba ya mafuta na gesi ya nchi hiyo inaongoza duniani. Lakini Uturuki na uhaba wa nishati, asilimia zaidi ya 90 ya mafuta na gesi inategemea kutoka nchi za nje. Ingawa Uturuki inapakana na Iraq, nchi yenye utajiri wa nishati, lakini kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo uwezekano wa ushirikiano wa kinishati kati ya Uturuki na Iraq ni mdogo, kwa hiyo Uturuki inashirikiana na Iran, na ushirikiano huo pia unaweza kusaidia Iran kufidia hasara inayosababishwa na vikwazo vya kiuchumi vya jumuiya ya kimataifa. Kutokana na mahitaji ya kila upande, katika miaka ya karibuni thamani ya biashara kati ya Uturuki na Iran imefikia ya dola za Kimarekani bilioni 7, na mwishoni mwa mwaka huu ingeweza kufikia bilioni 10. Ushirikiano wa kinishati hakika utaongeza zaidi thamani ya biashara kati ya pande mbili.
Pili ni mahitaji ya kisiasa. Kwa upande wa Iran, kuwa karibu na Uturuki, nchi ambayo ina athari yake katika Ulaya na hasa ni nchi rafiki na Marekani, inaweza kupunguza shinikizo la kimataifa.
Kwa upande wa Uturuki, ushirikiano kati yake na Iran unaweza kujiletea matokeo ya "kuua ndege watatu kwa jiwe moja". Kwanza, unasaidia usalama wa nishati nchini na kuinua hadhi ya kisiasa ya kikanda na kimataifa. Pili, ni unasaidia kuongeza uzito wa kisiasa katika mapatano na Marekani katika mapambano dhidi ya chama cha wafanyakazi cha Wakurdstan. Tatu, unasaidia kuboresha uhusiano wa kisiasa na nchi za Uturuki na nyingine za Asia ya Kati kwa kupitia Iran.
Wachambuzi wanaona kuwa ingawa hivi sasa nchi hizo mbili zinashirikiana katika sekta ya nishati, lakini ushirikiano wao hakika utakuwa na vikwazo, na vikwazo hivyo vinatokana zaidi na Marekani. Marekani siku zote inapinga ushirikiano wa kinishati kati ya Uturuki na Iran kwa sababu ushirikiano huo utaharibu mkakati wake wa kisiasa katika suala la nyuklia la Iran. Balozi wa Marekani nchini Uturuki Bw. Ross Wilson alisema kama Uturuki ikiacha ushirikiano na Iran Marekani itaiunga mkono Uturuki kuchimba nishati ya Iraq na Asia ya Kati, lakini Uturuki haijajibu lolote kuhusu pendekezo hilo.
Zaidi ya hayo, hivi karibuni baraza la chini la Marekani limepitisha azimio ambalo litayawekea vikwazo makampuni yatakayowekeza nchini Iran kwa zaidi ya dola za Kimarekani milioni 20. Kwa hiyo Uturuki ikitimiza ushirikiano na Iran pia itakumbwa na vikwazo.
Idhaa ya kiswahili 2007-11-21
|