Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-21 20:17:32    
Mapishi ya kuku na limao

cri

Mahitaji:

Nyama ya kuku gramu 300, wanga gramu 100, maji juisi ya limao gramu 250, sukari gramu 30, nyanya gramu 100, chumvi gramu 3, mvinyo wa kupikia gramu 5, vitunguu maji gramu 3, tangawizi gramu 3.

Njia:

1? Osha nyama ya kuku halafu uikate iwe vipande, koroga pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, pilipili manga, tangawizi na vitunguu maji. Koroga maji juisi ya limao pamoja na unga, chumvi, pilipili manga, yai na mafuta.

2? Washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, weka vipande vya nyama ya kuku kwenye unga uliokorogwa, halafu weka ndani ya sufuria vikaange, halafu vipakue.

3? Washa moto tena, mimina maji kwenye sufuria, halafu tia chumvi, sukari, maji juisi ya limao, korogakoroga halafu mimina maji ya wanga, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya kuku korogakoroga vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.