Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-22 16:58:29    
Mfuko wa Song Qingling wa China (sehemu ya pili)

cri

Watoto wa familia za mijini, kila mmoja ni mtoto pekee katika familia yake. Wazazi wao wanawapenda sana. Mfuko wa Song Qingling uliandaa kambi ya majira ya joto kwa watoto hao, ili kutoa fursa ya kuwapa uwezo katika maisha.

Tofauti na kambi nyingine za majira ya joto, kambi ya majira ya joto iliyoandaliwa na mfuko huo ilichagua mbuga ya mkoa wa Mongolia ya ndani ambayo iko mbali na mjini. Kila siku watoto hao walitembea kilomita 10 wakiwa wamebeba mizigo yenye uzito wa kilo zaidi ya 10, pia walipaswa kupika wenyewe na maji wanayopata ni yenye kikomo. Shughuli hizo zilikuwa changamoto kubwa kwa watoto hao.

Watoto wawili kutoka Beijing Yunzong na Yunbei wenye umri wa miaka 11 ni mapacha. Mwaka jana walijiandikisha kwenye kambi hii ya majira ya joto. Ingawa walipata matatizo mengi katika kambi hiyo, lakini walipozungumzia safari hiyo walifurahi sana. Yunzong alisema:

"Mambo mengi katika kambi hiyo ya majira ya joto hatukuwahi kuyaona hapo kabla. Tuliongeza uwezo watu katika maisha kutokana na shughuli hizo. Kwa hivyo ninaona kambi hii ina umuhimu sana."

???Mfuko wa Song Qingling pia unafuatilia sana ukuaji wa watoto wa vijijini na sehemu zenye matatizo ya kiuchumi. Kutokana na kuwa hali ya matibabu na afya katika sehemu zilizoko magharibi mwa China si nzuri, mfuko huo ulianzisha "mpango wa afya ya mama na watoto walioko magharibi mwa China", ili kutoa matibabu kwa mama na watoto wa vijijini; katika mikoa ya Shanxi, Ningxia, na Chongqing, mfuko huo pia ulianzisha "mpango wa kuwaandaa walimu wa magharibi", kuwasaidia walimu wa shule ya msingi wa vijijini kupata elimu zaidi, ili kuinua kiwango cha ufundishaji wa walimu.

Watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini pia wanafuatiliwa na mfuko huo. Katika jumba la sayansi na teknolojia kwa watoto la Song Qingling, mfuko huo ulianzisha kituo cha ujuzi wa sayansi kwa watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, ili kuwasaidia watoto hao waweze kuelewa zaidi ujuzi wa sayansi. Katika siku ya watoto ya mwaka huu, mfuko huo uliwaandalia watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini mashindano ya mfano wa magari yanayotumia nishati ya jua, ili kuongeza ujuzi wao katika mambo ya maisha yao baada ya masomo. Liu Rong alitoka kwenye kijiji cha mkoa wa Anhui, yeye alikuja kushiriki kwenye mafunzo kabla ya mashindano hayo. Kabla ya miaka miwili iliyopita, baba na mama yake walikuja Beijing na kufanya kazi hapo, na yeye alikuwa anasoma mjini Beijing.

Alitengeneza aina moja ya gari linalotumia nishati ya jua lenye ukubwa karibu sawa na gari dogo la kuchezea watoto, aina hiyo ya gari ikiwekwa ardhini kwenye mwangaza wa jua, inaweza kwenda mbele kwa mwelekeo uliowekwa.

Liu Rong alisema shughuli hizo zinamvutia sana na hajashiriki kwenye shughuli kama hizo katika maskani yake.

"Nimepata mengi kutokana na shughuli hizo, ninaona furaha kubwa nje ya darasa. Nina matumaini ya kushiriki kwenye shughuli nyingine nyingi kama hii katika siku za usoni."

Katibu mkuu wa Mfuko wa Song Qingling Bw. Li Ning alisema katika siku za usoni watatoa kipaumbele kwa watoto wa vijijini na sehemu zenye matatizo ya kiuchumi, na kufanya shughuli nyingi zaidi ili kuhimiza watoto wakue vizuri. Alisema:

"Kuna watoto wengi wanaobaki vijijini ambao wazazi wao wanafanya kazi za vibarua mijini. Katika sehemu zenye matatizo ya kiuchumi, kuna masuala mengi kama vile huduma duni za matibabu. Tunapaswa kuzingatia zaidi masuala hayo na kuongeza nguvu katika kutatua masuala hayo."

Idhaa ya kiswahili 2007-11-22