Hivi karibuni serikali ya Nigeria ilikataa makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani yaliyoanzishwa majuzi kuweko nchini humo, hatua ambayo inafanya shughuli za kutafuta sehemu mpya ya kuweka makao makuu hayo kukumbwa na matatizo tena.
Serikali ya Nigeria siku zote inapinga jeshi la Marekani kujenga makao makuu ya uongozi barani Afrika. Tarehe 19 mwezi Novemba rais Umaru Yar'adua alikuwa na mkutano pamoja na wabunge wa bunge la taifa na magavana kuhusu suala hilo. Baada ya mkutano huo, gavana wa jimbo la Kwara Bw. Bukola Saraki akieleza msimamo wa mwisho wa Nigeria akisema, Nigeria licha ya kupinga jeshi la Marekani kujenga makao makuu ya uongozi katika nchi yake, pia inapinga jeshi la Marekani kujenga makao makuu ya uongozi katika nchi nyingine za Afrika ya magharibi.
Rais George Bushi wa Marekani aliidhinisha mpango wa kujenga makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani barani Afrika mwezi Februari mwaka huu, jeshi la Marekani lilitangaza tarehe 2 mwezi Okatoba kuwa makao makuu ya jeshi la Marekani barani Afrika yameanzishwa rasmi na kuanza baadhi ya shughuli zake. Lakini shughuli za kutafuta mahali ma kujengea makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani haziungwi mkono barani Afrika. Nchi za Algeria, Moroco na Libya za Afrika ya kaskazini, Uganda ya Afrika ya mashariki pamoja na nchi wanachama 14 wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, zimeeleza wazi kuwa hazitaki makao makuu hayo yajengwe katika nchi zake au kutoa kituo cha kijeshi cha kudumu kwa jeshi la Marekani.
Ofisa mmoja wa wizara ya ulinzi ya Nigeria alisema, shauku ya serikali ya Marekani kuhusu ghuba ya Guinea inaifanya Nigeria ichukue hatua madhubuti ili kuhakikisha usalama wa lazima wa sehemu hiyo. Alisema, viongozi wa Nigeria wanaona kuwa, Marekani inadai kupambana na tishio la ugaidi, hiki ni kisingizio tu, na ni udhuru wa Marekani wa kujenga kituo cha jeshi la Marekani. Habari zinasema serikali ya Nigeria inaona kuwa lengo la Washington ni kutaka kuchukua mafuta ya asili. Ili kuzuia rasilimali za sehemu hiyo zisidhibitiwe kabisa na Marekani, serikali ya Nigeria imekuwa na mazungumzo na wakuu wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika na umoja wa uchumi wa Afrika ya magharibi ili kujadili namna ya kuzuia Marekani kuweka askari wengi kwenye ghuba ya Guinea.
Nchi za Afrika hazina imani na lengo la jeshi la Marekani kujenga kituo chake barani Afrika, kwanza zina wasiwasi kuwa huenda mamlaka za nchi zake zitaharibiwa. Zinaona kuwa baada ya jeshi la Marekani kujenga makao makuu ya uongozi na kuweka idadi kubwa ya askari barani Afrika, litaingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika, na nchi hizo zitapoteza mamlaka na udhibiti wa rasilimali zake. Marekani ikiwa ni nchi kubwa pekee yenye mabavu, inapenda kutatua masuala kwa njia ya kijeshi, ambayo inaleta wasiwasi kwa nchi nyingi za Afrika, n chi hizo zinaona huenda Marekani itaangusha serikali isiyoipenda kwa njia ya kijeshi.
Pili, maofisa wa Marekani wanapozungumza sana kuhusu uhusiano wa wenzi wa ushirikiano kati ya Marekani na nchi za Afrika, nchi za Afrika zinaamini kuwa lengo la Marekani la kufanya hivyo ni kwa ajili ya maslahi yake zaidi. Kwani Afrika imekuwa sehemu ya kwanza ya kununua mafuta ya asili ya petroli mwaka 2006 badala ya sehemu ya mashariki ya kati. Mafuta ya petroli yanayonunuliwa na Marekani kutoka Nigeria na Angola ni kiasi cha mapipa milioni 1.5 kwa siku, kikiwa ni 16% ya mafuta yanayonunuliwa kutoka nchi za nje. Licha ya hayo, mudai unaotumiwa wa kusafirisha mafuta kutoka Afrika hadi Marekani ni nusu tu ya muda kutoka Mashariki ya kati. Kwa kulinganishwa na mafuta ya asili ya petroli ya pwani ya bahari ya Caspian na sehemu ya Marekani ya kusini, kununua mafuta kutoka Afrika ni vizuri zaidi iwe kwa hali ya utulivu na gharama. Nchi za Afrika zinaona kuwa Marekani ilichukua hatua za kijeshi kuhusu sehemu muhimu zenye nishati iwe ni Afghanistan au Iraq, hali kadhalika kwa bara la Afrika.
Nchi za Afrika zinataka masuala ya Afrika yatatuliwe na Umoja wa Afrika, wala siyo kuingiliwa na nchi za nje. Marekani ikitumia kisingizio cha kupambana na ugaidi duniani, inafanya upanuzi wa kijeshi, bila shaka itachukiwa, na kutoaminiwa na nchi za Afrika. Kitu kinachofuatiliwa na nchi za Afrika ni suala la maendeleo, kuweko kwa jeshi la Marekani hakutaweza kutatua suala la umaskini, na kujenga makao makuu ya uongozi ya jeshi la Marekani kabisa siyo njia sahihi ya kuisaidia Afrika
|