Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-27 09:48:14    
Sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining

cri

Mkoa wa Qinghai uko kaskazini magharibi mwa China, na pia kaskazini mashariki ya uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, ambako ni chanzo cha mito mikubwa nchini China ikiwa ni pamoja na Mto Changjiang na Mto Manjano, pia ni mmoja kati ya mikoa inayotekeleza mkakati wa uendelezaji wa sehemu ya magharibi ya China. Sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining, ni eneo pekee la uendelezaji wa uchumi na teknolojia la ngazi ya taifa mkoani Qinghai. Katika miaka ya hivi karibuni, eneo hilo limekuwa linavutia kwa maendeleo ya uchumi ya Qinghai.

Sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining ilianzishwa rasmi mwezi Julai mwaka 2000. Wakati huo, serikali ya mji ilitenga Yuan za RMB laki 1 tu, na waanzilishi wa sehemu hiyo walianza shughuli zao katika hali ngumu, na ambapo hata walikuwa hawana nyumba hata moja ya kiwanda. Lakini baada ya juhudi za miaka 7, sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining imejenga kwa hatua za mwanzo mfumo za viwanda ambao kazi yake kule ni uyeyushaji wa madini, kemikali, utengenezaji wa mashine, vifaa vya ujenzi, uzalishaji wa dawa, mazao ya kilimo yasiyo na uchafuzi na dawa za kusaidia afya. Viwanda na makampuni yaliyoingia katika sehemu hiyo yamezidi 500, na kufanya uwekezaji kwenye mali zisizohamishika wenye thamani ya zaidi ya Yuan za RMB bilioni 10, na kuwasaidia watu karibu 20,000 kupata ajira moja kwa moja. Naibu mkurugenzi wa kamati ya mpango wa uchumi ya Qinghai Bw. Chen Zhizhong, alipozungumzia namna maendeleo ya sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining yanavyohimiza maendeleo ya viwanda mkoani Qinghai, alisema,

"Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya uchumi wa viwanda mkoani Qinghai imekuwa inaendelezwa vizuri. Mwaka 2006, viwanda vikubwa mkoani humo vilipata faida ya Yuan za RMB bilioni 24.03. Matokeo hayo yanatokana na ongezeko la viwanda vya sehemu muhimu, hasa ongezeko la viwanda mjini Xining limefikia asilimia 25.5, ambalo lilichukua nafasi ya kwanza mkoani Qinghai."

Ofisa huyo alisema, sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining imefanya kazi ya vielelezo katika kurekebisha na kuboresha muundo wa uchumi na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa mkoa huo. Maendeleo ya kasi ya sehemu hiyo hayawezi kutengana na mkakati wa maendeleo uliochukuliwa na idara ya usimamizi wa sehemu hiyo. Ofisa mhusika wa sehemu hiyo Bw. Guo Tianming anaona kuwa, kutilia maanani kuingiza teknolojia ya kisasa ya uzalishaji na wazo la maendeleo ni moja ya sababu muhimu za sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining kupata mafanikio. Alisema,

"Mkoa wa Qinghai una upungufu wa fedha, lakini naona tatizo kubwa ni kukosa mawazo ya kuendeleza sehemu hiyo yaani kuingiza mawazo ya kisasa kutoka nje, raslimali za kisasa za mtandao wa uuzaji na njia ya kisasa ya usimamizi; kuendeleza sehemu hiyo ni kutumia nguvu bora ya maliasili za huko, ili kujenga eneo kubwa la viwanda, na kutoa vielelezo na kuhimiza maendeleo."

Kwa kuelekezwa na mawazo hayo mapya ya maendeleo na utaratibu wa uendelezaji, katika mwaka mmoja baada ya kuanzishwa kwa sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining, sehemu hiyo imepata maendeleo makubwa katika ujenzi wa miundo mbinu, ujenzi wa miradi ya viwanda, kuvutia wawekezaji pamoja na usimamizi wa sehemu hiyo.

Kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Bozhong ya Qinghua iliingia kwenye sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining mwaka mmoja uliopita, ni kampuni inayoendeleza maliasili ya matunda ya seabuckthom. Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Lu Changzheng anaona kuwa, sehemu hiyo sio tu ni kituo muhimu cha kuimarisha uchumi wenye umaalum na shughuli zenye nguvu bora, bali pia ni sehemu muhimu kwa mkoa wa Qinghai kutimiza mchakato wa kuendeleza viwanda vya aina mpya. Alisema:

"Tumekaa mkoani Qinghai kwa mwaka mmoja, lakini tumeona kuwa uchumi wa sehemu hii unaendelezwa kwa kasi, hali ya maendeleo ni nzuri, huenda hii ni fursa nzuri kwa uchumi wa Qinghai kupata maendeleo halisi. Naona mkoa wa Qinghai ukitaka kuwa na maendeleo ya kasi zaidi, ni lazima uwe na mkusanyiko wa viwanda vyenye nguvu kwa mkoa huo, ambao unakusanya viwanda vinavyofanana na vinavyohusika katika sehemu moja. Mkusanyiko huo unaweza kuongeza nguvu ya kampuni moja kuwa nguvu ya makampuni mengi katika sehemu moja."

Hivi sasa sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining imekuwa jukwaa muhimu la mkoa wa Qinghai kufungua mlango na kushirikiana na nchi za nje. Kampuni ya mradi wa viumbe ya Mingxing ya Qinghai ni kampuni iliyowekezwa na wafanyabiashara kutoka Taiwan. Meneja mkuu wa kampuni hiyo anayetoka Taiwan Bw. Zhao Xia alisema,

"Nimekaa hapa Xining kwa zaidi ya miaka minne, naona msingi wa mkoa wa Qinghai bado ni dhaifu, lakini naona kuwa sehemu hiyo ina nia imara na msimamo sahihi wa kujiendeleza kuliko sehemu za ndani za China. Serikali za ngazi mbalimbali mkoani Qinghai zina moyo wa dhati wa kuvutia wawekezaji. Serikali inatilia maanani sehemu ya uendelezaji wa uchumi, na kutoa sera zenye unafuu; aidha mtizamo wa utoaji wa huduma wa huko ni mzuri kuliko sehemu nyingine, hivyo huduma zinazotolewa na idara za usimamizi za serikali ya sehemu ya Xining ni kamili zaidi."

Katika miaka ya karibuni, mkoa wa Qinghai umekuwa unakamilisha sera ya kuendeleza sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia, na kuharakisha uingizaji wa miradi yenye sifa nzuri. Kutokana na uhimizaji wa serikali, uingizaji wa mitaji na sifa yake kwenye sehemu hiyo unainuka siku hadi siku. Inakadiria kuwa, hadi kufikia mwaka 2010, thamani ya jumla ya uzalishaji wa sehemu ya uendelezaji wa uchumi na teknolojia ya Xining itafikia Yuan za RMB bilioni 13.5; na kuwasaidia watu zaidi ya 50,000 kupata ajira.

Idhaa ya kiswahili 2007-11-27