Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-28 15:39:20    
Familia kubwa ya kabila la Warussia

cri

Kwenye mji wa Yining wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang, kuna familia moja ya kabila la Warussia yenye watu wengi, wakiwemo bibi Nina, Bw. Nicola ambaye ni mkuu wa shule ya kabila la Warussia, na Bw. Alexander ambaye anaendesha kituo cha kutengeneza kodiani, Bibi Dina mwenye duka la mikate, na watu wengine wengi. Leo tutawaletea maelezo kuhusu familia hiyo.

Bibi Nina mwenye umri wa miaka 76 anatoka kabila la Warussia nchini China. Waanzilish wa kabila hilo walikuwa ni warussia, na waliohamia China mwishoni mwa karne ya 18. Wazazi wa Bibi Nina walikwenda mkoani Xinjiang zaidi ya miaka 70 iliyopita. Baada ya kuolewa, Bibi Nina alizaa na kulea watoto 16. Alisema,

"Sasa mimi nina watoto wa kiume wanane na wa kike wanne, wengine wamefariki dunia, tunaishi maisha mazuri."

Baadhi ya watoto wa Bibi Nina walikwenda nchi za nje, na wengine wanafanya kazi ya utafsiri kwenye miji mingine nchini China, sasa wanaoishi pamoja naye ni watoto watano. Binti yake mdogo Rida alipata mtoto mwaka jana, na sasa hajaenda kutafuta kazi, alipokumbuka alipokuwa mtoto, alisema,

"Nilizaliwa mwaka 1971, nina dada na kaka wakubwa wengi. Tulipokuwa watoto, tulicheza vizuri kila siku."

Mume wa Bibi Rida Bw. Nicola ni mkuu wa shule ya kabila la Warussia mjini Yining. Shule hiyo ni shule pekee ya kabila la Warussia mjini Yining, pia ni shule pekee inayofundisha wanafunzi kwa lugha mbili za Kichina na Kirussia mkoani Xinjiang. Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1985, na sasa ina wanafunzi zaidi ya 130. Bw. Nicola alieleza kuwa shule hiyo imeweka masomo mbalimbali kwa mujibu wa utaratibu wa elimu nchini China, na kufundisha wanafunzi kwa lugha mbili za Kichina na Kirussia, alisema,

"Kutokana na matakwa ya wakazi wa kabila la Warussia na utafiti wa idara za elimu, mwaka 1997 shule hiyo iliamuliwa kuwa ya shule inayofundisha watoto kwa lugha mbili. Lugha ya Kirussia ni somo muhimu katika shule hiyo, kila wiki kuna vipindi vitano hadi saba vya lugha ya kirussia ."

Bw. Alexander mwenye umri wa miaka 48 ni mtoto wa nne wa Bibi Nina. Kila siku baada ya kuwapeleka watoto wake shuleni, anaanza kazi kwenye kituo chake cha kutengeneza kodiani. Bw. Alexander si fundi hodari wa kutengeneza kodiani tu, bali pia ni hodari katika kupiga muziki kwa ala hiyo mjini Yining.

"Wazazi wangu pia walijifunza muziki, mama yangu alikuwa anapiga muziki kwa ala ya trigon, na baba yangu alikuwa anapiga gitaa na kodiani. Nilianza kupenda ala za muziki nilipokuwa mtoto."

Bw. Alexander aliwahi kutembelea Beijing, Ulumuqi na miji mingine na kupiga kodiani kwa wasikilizaji, pia akiwa na nafasi anatunga muziki mwenyewe. Binti yake mdogo Rita anastaajabu sana uwezo wa baba yake, alisema,

"Naona baba yangu ana uwezo mkubwa. Ingawa ana wateja wengi kila siku, lakini anatunga muziki. Muziki mzuri zaidi aliyotunga ni muziki wa sehemu tatu kuhusu Mto Yili. Anapiga muziki huyo mara kwa mara nyumbani, ninaupenda sana."

Wakazi wengine wa mji wa Yining wanasema Bw. Alexander ni mtu anayeuchukulia muziki kama maisha yake. Kituo chake cha kutengeneza kodiani kimeanzishwa kwa miaka zaidi ya 20, lakini historia ya Bw. Alexander ya kutengeneza ala hiyo ndefu zaidi alisema,

"Nilianza kujifunza kutengeneza kodiani nilipokuwa na umri wa miaka 15. Zamani baba yangu pia alikuwa fundi wa kutengeneza kodiani, alinifundisha ufundi huo."

Kituo cha Bw. Alexander cha kutengeneza kodiani kilianzishwa mwaka 1990, kabla ya hapo aliwahi kufanya kazi ya kutengeneza kodiani kwenye miji kadhaa ya mkoa wa Xinjiang ikiwemo Tacheng, Alatai na Ulumuqi. Hivyo mkoani Xinjiang watu wengi wanamjua Bw. Alexander kwa ustadi wa kutengeneza kodiani.

Lililoko jirani na kituo cha Bw. Alexander ni duka la mikate la bibi Dina. Dina ni binti mkubwa wa Bibi Nina. Zamani alijaribu kuendesha duka la nguo na vitu vidogo vya sanaa, lakini hakupata wateja wengi. Mwishowe aliamua kuanzisha duka hilo la mikate. Kwa kuwa mama yake amemfundisha njia nzuri ya kutengeneza mikate. Bibi Dina anaweza kutengeneza mikate yenye umaalumu wa kirussia, anatia vitu vingi vizuri kwenye mikate yake vikiwemo mafuta maalumu, mayai, sukari na mhopi, hivyo duka lake linawavutia wateja wengi kila siku. Watu wanapenda mikate anayoitengeneza na wananunua mikate mingi.

Bibi Lima alikuwa mke wa mtoto mkubwa wa Bibi Nina. Kwa bahati mbaya mtoto huyo alifariki dunia kwa ugonjwa miaka micheche iliyopita. Sasa ingawa bibi Lima ameolewa tena, lakini mara kwa mara anatembelea familia kubwa ya Bibi Nina. Alisema,

"Niliolewa tena na kuhama. Lakini nina watoto na jamaa wengine katika familia hiyo kubwa. Ninakuja hapa kila siku kuwatembelea."

Binti mdogo wa Bibi Nina Rida aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, ndugu wa familia hiyo wanapendana sana, na wana hisia kubwa kwa familia hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2007-11-28