Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-28 15:51:48    
Mapishi ya pilipili mboga na ngisi

cri

Mahitaji

Pilipili mboga gramu 250, ngisi gramu 250, chumvi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, maji ya wanga vijiko vitatu, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, kiasi kidogo cha vitunguu maji na tangawizi

Njia

1. kata pilipili mboga ziwe vipande, kata ngisi awe vipande.

2. chemsha maji, halafu tia slesi ya pilipili mboga kwenye maji, korogakoroga, ipakue. Na tia vipande vya ngisi kwenye maji korogakoroga, ipakue.

3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, tia vipande vya pilipili mboga na ngisi, korogakoroga, halafu tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mvinyo wa kupikia, maji ya wanga, korogakoroga, halafu mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.