Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-29 20:10:15    
Manowari ya jeshi la China yafanya ziara ya kirafiki nchini Japan

cri

   

Wasikilizaji wapendwa, manowari yenye makombora iitwayo "Shenzhen" ya jeshi la China iliwasili Tokyo, Japan tarehe 28 asubuhi, na kuanza ziara ya kirafiki ya siku 4 nchini humo. Hii ni mara ya kwanza kwa manowari ya jeshi la baharini la ukombozi la watu wa China kutembelea Japan, ambayo inafungua ukurasa mpya wa maingiliano kati ya China na Japan katika eneo la ulinzi.

Mnamo saa 4 ya asubuhi ya tarehe 28 mwezi Novemba, huku muziki ukipigwa na bendi ya jeshi la Japan, manowari ya "Shenzhen" ikiongozwa na manowari ya ulinzi iitwayo "Ikazuchi" ya Japan, iliingia kwenye ghuba ya Tokyo, na kutia nanga kwenye gati la Harumi. Sherehe ya mapokezi ilifanyika kwenye gati hilo. Maofisa wa wizara ya ulinzi na mambo ya nje za Japan, maofisa na askari wa kikosi cha ulinzi cha baharini, wajumbe wa jumuiya ya urafiki ya Japan na China pamoja na wafanyakazi wa ofisi ya ubalozi wa China nchini Japan, waliikaribisha manowari ya "Shenzhen". Mkuu wa kikosi cha ulinzi cha baharini cha Japan jenerali Eiji Yoshikawa alitoa hotuba akisema,

 

"Ziara hii ya 'Shenzhen', si kama tu itaimarisha maelewano na uhusiano wa kirafiki kati ya kikosi cha ulinzi cha baharini cha Japan, bali pia itafanya kazi muhimu ya kuimarisha na kuhimiza uhusiano wa urafiki wa ujirani mwema kati ya Japan na China."

Manowari hiyo ya kivita inayoitembelea Japan ni manowari kubwa ya kivita ya kisasa iliyosanifiwa na kutengenezwa na China. Tangu manowari hiyo ianze kutumika mwezi Aprili mwaka 1999, ilifanya ziara ya kirafiki katika nchi 13 za Asia, Afrika na Ulaya. Balozi wa China nchini Japan, Bw. Cui Tiankai alitoa hotuba akisema,

"Jeshi la China ni jeshi la kulinda amani na jeshi la kistaarabu, tunawakaribisha marafiki wa sekta mbalimbali za nchini Japan watembelee manowari hiyo, na kuzungumza na maofisa na askari wa China, waone sura mpya ya jeshi na wanajeshi wa China, na kuifahamu China yenye mabadiliko na maendeleo kwa mfululizo."

Mkuu wa manowari hiyo meja jenerali Xiao Xinnian, akitoa hotuba alisema,

Manowari ya "Shenzhen" imechukua wanajeshi 345, urafiki wa watu wa China bilioni 1.3 pamoja na matarajio ya amani na masikilizano. Ninaamini kabisa kuwa, maingiliano ya wanajeshi na pande zetu mbili, pamoja na maingiliano kati yetu na wakazi wa hapa, bila shaka yataimarisha maelewano ya pande mbili na kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya China na Japan, na kutoa mchango kwa ajili ya kubadilisha bahari kubwa inayounganisha China na Japan kuwa bahari ya amani, urafiki na ushirikiano."

       

Watu waliofika huko kushiriki kwenye sherehe ya mapokezi ni pamoja na marafiki wengi wa Japan, wajapani wenye asili ya China na wachina wanaoishi huko, ambao wanafuatilia sana ziara hiyo ya manowari ya China. Mzee mjapani aliyewahi kujiunga na jeshi la anga la jeshi la ukombozi la umma la China, Bw. Sunahara Megumu alisema,

"Tumekuwa tunasubiri siku hii kwa miaka mingi, nimefurahi sana. Wenzangu wengi niliokuwa nao vitani, walitokwa na machozi. Kwa wanajeshi, maingiliano ya kijeshi ya pande hizo mbili ni jambo linalotarajiwa sana. Si rahisi kufikia hatua ya maingiliano ya mambo ya kijeshi."

Mwanamke mmoja mjapani alikuja pamoja na mtoto wake, alisema,

"Ninatarajia kuwa urafiki kati ya Japan na China utaimarishwa zaidi katika siku za baadaye. Ninaipenda sana China, nimempeleka mtoto wangu katika shule ya Zhonghua kujifunza lugha ya Kichina, ninataka mtoto wangu amalize kazi ambayo hatujaimaliza, na kuwa daraja ya urafiki kati ya Japan na China."

Baada ya kumalizika kwa sherehe ya mapokezi, bendi ya jeshi la baharini la China na bendi ya kikosi cha ulinzi wa baharini cha Japan zilifanya maonesho ya muziki kwa pamoja.