Rais Pervez Musharraf wa Pakistan tarehe 29 baada ya kuapishwa kuwa rais wa Pakistan bila wadhifa wa kijeshi, alisema tarehe 16 Desemba ataondoa amri ya hali ya hatari nchini Pakistan, na kuacha kufuata katiba ya muda iliyotangazwa kabla ya hapo.
Asubuhi ya tarehe 29 Bw. Pervez Musharraf aliyejiuzulu wadhifa wa mkuu wa jeshi aliapishwa kuwa rais wa Pakistan kwa kipindi kipya cha miaka mitano bila kuwa na wadhifa wa kijeshi. Jaji mkuu wa mahakama kuu ya Pakistan Bw. Hameed Dogar aliendesha sherehe ya kuapishwa kwake. Kwenye sherehe hiyo Bw. Pervez Musharraf alisema Pakistan imetoka kwenye dhoruba ya kisiasa, na yeye kuwa rais bila wadhifa wa kijeshi ni kumbukumbu ya historia ya Pakistan. Alisema anaamini kuwa Pakistan itabadilika na kuwa na nguvu zaidi.
Jioni ya siku hiyo, Bw. Pervez Musharraf alitoa hotuba kwa njia ya televisheni na redio akisema, hivi sasa tishio la ugaidi linaloikumba Pakistan limeathiri maendeleo ya uchumi, na baadhi ya vyombo vya habari vinachangia tishio hilo, hali ya hatari ililazimika kutangazwa, na hatua hiyo ilipata idhini ya vyombo vya sheria na hatua hiyo ilihakikisha taifa linaendelee kama kawaida. Aliahidi kuwa tarehe 16 Desemba ataondoa amri ya hali ya hatari na kufufua katiba ya taifa. Bw. Musharraf alisema, hivi sasa kazi muhimu ni uchaguzi wa bunge. Alivitaka vyama vyote vya kisiasa vishiriki kwenye uchaguzi huo na kuahidi kwamba atahakikisha kwa juhudi zote uchaguzi utafanyika tarehe 8 Januari mwaka kesho kama ilivyopangwa. Alasiri ya siku yiyo, vikwazo barabarani mjini Islamabad vilianza kuondolewa, na barabara ya "katiba" iliyofungwa kabla ya hapo imefunguliwa, na walinzi kwenye idara za serikali wameondolewa.
Jumuyia ya kimataifa imempongeza Bw. Musharraf kwa kuapishwa kuwa rais wa kipindi kipya. Rais Hu Jintao wa China tarehe 29 alimtumia salamu za pongezi. Bw. Musharraf alimwambia balozi wa China aliyealikwa kwenye sherehe ya kuapishwa kwake Bw. Luo Zhaohui kwamba, kuwa na urafiki na China ni jiwe la msingi wa mkakati wa mambo ya nje kwa Pakistan, na pia ni maoni ya pamoja ya vyama visivyo tawala. Alisema katika kipindi kipya Pakistan itaendelea kuthamini uhusiano kati yake ya China na kusukuma mbele ushirikiano katika sekta mbalimbali. Alisema ana imani kubwa kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili utakuwa mzuri zaidi.
Wachambuzi wanaona kuwa sababu ya Bw. Musharraf kutangaza kuondoa amri ya hali ya hatari nchini Pakistan mara tu baada ya kuwa rais ni nyingi, licha ya kufufua mchakato wa demokrasia na kuboresha hali ya usalama, pia inatokana na shinikizo la kisiasa kutoka ndani na nje ya Pakistan. Mwanzoni alipotangaza Pakistan kuingia kwenye hali ya hatari, Jumuyia ya Madola ilisimamisha uanachama, na nchi za Marekani na Uingereza pia zilitangaza kuwa zitafikiria upya misaada yao kwa Pakistan. Tarehe 28 baada ya Bw. Musharraf kujiuzulu wadhifa wa kijeshi rais George Bush alionesha kukaribisha hatua hiyo, lakini alimtaka aondoe amri ya hali ya hatari mapema iwezekanavyo. Watu wanaompinga na vikundi vya wanasheria mara nyingi walifanya maandamano wakipinga amri ya hali ya hatari nchini Pakistan. Kutokana na kuwa "Hekaheka za Demokrasia ya Vyama Vyote", APDM, zilizoongozwa na chama cha Muslim League zilitangaza kuwa, kama serikali haitatangaza kumaliza amri hali ya hatari, vyama vya harakati hizo havitashiriki kwenye uchaguzi wa bunge utakaofanyika tarehe 8 januari mwakani. Mwenyekiti wa chama kingine cha upinzani, Chama cha Umma, Bi. Benazir Bhutto pia alisema kama amri haitaondolewa kuna uwezekano wa kususia kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Wachambuzi wanaona kuwa kumaliza amri ya hali ya hatari licha ya kuweza kupunguza "shinikizo la kidemokrasia" la nchi za Magharibi kwa Pakistan, pa kunasaidia kusambaratisha muungano wa vyama vya upinzani kususia uchaguzi wa bunge.
Idhaa ya kiswahili 2007-11-30
|