Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-05 15:33:03    
Teknolojia ya Digital Family yaongoza njia ya maisha ya wachina katika siku za baadaye

cri

Kama tunaweza kutumia zana moja kudhibiti kutoka mbali vyombo mbalimbali vya umme nyumbani kama kompyuta na televisheni, maisha kama hayo si ni rahisi sana? Leo utawaelezeni kuhusu teknolojia ya Digital family inayojitahidi kutimiza lengo hilo.

Teknolojia ya Digital Family inawakilisha njia ya maisha katika siku za baadaye. Chombo muhimu katika mfumo wa Digital family ni kompyuta ya hali ya juu au televisheni yenye uwezo nyingi zinazounganishwa na kamera ya kitarakimu, simu za mkononi, sinema ya nyumbani na hata mfumo wa usalama kwenye mtandao wa upashanaji habari, mtandao wa matangazo ya televisheni na radio na mtandao wa Internet. Mfumo huo untawezesha watumiaji wadhibiti vyombo yote nyumbani kwa kutumia zana moja ya udhibiti kutoka mbali na kuweka mazingira ya kisasa ya maisha.

Wakati mfumo wa "Digital Family" ikijengeka, utaleta raslimali nyingi za burudani nyumbani. Televisheni ikiwa ni chombo cha umeme kinachomilikiwa kwa wingi zaidi kwenye familia za China, hivyo televisheni ni chombo muhimu katika mfumo huo, lakini si televisheni ya kawaida bali ni televisheni yenye picha safi. Televisheni ya aina hiyo si kama tu inainua sifa ya picha, bali muhimu zaidi ni kwamba ina vyanzo vingi zaidi vya kupokea matangazo. Televisheni ya kawaida inaunganishwa kwenye mtandao wa matangazo ya televisheni, lakini televisheni yenye picha safi ina soketi ya USB na inaweza kuunganishwa na kuonesha yaliyomo kwenye harddisk unayoweza kutembea nayo, pia televisheni hiyo inaweza kuunganishwa na kompyuta, pia inaweza kuunganishwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Internet na kuonesha video kwenye mtandao huo.

Kama hivyo, watumiaji wakichoka na vipindi vinavyotolewa kwenye mtandao wa matangazo ya televisheni, wanatumia zana ya udhibiti kutoka mbali tu, wataweza kuchagua na kuonesha matangazo wanayoyapenda kwenye mtandao wa Internet. Mkurugenzi wa bodi ya kampuni ya teknolojia ya mtandao wa njia pana ya Tianbo Bw. Lu Pin alisema:

"matangazo ya televisheni ni chanzo kidogo, yana vipindi 30 hadi 40 tu. Lakini mtandao wa Internet hauna mipaka, una chaguo nyingi zaidi."

Mbali na hayo, mfumo wa Digital Family pia unawezesha watumiaji kucheza michezo kwenye mtandao, michezo hiyo inatumia mfumo wa kutambua vitendo vya mwili na kuleta burudani kama unavyofanya michezo ya kweli. Kama vile utaweza kucheza bowling au mpira wa meza mbele ya skrini. Data za vitendo vyako zitatambuliwa na kutumiwa kwenye mashine ya michezo inayounganishwa kwenye mtandao wa Internet, kwa hivyo utaweza kucheza na mtu yeyote duniani bila kujali mahali alipo.

Teknolojia ya Digital Family pia inatoa huduma ya ulinzi nyumbani, ukiunganisha kemera na zana husika kupitia mtandao wa bila waya, mahali popote ulipo utaweza kuchunguza moja kwa moja hali ya nyumbani kwenye mtandao wa njia pana. Mkurugenzi wa mpango wa soko duniani wa kampuni ya upashanaji habari ya ZTE Bi. Wang Meili alisema:

"ninaweza kuangalia watoto na wazee nyumbani kupitia mfumo huo, au wakati hakuna watu nyumbani, pia nitaweza kuchunguza hali ya usalama nyumbani. Huduma hiyo hivi sasa imekuwa inakaribishwa sana nchini China na katika nchi za nje."

Wazo la Digital Family nchini China lilianzishwa mwishoni mwa karne iliyopita, lakini hivi sasa teknolojia hiyo bado iko kwenye kipindi cha maendeleo ya mwanzo nchini China. Mwezi Juni mwaka 2005, Wizara ya upashanaji habari ya China ilitangaza rasmi vigezo vya huduma ya kutumika kwa pamoja kwa raslimali kwenye zana za upashanaji habari, vinavyoitwa kwa ufupi IGRS. Hivyo ni "vigezo vya kwanza vya China" vilivyoanzishwa na kuvumbuliwa na makampuni ya China kwa ajili ya zana za upashanaji habari na vyombo vya umeme.

Naibu mkurugenzi wa bodi ya kampuni ya kituo cha mradi wa teknolojia za IGRS Bw. Liu Qingtao alisema, hivi sasa bidhaa zaidi ya 20 zinazotumia vigezo vya IGRS zimetolewa sokoni, zikiwemo kompyuta ya laptop, simu ya mkononi, televisheni ya IGRS na projekta. Mwaka 2006 kwa jumla bidhaa milioni 2 kati ya hizo ziliuzwa nchini China.

Wakati IGRS ilipoanzishwa miaka mitatu iliyopita, makampuni matano tu yalikuwa yanazalisha bidhaa husika, lakini hivi sasa idadi hiyo imeongezeka kufikia mia moja, na kila wiki kampuni moja mpya ya IGRS itaanzishwa. Bw. Liu Qingtao alisema:

"katika siku za baadaye, zana zote zinazotumia vigezo vya IGRS zikiwemo kompyuta, televisheni na simu za mkononi zitawekwa alama ya IGRS, watumiaji wakinunua zana zenye alama hiyo, wataziunganisha na kuunda mfumo wa Digital Family."

Idhaa ya kiswahili 2007-12-05