Mkutano wa 28 wa siku mbili wa Kamati ya Ushirikiano ya nchi za Ghuba ulifungwa tarehe 4 huko Doha, mji mkuu wa Qatar. Mkutano huo umetoa "Taarifa ya Doha" na kufikia makubaliano kuhusu uchumi na usalama wa kikanda. Kutokana na kuwa mkutano huo wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Kiarabu za Ghuba utatangaza soko la pamoja la nchi za Ghuba, mkutano huo unafuatiliwa sana. Kwenye ufungaji wa mkutano huo katibu mkuu wa Kamati Bw. Abdul Rahman al-Attiya alitangaza kuwa, mkutano huo umeamua kuanzisha soko la pamoja la nchi za Ghuba mwaka kesho. Alisema,
"Kamati kuu ya Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Ghuba inatangaza kuwa kuanzia tarehe mosi Januari mwaka 2008 soko la pamoja la Ghuba litaanzishwa."
Suala la soko la pamoja la Ghuba lilitolewa kwenye mkutano wa 23 uliofanyika mwaka 2002 kwa lengo la kuhakikisha haki sawa katika mambo ya makazi, kazi, uwekezaji, biashara, matibabu na elimu, na uliweka ratiba ya kuanzisha soko la pamoja mwishoni mwa mwaka 2007. Baada ya juhudi za miaka mitano, nchi wanachama wa Kamati hiyo ziliafikiana kuhusu soko hilo la pamoja. Akizungumza kuhusu soko hilo Bw. Rahman al-Attiya alisema,
"Lengo la kuanzisha soko la pamoja ni kupata 'soko moja' ili watu wa nchi zote za Ghuba wanufaike na uchumi wa Ghuba, kupanua eneo la uwekezaji ndani ya nchi wanachama na kutoka nchi za nje, kuongeza faida kutoka uchumi wa Ghuba, kuinua uwezo wa ushindani, kutumia maliasili kwa tija kubwa, kuinua hadhi ya nchi wanachama wa Kamati hiyo katika mazungumzo ya kimataifa na kuinua heshima katika uchumi duniani."
Cha kuzingatia zaidi ni kwamba rais wa Iran Bw Mahmoud Ahmadinejad alialikwa kuhudhuria mkutano huo. Vyombo vya habari vinaona kuwa nchi wanachama wa Kamati hiyo zina matumaini ya kuimarisha uhusiano na Iran, nchi muhimu jirani, ili kuhakikisha usalama na utulivu wa kikanda. Lakini hivi sasa kutokana na suala la nyuklia, uhusiano kati ya Iran na Marekani ni mbaya, na nchi wanachama wa kamatai ya ushirikiano ya nchi za Ghuba zina uhusiano mzuri na Marekani. Kuhusu uhusiano kati ya nchi za Ghuba na Marekani, waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Qatar Bw. Jassem al-Thani kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema,
"Nchi zote wanachama wa Kamati ya Ushirikiano wa Nchi za Ghuba zina uhusiano mzuri na Marekani. Lakini uhusiano huu mzuri hauna maana ya kutuzuia kuendeleza uhusiano na Iran. Iran ni nchi jirani yetu, itakuwa ni manufaa kwa kanda ya Ghuba kama tukiweza kuendeleza uhusiano na Iran na kuufanya uhusiano huo uwe tulivu. Kwa hiyo tunaona kuwa uhusiano na nchi fulani haufai kujengwa kwa kuondoa uhusiano na nchi nyingine."
Kwenye mkutano huo nchi za Ghuba zilifuatilia sana hali ya siasa ya kimataifa na uchumi wa China unaokua haraka. Katibu mkuu wa Kamati hiyo Bw. Abdul Rahman al-Attiya alisema, Kamati yake itafanya mazungumzo na China kuhusu kuanzisha soko huria na kusisitiza kwamba suala hilo ni muhimu sana. Alisema,
"Kuanzisha soko huria na China ni manufaa kwa pande zote mbili, hivi sasa mazungumzo kuhusu suala hilo yamepata mafanikio makubwa na yataendelea mwishoni mwa mwaka huu."
Mkutano huo pia umefikia maoni ya pamoja kuhusu masuala ya kimataifa na ya kikanda. Rais wa Qatar Bw. Khalifa al-Thani alisema,
"Mkutano huu uliofanyika kwa mafaniko unatokana na juhudi za kila nchi mwanachama, mkutano huu utafanya uhusiano kati ya nchi za Ghuba uzidi ku9marika, na uhusiano wa karibu zaidi na wenye utulivu zaidi."
Idhaa ya kiswahili 2007-12-05
|