Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-05 19:58:25    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na maharagwe

cri

Mahitaji

Maharagwe gramu 350, nyama ya ng'ombe gramu 150, chumvi gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 8, sukari gramu 5, pilipili hoho gramu 5, vipande vya vitunguu maji gramu 3, mchuzi wa sosi gramu 3.

Njia

1. kata nyama iwe vipande, koroga nyama pamoja na wanga.

2. washa moto, mimina maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia maharagwe kwenye maji, korogakoroga, yapakue. Tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya nyama kwenye sufuria, korogakoroga vipakue.

3. washa moto tena, tia pilipili hoho korogakoroga, halafu tia maharagwe korogakoroga, halafu tia vipande vya nyama, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mchuzi wa sosi, korogakoroga, tia sukari korogakoroga, halafu mimina maji ya wanga korogakoroga, ipakue, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.