Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-06 16:10:46    
Mwalimu mwanamke Ukraine aliyefanya kazi nchini China kwa miaka 16

cri

Bibi Kovaliova amefundisha lugha ya kirussia nchini China kwa miaka 16, na alipata tuzo ya urafiki ya China kwa wataalamu kutoka nchi za nje ambayo ni tuzo kubwa zaidi ya serikali ya China kwa wataalamu kutoka nchi za nje.

Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, Bibi Kovaliova aliyekuwa na umri wa miaka 43 akiwa mtaalamu na mwalimu wa lugha ya kirussia alitumwa na wizara ya elimu ya juu ya Urusi ya zamani kwenye shule moja mjini Xi'an nchini China.

Kama ilivyo kwa wageni wengine wanaokuja nchini China, Mwanzoni Bibi Kovaliova alipata matatizo mengi kama vile kutofahamu lugha ya kichina na kutozoea vyakula vya kichina. Alikumbusha, akisema,

"Sikuweza kutumia vijiti, ilikuwa vigumu sana kwangu, pia sikuweza kuzoea vyakula vya kichina. Sikuweza kuongea kwa kichina, mambo hayo yalikuwa ni matatizo makubwa kwangu kuwasiliana na watu wa China. Kwa bahati nzuri, marafiki zangu walinisaidia sana kwa moyo wa dhati."

Kabla ya kuzoea lugha ya kichina na vyakula vya kichina, Bibi Kovaliova alipata tatizo kubwa zaidi. Mwishoni mwa mwaka 1991, Urusi ya zamani iliposambaratika, akiwa mtaalamu aliyetumwa na Urusi kuja China, Bibi Kovaliova alikumbwa na hali ngumu. Wakati huo, alikuwa analipwa mshahara na serikali ya Urusi ya zamani na serikali ya China, baada ya mwaka 1991 Urusi ilisimamisha kumlipa mshahara. Alikuwa anapaswa kufanya uamuzi wa kuendelea kufanya kazi nchini China au kurudi nchini Ukraine.

Mwishowe aliamua kuendelea kuishi nchini China. Alisema alipaswa kutekeleza mkataba wake.

"Mimi ni mtu mwenye furaha na ninaweza kufanya kila kitu kwa uchangamfu. Ninaona kuwa watu wanapata taabu mbalimbali katika maisha yao, lakini ninaamini kuwa masuala yote yanaweza kutatuliwa. Na jambo muhimu ni kuwa ninapenda kufanya kazi nchini China kwa moyo wa dhati."

Wakati alipokuwa anafundisha mjini Xi'an, Bibi Kovaliova alikutana na profesa wa chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Xi'an Bw. Yu Yang ambaye sasa ni mume wake. Wakati alipokumbwa na matatizo makubwa, Bw. Yu Yang alimsaidia siku zote, na alimsaidia katika maisha yake.

Bibi Kovaliova alisema:

"ninamshukuru sana, kwa sababu wakati nilipokuwa na matatizo, alikuwa ananisaidia siku zote. Msaada huo ni msaada halisi, pia ni msaada wa kiroho. Kama isingekuwa na msaada wake, huenda ningekuwa nimerudi nyumbani."

Kutokana na msaada kutoka kwa mume wake na marafiki zake nchini China, Bibi Kovaliova alizoea maisha nchini China siku baada ya siku. Baada ya muda wake kukaa mjini Xi'an kwa miaka mitatu kwisha, alipata mwaliko kwenda Shanghai na Tianjin kufundisha katika vyuo vikuu. Kuanzia mwaka 2002, alianza kazi ya kufundisha lugha ya kirussia kwenye chuo kikuu cha Xinjiang.

Idhaa ya kiswahili 2007-12-06