Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-07 19:10:10    
Matarajio kuhusu mkutano wa viongozi wa Ulaya na Afrika

cri

Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya na nchi 53 za Afrika utafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 9 huko Lisbon, mji mkuu wa Ureno, nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya. Kufanyika kwa mkutano huo ulioahirishwa mara kadhaa kumeonesha kuwa sera za Umoja wa Ulaya kwa Afrika zimebadilika kuwa busara.

Mkutano kama huo wa kwanza ulifanyika mwezi Aprili mwaka 2004 huko Cairo, na mkutano huo wa pili ulipangwa kufanyika mwaka 2003 mjini Lisbon, lakini kutokana na kuwa nchi za Afrika hazikukubali uamuzi wa Umoja wa Ulaya kumkataa rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kuhudhuria mkutano huo uliahirishwa mara kadhaa mpaka baadaye ulipopoewa msukumo na Ureno, Ufaransa na Hispania. Kwa mujibu wa ratiba, mkutano huo utajadili zaidi mambo ya amani na usalama, wahamiaji, nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, na kupitisha nyaraka za "Mkakati wa pamoja wa Umoja wa Ulaya na Afrika" na "Utekelezaji wa mpango wa mwaka 2008-2010". Vyombo vya habari vimegundua kwamba kulingana na mkutano wa kwanza uliofanyika miaka saba iliyopita, mazingira na maudhui ya mkutano huo yamebadilika kabisa.

Kwanza, mshikamano wa nchi za Afrika katika juhudi za kujiimarisha ni nguvu ya kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo. "Taarifa ya Cairo" iliyotolewa kwenye mkutano wa kwanza ilisisitiza haja ya kuanzisha uhusiano mpya wa kiwenzi, na ilikuwa mwanzo mwema wa kuimarisha uhusiano kati ya Ulaya na Afrika na kuelekea kwenye mazungumzo ya pande zote. Mwaka 2001 nchi za Afrika ziliandaa zenyewe "Mpango mpya wa Ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi ya Afrika", kwa mara ya kwanza zilitoa sauti za kuanzishwa kwa uhusiano wa aina mpya wenye usawa na kunufaishana kati ya Ulaya na Afrika. Mwaka wa pili Umoja wa Afrika (AU) ulitangaza kuanzishwa, hii inaashiria kwamba Afrika imepiga hatua nyingine katika kujiimarisha. Mfano mwingine wa kuimarika kwa ushirikiano wa nchi za Afrika, ni Ureno kumwalika robert Mugabe kuhudhuria kwenye mkutano huo kutokana na shinikizo la nchi za Afrika.

Pili, kutokana na jinsi nchi kubwa zinavyozingatia mambo ya Afrika, nchi za Umoja wa Ulala hazina budi kurekebisha sera kuhusu Afrika na kuboresha uhusiano kati ya Ulaya na Afrika ni matakwa ya lazima. Kwa vyovyote vile, Bara la Afrika ni muhimu sana kwa nchi za Ulaya iwe ni katika athari ya kisiasa au katika maendeleo ya uchumi, ustawi na utulivu wa Afrika unahusiana moja kwa moja na hatma ya Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umetambua kwamba, kutokana na kuinuka kwa hadhi ya Afrika duniani, Umoja wa Ulaya hauwezi kukwepa ushirikiano wa Afrika katika mapambano dhidi ya ugaidi, usalama wa nishati, mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuzuia kuenea kwa magonjwa, na mambo yote hayo hayawezi kutekelezwa, bila kuwa na usawa katika mazungumzo na maingiliano na Afrika.

Mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika Desemba mwaka 2005 ulipitisha mkakati mpya kwa Afrika, mkakati huo unasema Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na ushirikiano na Afrika ili kutimiza amani na utulivu, kuhimiza maendeleo ya biashara na uchumi, kuongeza misaada na kusamehe madeni, na katika miaka 10 ijayo utawekwa uhusiano wa kiwenzi ili kusaidia kutimiza malengo ya milenia barani Afrika.

Vyombo vya habari vimegundua kwamba ingawa nchi zote za Afrika zimealikwa kushiriki kwenye mkutano, lakini mpaka sasa waziri mkuu wa Uingereza Bw Gordon Brown bado anashikilia msimamo wa kutohudhuria mkutano huo, kama Bw Mugabe atahudhuria. Vyombo vya habari vinaona kuwa mkutano huo ni fursa nzuri ya kuweka mwelekeo wa uhusiano kati ya Ulaya na Afrika, na pande zote mbili zina matumaini makubwa juu ya mkutano huo, lakini maneno matupu haujengi, bali kwa vitendo.