Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-10 19:14:30    
Jumba la makumbusho ya mapinduzi kwenye mlima Jinggang

cri

   

Mlima Jinggang ulioko kwenye mkoa wa Jiangxi, sehemu ya kati ya China, ni mlima mkubwa wenye misitu minene. Zaidi ya miaka 80 iliyopita, wakomunisti wa China walijenga kituo cha kwanza cha mapinduzi kwenye sehemu ya vijiji, ambacho kinasifiwa kuwa ni sehemu yalipoanzia mapinduzi nchini China. Hivi karibuni, ujenzi wa jumba la makumbusho ya mapinduzi kwenye mlima Jinggang ulioko kwenye tarafa ya Ciping, ambalo ni jengo la alama ya historia ya mapinduzi ya sehemu ya mlima Jinggang ulikamilika. Tangu jumba hilo la makumbusho lifunguliwe tarehe 27 mwezi Oktoba, watalii wengi walikwenda kutembelea huko, ambapo maonesho yenye wazo jipya yaliwafanya watazamaji wajione kama wao wenyewe walikuwa katika miaka ile.

Jumba la makumbusho ya mapinduzi ya mlima Jinggang ni jengo lenye eneo la mita za mraba zaidi ya elfu 20, kumbi zake 6 zinaonesha mabaki ya vitu zaidi ya 800, picha zaidi ya 2,000 pamoja na vitu vingine vya kihistoria. Umbo la jumba hilo la makumbusho ni kama la herufi ya U, paa la jengo hilo ni la rangi nyekundu, sehemu ya mbele ya jengo la makumbusho kuna nguzo 6 kubwa, na jengo zima la makumbusho ni jengo kubwa sana.

Mara tu baada ya kuingia kwenye ukumbi wa Jumba la makumbusho, watazamaji wanaweza kuona sanamu ya taa ya kibatari kilichoko mbele ya mlima Jinggang, tofauti na majumba mengine ya makumbusho ya nchini China, ambayo yanaweka sanamu za watu. Mkuu wa shirika la gazeti la picha la Jiangxi, Bw. Guo Jiasheng alisema,

"Wazo letu kuhusu sanamu hii ni kuonesha mambo ya jana, leo, rangi nyekundu na rangi ya kijani. Hili ni wazo jipya na kubwa. Kuhusu jana, tunaona kibatari hiki ambacho kiliangaza njia ya mapinduzi hadi kwenye ushindi, ilitumiwa na mwanzilishi wa mapinduzi ya China, Mao Zedong wakati alipokuwa anaandika makala kwenye jengo lenye pembe nane."

   

Ndani ya jengo hilo la makumbusho, yamewekwa mazingira mengi makubwa ya maonesho yanayotumia zana za teknolojia ya kisasa ya sauti, mwanga hata radi kwa njia ya umeme, yakionesha matukio ya kihistoria yakiwemo ya "uasi wa Nanchang wa tarehe mosi mwezi Agosti", "kukutana kwa majeshi kwenye mlima Jinggang" na "safari ndefu ya jeshi jekundu". Katika mazingira hayo, mbinu za kiteknolojia za sauti, mwanga hata radi kwa njia ya umeme, pamoja na michoro na sanamu zilizowekwa humo, zinawafanya watazamaji kama wao wenyewe wawe katika hali halisi ya miaka ile. Watazamaji wengi walipoyaona hayo, waliyasifu mara kwa mara. Ili kukidhi matakwa ya watazamaji vijana, picha za katuni za FLASH zilitumika katika maonesho hayo, ambazo zinaongeza shauku ya vijana kuhusu historia ya jeshi jekundu la China ya miaka ile.

Sauti mnayoisikia ni wimbo ulioko kwenye picha za katuni za FLASH kuhusu nidhamu tatu zilizowekwa kwa jeshi jekundu. Kutumia picha za katuni za FLASH katika jumba la makumbusho ya historia siyo mbinu inayotumika katika majumba mengine ya makumbusho nchini China. Kutokana na picha hizo za katuni za FLASH, watazamaji hususan wanafunzi wa shule za msingi, wanaweza kufahamu mara moja mambo yaliyomo kuhusu nidhamu tatu za jeshi jekundu la China, ikiwemo ya kutochukua sindano na uzi wa umma. Je, mbona inachukuliwa kuwa ni mbinu ya picha za katuni za FLASH? Kuhusu swala hilo, kiongozi wa ujenzi wa jumba la makumbusho ya mapinduzi la mlima Jinggang, Bw. Ouyang Sujin alisema,

"Hii inatumika kwa mara ya kwanza nchini China, mwanzoni tulikuwa na wasiwasi kama watazamaji wataipenda. Ukweli umeonesha kuwa kuwaelimisha watoto kwa mtindo wanaopenda kutapata ufanisi mzuri zaidi."

   

Ingawa mlima Jinggang hivi sasa uko katika kipindi kisichokuwa na watalii wengi, lakini baada ya kuzinduliwa kwa jumba hilo la makumbusho, watazamaji wanafikia elfu kadhaa kwa siku, hususan katika siku mbili za tarehe 27 na 28 mwezi Oktoba baada ya kuzinduliwa kwa maonesho hayo, idadi ya watazamaji ilikuwa karibu 2000. Walionesha shauku kubwa kuhusu maonesho hayo yenye wazo la uvumbuzi. Bw. He Hailiang kutoka mji wa Changsha, mkoani Hunan, alisema maonesho hayo yamemwelimisha, ameona moyo wa kuchapa kazi na bila kuogopa taabu.

"Ninaona, baada ya kuelimishwa na maonesho, nitapiga hatua katika kuboresha tabia yangu, na pia itahimiza moyo wetu wa kufanya ushirikiano na kupigania mafanikio makubwa zaidi."