Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-12 15:11:45    
Mji wa Enshi mkoani Hubei waeneza teknolojia ya matumizi ya gesi ya kinyesi

cri

Gesi ya kinyesi ni gesi inayopatikana baada ya kuchachishwa kwa kinyesi, majani na na vitu vingine vilivyooza, gesi hiyo inaitwa methane kitaaluma. Sehemu inayojiendesha ya makabila ya waTu na waMiao ya mji wa Enshi iliyoko kusini magharibi mwa mkoa wa Hubei, ni eneo muhimu la hifadhi ya misitu nchini China. Tokea mwaka 2000, sehemu hiyo imeeneza teknolojia ya matumizi ya gesi ya kinyesi kote vijijini.

Katika kijiji cha Xiaba kwenye sehemu hiyo, kila familia ina shimo la gesi ya kinyesi, kwa kawaida shimo hilo lina kina cha mita mbili na ukubwa wake unategemea idadi ya watu kwenye familia, kwa wastani kila mtu anahesabiwa kuwa na mita mbili ya ujazo. Kwa mfano familia yenye watu watano itajenga shimo la mita 10 ya ujazo ambalo linaunganishwa na choo na mazizi ya mifugo. kwa kawaida gesi ya kinyesi inayozalishwa itakidhi mahitaji ya kupikia, kutoa mwagaza na kuongeza joto nyumbani kwa mwaka mzima. Mwanakijiji Bi. Chen Yanqun alisema, hivi sasa baada ya kumaliza kazi za mashambani naweza kupika chakula tu nikiwasha gesi ya kinyesi. Lakini zamani itachukua saa moja kupika chakula. Hivi sasa natumia nusu saa kutayarisha chakula. Bi. Chen alisema:

"gesi inayozalishwa kutokana na kinyesi cha nguruwe watatu au wanne itakidhi mahitaji ya familia yetu. Zamani tulikuwa tunatumia kuni kupika chakula, si kama tu tulitakiwa kufanya kazi ngumu, bali pia kuni si nishati safi. Gesi ya kinyesi kweli inawakomboa wanawake vijijini."

Matumizi ya kuni si kama tu yanaleta uchafuzi kwa mazingira, bali pia huleta madhara kwa afya za wakulima. aidha, kila mwaka miti yenye mita za ujazo ziadi ya milioni moja inawaka kutengenezea nishati.

Kuhusu hali hiyo, serikali ya sehemu hiyo ya Enshi iliweka mpango wa kujenga mashimo laki 7 ya kuzalisha gesi ya kinyesi, na kutoa ruzuku yuan 500 hadi 1000 kwa familia zilizojenga mashimo hayo. Sera hiyo imefanya idadi ya mashimo iongezeke na kuwa laki moja kila mwaka. Imefahamika kuwa, hivi sasa mpango huo umeshamalizika kwa kiwango cha nusu.

Matumizi ya gesi ya kinyesi yameboresha maisha ya wakazi wa huko. Mwanafunzi wa shule ya msingi ya kijiji cha Jiugenshu cha mji huo Qi Duanchao anasoma katika darasa la sita, kutokana na kuwa nyumba yake kuwa mbali na shule, yeye anaishi kwenye bweni la shule, na anarudi nyumbani kila baada ya wiki moja au mbili. Katika shule hiyo kuna wanafunzi wengi wanaoishi shuleni kama ilivyo kwa Qi Duanchao. Kabla shule hiyo haijajenga shimo la kuzalisha gesi ya kinyesi, kuoga kwa maji ya moto ni ndoto kwa wanafunzi hao. Lakini kutokana na mradi wa matumizi ya gesi ya kinyesi katika shule ye msingi na ya sekondari iliyoanzishwa mwaka 2006 kwenye sehemu hiyo, shule ya Jiu Genshu imekuwa moja ya shule zilizonufaika na matumizi mapema. Kuanzia mwaka jana, Qi Duanchao alikuwa anaweza kuoga kwa kutumia maji ya moto kwenye chumba cha kuogea shuleni. Alisema:

"naoga mara mbili au tatu kila wiki, kila alasiri baada ya kucheza na wanafunzi wenzangu au kupiga mpira, jasho hututoka, tunaenda kuoga kwenye bafu linalotumia gesi ya kinyesi. Naona matumizi ya gesi ya kinyesi yametuletea urahisi katika maisha."

Ofisa wa kijiji hicho Bw. Zou Anping Anping alisema, kutokana na ujenzi wa mashimo hayo, uchafuzi ovyo mitaani umekwisha, hivi sasa mitaa na kila nyumba zote ziko katika hali ya usafi. Matumizi ya gesi ya kinyesi si kama tu yameboresha mazingira, bali pia yanasaidia kuhifadhi misitu. Bw. Zou Anping alisema:

"kwa fano kijiji chatu kina mashimo 980, kila shimo linapunguza ukataji wa miti la hekta 0.3, kwa ujumla mashimo hayo yanahifadhi misitu yenye eneo la hekta 330."

Imefahamika kuwa hivi sasa matumizi ya gesi ya kinyesi yaliyoenezwa kwenye sehemu nzima ya Enshi yanaweza kupunguza ukataji wa misiti kwa hekta laki moja kila mwaka. Kwa hivyo hivi sasa misitu inafunika asilimia 67 ya eneo la sehemu hiyo, hali ya mzingira ya kiikolojia imeboreka kidhahiri. Aidha, manufaa ya kiuchumi ya moja kwa moja yaliyoletwa na matumizi ya gesi ya kinyesi yamezidi yuan milioni 150, matumizi ya jumla ya mabaki ya kinyesi kilichooza pia yanapunguza matumizi ya mbolea na dawa za kilimo. Mwanakijiji cha kijiji cha Denglongba Bw. Xiao Hongjun alisema, mabaki ya kinyesi ni mbolea mzuri, na yanaweza kutumika moja kwa moja mashambani, si kama tu yanaweza kuzuia wadudu kwa ufanisi, bali pia yanaweza kuinua sifa ya mazao. Hivi sasa shamba la chai la Bw. Xiao Hongjun linaleta pato la yuan elfu 7 kwa mwaka, likiwa limeongezeka kwa yuan zaidi ya elfu 2 kuliko lile la zamani.