Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-12 15:32:57    
Mapishi ya supu ya mwani na nyama ya mbavu za nguruwe

cri

Mahitaji

Nyama ya mbavu za nguruwe gramu 200, mwani gramu 50, vipande vya tangawizi gramu 5, chumvi vijiko viwili, mvinyo wa kupikira kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja

Njia

1. osha mwani , halafu weka kwenye sufuria yenye maji, chemsha kwa mvuke kwa nusu saa, halafu osha tena, na weka kwenye maji kwa saa nne halafu uikate iwe vipande.

2. mimina maji kwenye sufuria, tia mbavu za nyama ya nguruwe, vipande vya tangawizi, vitunguu maji, mvinyo wa kupikia, chemsha kwa dakika 20, halafu punguza moto, tia vipande vya mwani, endelea kuchemsha kwa nusu saa, ondoa vipande vya tangawizi, vitunguu maji, tia chumvi, mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga. Ipakue. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.