Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-13 18:46:44    
Mwalimu mwanamke wa Ukraine aliyefanya kazi nchini China kwa miaka 16

cri

Katika kipindi kilichopita tuliwaletea maelezo kuhusu maisha ya Bibi Aleksandra Kovaliova kabla hajaanza kufanya kazi ya kufundisha lugha ya kirussia kwenye chuo kikuu cha Xinjiang. Leo tunaendelea kuwafahamisha kuhusu maisha yake katika chuo hicho.

Bibi Kovaliova anafuatilia sana kuwawezesha wanafunzi kuongeza nia ya kujifunza lugha ya Kirussia. Kila mwaka, chuo hicho kinaandaa tafrija ya mwaka mpya ya michezo ya kuigiza kwa lugha za kigeni. Bibi Kovaliova aliwaambia wanafunzi wake waandae mchezo wa kuigiza wao wenyewe, hata kuwahimiza kutunga mchezo huo. Katika tafrija ya mwaka jana, wanafunzi wake ambao walijifunza lugha ya kirussia kwa muda wa nusu mwaka, walipata tuzo ya nafasi ya pili ya kucheza mchezo wa kuigiza.

Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa wa Xinjiang ulifanya mawasiliano mengi na Russia na nchi mbalimbali za Asia ya kati, watu wengi wanapenda kujifunza lugha ya kirussia. Lakini mkoani Xinjiang kuna upungufu mkubwa wa walimu wa lugha ya kirussia na viwango vya ufundishaji kwa walimu wa lugha ya kirussia ni tofauti. Njia ya anayotumia mwalimu Kovaliova kufundisha inafanya kazi kubwa katika kuinua kiwango cha ufundishaji wa lugha ya kirussia mkoani Xinjiang na kuwaandaa walimu hodari wengi zaidi wa lugha ya kirussia nchini China.

Ofisa anayeshughulikia mambo ya mafunzo ya chuo kikuu cha Xinjiang Bibi Manze alisema,

"Yeye ametusaidia sana. Kwa upande mmoja anafundisha wanafunzi wa chuo hicho. Kwa upande mwingine anawaandaa walimu vijana, kufanya mawasiliano nao na kuwasaidia kuinua kiwango chao cha ufundishaji."

Bibi. Bi Xinghui ni mwalimu kijana wa chuo kikuu cha Xinjiang. Kutokana na msaada wa Bibi Kovaliova, yeye amekuwa mmoja kati ya watu walio uti wa mgongo katika kufundisha lugha ya kirussia. Anamshukuru sana, alisema,

"sisi walimu vijana tulipomwuliza maswali, kila mara alitujibu kwa uchangamfu, hata tulimpigia simu wakati wa usiku, tukajadiliana naye kuhusu suala moja kwa saa moja hadi saa mbili kwenye simu, lakini alitujibu bila kujali uchovu. Walimu wote wanamsifu mwalimu huyo mzee kwa kuchapa kazi."

Wakati alipofanya kazi katika chuo kikuu cha Xinjiang, alishiriki kwenye kazi ya kutunga na kupitisha vitabu vya lugha ya kirussia, na kufanya juhudi kwa ajili ya kuinua kiwango cha ufundishaji wa lugha ya kirussia nchini China. Mwaka 2003, serikali ya Xinjiang ilimpa tuzo ya "Tianshan" ili kumsifu kwa mchango mkubwa alioutoa katika ufundishaji wa lugha ya kirussia nchini China. Mwaka jana, Bibi Kovaliova pia alipata tuzo ya urafiki ambayo inatolewa na serikali ya China kwa wataalamu wa nchi za nje waliofanya kazi nchini China. Yeye ni mtaalamu pekee wa nchi za nje aliyepata tuzo hii katika mambo ya elimu ya mkoa wa Xinjiang. Alipokumbusha safari yake ya kuja mjini Beijing kuppokea tuzo hiyo, alisema,

"nilifurahi sana nilipojua nimepata tuzo hii. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alitushukuru kwa kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya China. Niliongea naye sana na kupiga picha naye picha hii ninaitunza sana."

Katika miaka 16 aliyokaa nchini China, ameshuhudia mabadiliko makubwa ya jamii ya China, na anaipenda China. Alisema,

"Nimekwenda kwenye miji mingi nchini China, ninaipenda sana China. Mambo yanayonivutia ni uchumi wenye maendeleo ya kasi. Sehemu nyingi zinaendelezwa kwa kasi na ujenzi unafanyika huku na huko. Sura ya mji wa Wurumuqi na chuo chetu pia imebadilika kuwa mpya."

Bibi Kovaliova alisema ingawa anarudi Ukraine kukutana na jamaa zake wakati wa likizo ya majira ya joto, lakini hafikiri kuacha kazi yake. Yeye anaona kuwa kuwaandaa watu wenye ujuzi wa lugha ya kirussia kuna manufaa kwa China na Ukraine.