Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-13 19:36:47    
Baada ya Mkutano wa Annapolis, sehemu ya mashariki ya kati inakaribia na amani?

cri

Katika mwaka 2007, kwenye sehemu ya mashariki ya kati, mbali na mapambano kati ya Israel na Palestina, migongano mikali kati ya makundi ya Palestina imeleta utatanishi zaidi kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina. Na Mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya mashariki ya kati uliofanyika tarehe 27 Novemba, mwaka 2007 huko Annapolis, Marekani umeleta matumaini kwa watu wanaotarajia amani na usalama. Lakini wasiwasi walio nao watu bado haujaondolewa.

Kwenye Mkutano huo, rais George Bush wa Marekani alitangaza kuwa Palestina na Israel zitaanzisha tena mazungumzo ya amani, na zitafanya juhudi zote kadiri ziwezavyo kufikia makubaliano ya amani kuhusu masuala makubwa ya mamlaka ya Jerusalem, kurudi kwa wakimbizi, kugawa mipaka, na mustakabali wa makazi.

Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw Mahmoud Abbas walieleza matumaini yao ya kuhimiza mazungumzo ya amani. Bw. Olmert alisema:

"Mazungumzo hayo yatahusiana na masuala yote yaliyoepukwa na pande mbili, lakini tutajadiliana kwa uwazi, moja kwa moja na kwa ushupavu. Hatutaweza kukwepa masuala yoyote kwa makusudi".

Bw. Abbas alieleza imani yake akisema:

"Wakati wa kukomesha mzunguko mbaya wa umwagaji damu, mabavu na ukaliaji umewadia. Palestina na Israel zinapaswa kuwa na imani na matumaini ili kukabiliana na hali ya siku za usoni. Sehemu ziliko Palestina na Israel zimewahi kusifiwa kuwa ni sehemu ya upendo na amani, hivyo sehemu iliyokithiri kwa vurugu za vita isingekuwa jina la sehemu hiyo".

Mbali na hayo, pande hizo mbili ziliamua kuanzisha kamati ya uelekezaji itakayowajibika kutunga mpango wa mazungumzo na kusimamia mchakato wa mazungumzo; kudumisha utaratibu wa Mkutano kati ya wakuu wa pande hizo mbili kila baada ya muda fulani, ili kutatua masuala husika kwenye mazungumzo hayo.

Mkutano wa Annapolis umeonesha misimamo ya pande mbalimbali kuhusu mchakato wa amani, Mkutano huo kweli umeweka mwanzo mzuri kwa ajili ya kuanzisha tena mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel. Lakini hali halisi ya miongo kadhaa iliyopita imeonesha kuwa, njia ya amani ya Palestina na Israel hakika itakuwa na vipengele. Ofisa wa Taasisi ya REUT ambayo ni Jumuiya ya washauri mabingwa ya Israel Bw. Gidi Grinstein, ambaye alikuwa katibu wa kikundi cha Israel pia ni msuluhishi katika mazungumzo kati ya Israel na Palestina ya mwaka 1999 hadi 2001 alisema, mazungumzo yanayohusu masuala makubwa yakianza, matatizo na migongano mbalimbali hakika itaonekana wazi. Alisema:

"Wamarekani wanadhani wamepata mbinu mzuri, hivyo wanaweza kukwepa kanuni za kimsingi ili kuzihimiza Palestina na Israel zianzishe kikundi cha kazi na kuzihimiza zianzishe mazungumzo. Lakini kama kufuata njia hiyo, tutakuta matatizo mengi. Kwa Israel, taabu zitatokana na mfumo wa kisiasa, kwani serikali ya Israel iliundwa upya mara kwa mara, madaraka ya kisheria na kiutawala yamesambaa kwenye idara nyingi kupita kiasi, tena tutakuta migongano mikubwa kuhusu namna ya kutatua suala la Palestina. Tunaweza kusema kuwa, kisiasa Israel ikichukua hatua yoyote ya kurudi nyuma itamaanisha kuleta msukosuko wa kisiasa nchini Israel, na Palestina iliyoko katika hali ya mfarakano kwa hivi sasa hakika itakabiliwa na taabu zake".

Wakati wa Mkutano wa Annapolis, makundi yenye siasa kali ya Hamas na Jihad yalifanya maandamano makubwa huko Gaza na sehemu ya magharibi ya Mto Jordan, yakipinga kuitishwa kwa Mkutano huo. Hii imeonesha hali dhaifu ya Bw. Abbas na serikali ya mpito ya Palestina iliyoanzishwa kwenye sehemu ya magharibi ya Mto Jordan baada ya kundi la Hamas kudhibiti ukanda wa Gaza mwezi Juni mwaka huu.

Profesa wa Chuo kikuu cha Birzeit cha Palestina Bw. Ghassan al Khati ambaye alikuwa mjumbe wa kikundi cha upande wa Palestina kwenye mazungumzo kati ya Palestina na Israel ya mwaka 1991 hadi 1993, alisema katika hali dhaifu kupita kiasi waliyonayo viongozi wa pande hizo mbili, matumaini ya kufikia makubaliano ya amani ni madogo sana.