Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-14 17:25:37    
Ukungu uliotanda suala la nyuklia la Iran waanza kupungua

cri

Tarehe 24 mwezi Machi mwaka huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio jipya la kuiwekea Iran vikwazo dhidi ya mradi wa kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran haikutishika badala yake inaendelea na mpango wake wa nyuklia. Tunapokumbuka hali ya mwaka 2007 mvutano kuhusu suala la nyuklia la Iran ulikuwa mkali, na ukungu kuhusu suala hilo ulikuwa mzito mpaka mwishoni mwa mwaka huu ambapo idara za upelelezi za Marekani kutangaza "tathmini kuhusu habari za upelelezi", ukungu umeanza kupungua na watu wameanza kuona mwangaza wa jua. Ingawa mwaka 2008 mvutano kuhusu suala la nyuklia la Iran utaendelea, lakini mvutano huo utainufaisha zaidi Iran. Tarehe 9 Aprili mwaka huu rais wa Iran alisema,

"Iran imekuwa na uwezo wa kuzalisha nishati ya nyuklia kwa viwanda, na imeingia kwenye nchi zenye teknolojia ya nyuklia. Kwa mujibu wa mpango, Iran itazalisha umeme megawati elfu 20 kwa ajili ya matumizi ya matibabu, kilimo na viwanda."

Tarehe 28 Agosti mwaka huu kwa mara nyingine tena rais wa Iran alitangaza kuwa Iran imekuwa "nchi ya nyuklia" na itaendelea kutekeleza mpango wake wa nyuklia kwa ajili ya matumizi ya amanai.

Ni bahati nzuri kwamba jumuyia ya kimataifa inaonekana kuwa na utulivu na kutumia busara. Katibu mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohamed El Baradei mara kadhaa alisisitiza kuwa, kufanya mazungumzo ni njia nzuri ya utatuzi wa suala la nyuklia la Iran. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi pia aliwahi kusisitiza kuwa suala la nyuklia la Iran linatakiwa kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia. Waziri wa mambo ya nje wa Russia alisema,

"Tunaamini kuwa katika jamii ya leo duniani, mabavu hayasaidii chochote katika utatuzi wa matatizo, hali kadhalika kwa suala la nyuklia la Iran."

Ingawa Iran inakabili vikwazo kwa msimamo mkali, lakini haijafunga mlango wa kukataa kufanya mazungumzo. Tarehe 9 Aprili rais wa Iran alisema,

"Iran siku zote inataka ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, na inakubali shirika hilo kutuma watu kufanya ukaguzi nchini humo, mradi wa nyuklia wa Iran ni wazi, na mpaka sasa haiko nje ya eneo la matumizi ya amani."

Tarehe 23 Juni mwaka huu Bw. Baradei alipozungumza na mjumbe wa kwanza wa mazugumzo Bw. Ali Larijani alisema,

"Kwa niaba ya serikali ya Iran Bw. Ali Larijani amesema Iran inataka kutatua suala hilo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na kujadiliana kuhusu masuala muhimu."

Hata hivyo Marekani inaendelea kushikilia msimamo ule ule wa zamani ikijaribu kushirikisha nchi nyingine kuongeza nguvu ya kuiwekea vikwazo Iran. Lakini cha ajabu ni kwamba tarehe 3 Desemba idara ya upelelezi ya Marekani ilitoa taarifa ikisema Iran ilisimamisha mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia mapema mwaka 2003.

Mtaalamu wa masuala ya usalama wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Arizona Bw. Yoav Gortzak alisema,

"Taarifa ni msaada mkubwa kwa Iran, kwa sababu hata idara ya upeleleza ya Marekani haiamini kama Iran ina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia sembuse kuzishawishi nchi nyingine kushiriki kwenye vitendo vya kuiwekea vikwazo Iran."

Lakini rais George Bush wa Marekani anaonekana mkaidi, alisema Marekani haitabadilisha sera zake dhidi ya Iran. Alisema,

"Iran inapaswa kuchagua moja kati ya mambo ya mawili, ama ieleze kila kitu kuhusu shughuli zake za nyuklia, au iendelee kutengwa na jumuyia ya kimataifa."

Balozi wa China nchini Iran Bw. Hua Liming alisema,

"Katika mwaka 2008 uwezekano wa Marekani kutumia mabavu dhidi ya Iran utakuwa mdogo, na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki litakuwa na ushirikiano mkubwa zaidi na Iran ili kuufanya mpango wa Iran uwe wazi zaidi."

Idhaa ya kiswahili 2007-12-14