Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-17 16:48:45    
Shamba la mapumziko la Ziwa Taihu la mji wa Suzhou

cri

Shamba hilo la mapumziko lenye eneo la hekta 30, liko kwenye mlima wa magharibi wa mji wa suzhou, ni shamba lenye uwezo mbalimbali, ikiwemo uzalishaji wa mazao ya kilimo, kuishi na utalii. Kwenye shamba hilo, kuna maeneo ya miti ya matunda, mifugo na mabanda ya joto ya kioo ya kuotesha mimea katika majira ya baridi: kwenye sehemu ya uzalishaji mitunda yenye urefu wa zaidi ya mita 300, imepandwa mimea ya matikiti ya aina zaidi ya 40 za Taiwan; kwenye sehemu ya ufugaji, licha ya kuweko sungura, kuku, mbuzi, pia kuna wanyama adimu elk na yak; ndani ya mabanda ya joto imepandwa mimea ya matango na nyanya inayotumia mbolea ya samadi tu. Bw. Cai Shengjia alisema kwa fahari kuwa, maji yanayotumiwa kumwagilia mboga na mitunda ni mvua iliyokusanywa na zana maalumu na kuchujwa, hivyo mboga zinazozalishwa hapo zina ladha ya kipekee.

"Ninachukua mfano wa matanga madogo, matango madogo yanayouzwa masokoni ni yenye vitu vya uchafuzi vya dawa za kilimo na vitu vya kikemikali, lakini matango yetu hayana vitu hivyo, tena yana maji mengi ndani yake. Nimesema mengi juu yake, ukila utaona tofauti yake."

Kutokana na uzoefu uliopatikana, mboga na matunda mengi ya Taiwan yanaota vizuri huko Taiwan, lakini hayaoti vizuri kwenye sehemu ya China bara, lakini hilo sio tatizo kubwa kwa Bw. Cai mwenye uzoefu mwingi.

"Mengi ya mazao ya kilimo ya Taiwan yalihamishiwa China bara miaka mingi iliyopita, tunayafanya yazoee mazingira ya hapa kwa kutumia uzoefu na teknolojia yetu, nimewafahamisha wenye mashamba wengi. Sasa tumekuwa na uzoefu mpya kuhusu suala hilo, ambao unayafanya mazao ya Taiwan yazoee haraka mazingira ya hapa."

Suala linalofuatiliwa na wakazi wa kawaida kuhusu mboga na matunda yanayotoka mbali Taiwan ni bei zake, Bw. Cai alisema, kwa kuwa gharama ya uzalishaji wake ni kubwa, hivyo bei ya mboga hizo zinazotoka kwenye mashamba ya kilimo kwa kawaida ni kubwa mara 3 au 4 hivi kuliko zile za mboga za kawaida, hivyo mboga na matunda hayo yanauzwa kwenye mahoteli au supamaketi za kiwango cha juu.

Bw. Cai alisema, shamba la mapumziko la kisiwani Taiwan limekosa nafasi mpya ya maendeleo, lakini sekta husika katika China bara ziko katika hatua ya mwanzo kabisa, hivyo kuna nafasi kubwa za kimasoko. Sehemu ya delta ya mto Changjiang ina uwezo mkubwa wa ununuzi, na inafaa sana kwa maendeleo ya shamba la mapumziko. Shamba la Ziwa Taihu ambalo mazao yake hayana uchafuzi, ni shamba la kwanza la aina hiyo katika mji wa Suzhou, lilipoanzishwa mwanzoni kulikuwa na shida na matatizo. Bw Cai alisema,

"Shughuli za mashamba ya utalii na shughuli za mapumziko kama kwenye shamba letu ni kidogo sana. Gharama ya uzalishaji na faida ya uwekezaji wa kilimo ni ndogo sana, hivyo hakuna mtu kati ya wafanyabiashara wa Taiwan waliofika China bara miaka mingi iliyopita, wanaofanya shughuli hizo kutokana na faida yake kuwa ndogo; tena sekta hiyo inahusiana na pande nyingi, ukitaka kuanzisha mkahawa kama huo wetu, unatakiwa kupata leseni za aina mbalimbali, katika upande huo kuna kanuni nyingi za kisheria zikiwa ni pamoja na ukaguzi wa usafi wa chakula na wazimamoto. Viwanda vya wafanyabiashara wa nchi za nje na wa Taiwan havina uzoefu kama huo. Tunatarajia kuwa kwa kuwa wamefika hapa, basi waendeshe shughuli zao kwa kufuata kanuni na sheria, ni dhahiri kuwa wanatakiwa kupitia mchakato mrefu wa kisheria, utaratibu na kupata idhini wa serikali, hiyo ndiyo shida kubwa inayotukumba."

Teknolojia ya kilimo ya Taiwan ni ya kisasa zaidi kuliko ya China bara, na hiyo pia ni moja ya sababu ya kupenda kuwekeza katika sekta ya kilimo na utalii kwa wafanyabiashara wa Taiwan. Naibu mkurugenzi wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la mji wa Suzhou, Bw. Wu Wenyuan alieleza jinsi wafanyabiashara wa Taiwan wameleta wazo la kisasa kuhusu shamba ambalo pia linatoa huduma za mapumziko kwa watalii, tena wameleta uzoefu wa kisasa wa usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kilimo, akisema:

"Kujengwa na kuendeshwa kwake kutahimiza na kufanikisha mabadiliko ya kilimo kwenye kisiwa cha mlima wa magharibi na sehemu yote ya ziwa Tai ya Suzhou, kuleta maendeleo ya kasi na kuwa mfano muhimu wa kuigwa katika kuunganisha kilimo cha kisasa na sekta ya huduma ya utalii; Kwa upande mwingine, mafanikio ya shamba ambalo pia linatoa huduma za mapumziko kwa watalii yataleta nafasi na mfano wa kuigwa kwa ushirikiano na maendeleo ya kilimo na sekta za utalii ya kando mbili za mlangobahari wa Taiwan, na yatahimiza ushirikiano wa sekta mbalimbali za uzalishaji mali za kando hizo mbili."

Naibu mwenyekiti wa chama cha Guomintang cha China, Bw. Jiang Bingkun alitembelea maonesho ya elektroniki na upashanaji habari ya Suzhou yaliyofanyika katika mji wa Suzhou, alipoambiwa kuwa shamba ambalo pia linatoa huduma za mapumziko kwa watalii la ziwa Tai la Suzhou limezinduliwa, alikwenda huko kuwapongeza, akisema:-

"Suzhou siyo tu ni mahali pazuri kwa kuwekeza kwa teknolojia ya kisasa, bali pia ni mahali pazuri pa kuwekeza kwa sekta ya utoaji huduma ya utalii. Mji wa Suzhou ni mahali penye wafanyabiashara wengi wa Taiwan kuliko sehemu nyingine nchini, tena umaalumu wake siyo tu kuna sekta nzuri ya elektroniki, bali pia kuna mandhari nzuri na vivutio vingi, pamoja na ardhi kubwa. Kilimo kwa ajili ya shughuli za mapumziko pia kimekuwa njia moja nzuri ya kutatua suala la vijiji la Taiwan katika siku za baadaye. Ninaamini kuwa kundi hilo la watu litatumia uzoefu wa Taiwan, licha ya kutumia vizuri ardhi ya hapa, litahifadhi mazingira ya kimaumbile na kuongeza nafasi za ajira, pia ninatarajia uwekezaji huo licha ya kuhimiza ustawi wa sehemu hiyo, utahimiza amani ya kando mbili za mlangobahari wa Taiwan."

Idhaa ya kiswahili 2007-12-17