Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-19 14:59:36    
Ngoma ya Sarhe ya kabila la Wa-tu

cri
Kwenye vijiji vya kabila hilo wakati wazee wanapofariki dunia, wanavijiji husanyika kucheza ngoma ya Sarhe usiku kucha, na hata kwa siku kadhaa. Inasemekana kuwa chanzo cha ngoma hiyo ni ngoma ya vita na ya sadaka ya wahenga wa kabila la Wa-tu. Naibu mkurugenzi wa kamati ya makabila na dini ya wilaya inayojiendesha ya makabila ya Wa-tu na Wamiao ya Enshi Bw. Tian Fagang ambaye pia ni naibu mkuu wa Shirikisho la Utafiti wa Mila na Desturi za Makabila la wilaya hiyo aliwaelezea waandishi wetu wa habari sababu ya ngoma hiyo kupewa jina la Sarhe, alisema,

"Sarhe ni neno la linalotajwa sana katika ngoma hiyo. Ngoma hiyo huchezwa huku nyimbo zikiimbwa. Kila sentensi kwenye nyimbo hizo inafuatiwa na neno Sarhe, hivyo ngoma hiyo ikaitwa Sarhe."

Sehemu ya asili ya ngoma hiyo ni tarafa ya Yesanguan. Kwenye tarafa hiyo, waandishi wetu walijionea ngoma hiyo maarufu. Baada ya bibi Tian Xiuju aliyekuwa na umri wa miaka 70 kufariki dunia, jamaa wa familia yake waliandaa mahali pa kucheza ngoma ya Sarhe, kisha jamaa wengine kutoka vijiji mbalimbali pia walikuja. Ngoma ngoma ya Sarhe ilichezwa usiku huo na watu wengi.

Mwanamume mmoja wa kabila la Wa-tu alipiga ngoma moja kubwa huku akiimba kwa sauti kubwa, na kwa kufuata midundo ya ngoma aliyopiga, wavulana watatu walicheza ngoma, huku wakiimb pamoja na mpigaji ngoma. Watu wengine walikusanyika kwenye chumba cha mazishi walishiriki kwenye ngoma hiyo, mmoja baada ya mwingine. Bw. Tian Fagang alisema,

"Watu wanapocheza ngoma ya Sarhe, wanaonesha huzuni kubwa kwa marehemu, na hata wanajisahau kama wamefiwa. Hii ndiyo nguvu ya kucheza ngoma hiyo."

Kucheza ngoma ya Sarhe ni njia nzuri ya watu wa kabila la Wa-tu kueleza hisia zao. Nyimbo zinazoandamana na ngoma hiyo zinaimbwa kwa sauti kubwa, na maneno yake yanahusu mambo mbalimbali. Baadhi ni kumbukumbu ya marehemu na kueleza mambo yake, mengine yanawasifu watu wa kale na kueleza matukio ya kihistoria, na mengine yanasimulia hadithi za asili. Aidha midundo ya ngoma hiyo pia ina umaalumu sana. Bw. Tian Fagang alisema,

"Watu wa kabila la Wa-tu wanacheza ngoma hiyo kwa nguvu na kwa mtindo wa kiasili. Kuna mitindo migumu kwenye ngoma ya Sarhe, hata wacheza ngoma maprofesa hawawezi kucheza ngoma hiyo."

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa makabila madogo madogo ya Chuo Kikuu cha Makabila Madogo Madogo cha mkoa wa Hubei Bw. Tian Wanzhen aliyefuatilia ngoma ya Sarhe kwa miaka mingi aliona kuwa mitindo ya ngoma hiyo inahusiana sana na imani ya tambiko la chui mweupe mwenye milia. Alisema,

"Ngoma ya Sarhe ina umaalumu wa imani ya tambiko la chui mweupe mwenye milia, watu wanapocheza ngoma hiyo wanachuchumaa kama chui."

Ngoma ya Sarhe haikusaidia kudumisha imani ya tambiko ya kabila la Wa-tu tu, bali pia imeonesha maoni ya watu wa kabila hilo kuhusu kifo. Watu hao wanaona kuwa watu wanazaliwa na wanakufa, wanawaaga marehemu kwa nyimbo na ngoma zenye furaha. Bw. Tian Fagang aliona kuwa maoni hayo ni sababu inayofanya ngoma ya Sarhe idumu kwa maelfu ya miaka. Alisema,

"Mtu akifariki dunia, jamaa na marafiki zake hata jirani watakusanyika kucheza ngoma ya Sarhe mpaka watakapompeleka kaburini kumpekeka kaburini. Hii ni mila na desturi ya watu wa kabila la Wa-tu. Wanaona kuwa watu watapata maisha mapya baada ya kifo, aidha watu wa kabila la Wa-tu ni hodari katika kuimba nyimbo na kucheza ngoma, hivyo ngoma inachezwa hata kwenye mazishi."

Lakini katika miaka kadhaa iliyopita, ngoma ya Sarhe ambayo ni alama ya utamaduni wa kiasili wa kabila la Wa-tu ilidhoofika kutokana na maingiliano ya utamaduni ya kisasa, na watu wanaojua kucheza ngoma hiyo walikuwa wakipungua mwaka hadi mwaka. Kutokana na kukabiliwa na changamoto ya kutoweka kwa ngoma hiyo, serikali ya sehemu hiyo ilichukua hatua madhubuti ili kuiokoa. Mwaka 2002, serikali ya wilaya ya Enshi iliwatafuta wasanii wa utamaduni wa asili, na kuwateua watu 16 kuwa wasanii wakubwa wa utamaduni wa asili, na kuwapa ruzuku ili kuwasaidia kueneza utamaduni huo.

Chini ya msaada wa serikali, wachezaji ngoma ya Sarhe wanaichukulia kazi ya kurithi na kuendeleza ngoma hiyo kuwa ni wajibu wao. Bw. Huang Zaixiu mwenye umri wa miaka 52 anatoka kwenye tarafa ya Yesanguan ya wilaya ya Enshi, yeye ni mchezaji maarufu zaidi wa ngoma ya Sarhe kwenye sehemu hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa anashiriki kwenye maonesho ya ngoma ya Sarhe mara kwa mara, huku akikusanya nyimbo za ngoma hiyo na kuwafundisha wanafunzi. Mbali na hayo alianzisha kikundi chake cha ngoma ya Sarhe , na kuitambulisha ngoma hiyo sehemu za nje. Bw. Huang Zaixiu ana matumaini makubwa na mustakabali wa ngoma ya Sarhe, alisema,

"Kwenye sehemu za vijijini, vijana wengine wanapenda kucheza ngoma ya Sarhe. Aidha serikali yetu inazingatia sana kuendeleza ngoma hiyo, hivyo sikubali ngoma hiyo ipotee. "

Idhaa ya kiswahili 2007-12-19