Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-19 19:42:06    
Chuo cha Confucius chawaletea wageni urahisi wa kujifunza lugha ya kichina

cri

Hivi karibuni, chuo cha Confucius ambacho ni cha kwanza cha kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa njia ya radio kilianzishwa rasmi katika Radio China Kimataifa, jambo hilo ni habari nzuri kwa marafiki wa nchi za nje wanaopenda utamaduni wa China na wanaotaka kujifunza lugha ya Kichina, kwa kuwa sasa wana njia mpya ya kujifunza lugha ya kichina, yaani kupitia matangazo ya radio.

Wasikilizaji wapendwa, huenda hamuamini kuwa mlikuwa mnamsikiliza msichana mwenye umri wa miaka 9 kutoka Serbia akisoma maandishi ya Confucius. Msichana huyo ana jina zuri la kichina Su Liya, alikuja China miaka mitatu iliyopita pamoja na mama yake anayefanya kazi nchini China. Mama yake Bi. Su Chunyu alisema:

"tulikuja China miaka mitatu iliyopita. Wakati huo hakuweza kuongea kwa kichina hata kidogo, kwa muda wa miezi miwili au mitatu, hakusema hata kidogo, hata alipoulizwa kitu, hakujua la kujibu. Kwa hivyo baadhi ya wakati alipocheza na watoto wengine wa China, alikuja na kuniuliza maana ya Zhuo Mi Cang, halafu nilimwambia ni mchezo wa kombolela, akarudi na kucheza na watoto hao. Kwa njia hiyo tu, alianza kujifunza lugha ya Kichina kidogo na kidogo, baada ya muda mrefu, hivi sasa amekuwa ni kama mwenyeji wa Beijing."

Kwenye mazingira ya lugha ya Kichina, msichana Su Liya amelewa lughaya Kichina kwa haraka sana. Kuanzishwa kwa Chuo cha Confucius cha katika Radio China Kimataif ni kutokana na mtizamo huo yaani kuweka mazingira ya lugha ya Kichina kwa wasikilizaji. Imefahamika kuwa chuo hicho kilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Radio China Kimataifa na makao makuu ya chuo cha Confucius, ambayo ni jumuiya isiyo kibiashara inayolenga kueneza utamaduni wa China na lugha ya China na kuunga mkono ufundishaji wa lugha ya kichina. Chuo hicho kitaandaa vipindi vya kufundisha lugha ya Kichina kwa lugha 38 kwa mujibu wa kitabu cha kiada cha lugha ya Kichina. Vipindi hivyo vitatangazwa duniani kwa njia ya radio na mtandao wa Internet. Kwa hivyo katika siku za baadaye, wasikilizaji wa CRI kote duniani wataweza kujifunza lugha ya Kichina kwa kufuata kitabu halisi cha kiada kilichotungwa kwa lugha ya kichina.

Naibu waziri wa elimu wa China Bw. Zhang Xinsheng alisema, kuanzishwa kwa chuo cha Confucius katika Radio China Kimataifa kumejenga daraja la urafiki angani, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wa nchi mbalimbali kujifunza lugha ya Kichina. Bw. Zhang Xinsheng alisema,

"chuo hicho chenye manufaa maalum yasiyo na mbadala kinaweza kukidhi vizuri zaidi na kwa ufanisi zaidi matakwa ya watu wa nchi mbalimbali duniani kujifunza lugha ya Kichina. Ya kwanza, Radio China Kimataifa imekuwa na uzoefu wa miaka zaidi ya 40 kuhusu kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina; ya pili, mafunzo ya chuo hicho pia yanafuata kanuni na umaalum wa elimu ya kutoka mbali."

Serikali ya China ilianzisha idara za kutoa mafunzo kwa watu wa nchi mbalimbali duniani kuanzia mwaka 2004, na kuzipa idara hizo jina la wawakilishi wa Confucious aliyekuwa mmoja kati ya utamaduni wa jadi wa China. Mpaka sasa, China imejenga vyuo zaidi ya 200 vya Confucius katika nchi na sehemu zaidi ya 60.

Kutokana na mawasiliano kati ya China na dunia kuendelea kuimarishwa na kupanuliwa, thamani ya kiutamaduni na ya kimatumizi ya lugha hiyo pia imeinuka, watu wengi zaidi wa nchi za nje wameanza kujifunza lugha ya Kichina. Kwa mujibu wa takwimu husika, hivi sasa watu zaidi ya milioni 30 wa nchi za nje kote duniani wanajifunza lugha hiyo, na upungufu wa walimu kwenye vyuo vya Confucius umeanza kuonekana. Chuo cha Confucius kimeanzishwa katika Radio China Kimataifa kutokana na hali hiyo.

Mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa shughuli za kueneza lugha ya Kichina duniani Bi. Xu Lin alisema, kuanzishwa kwa chuo hicho kunasaidia kuziba pengo la upungufu uliopo kwenye vyuo vya Confucius katika kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina.

Imefahamika kuwa hivi sasa Radio China Kimataifa ina klabu zaidi ya elfu tatu za wasikilizaji kote duniani. Chuo cha Confucius kilichanzishwa katika Radio China Kimataifa kitaanzisha "darasa la Confucius kwa njia ya radio" katika nchi au sehemu zenye mazingira bora. Wanachama wa klabu si kama tu wanaweza kujifunza Kichina kwa kusikiliza vipindi vya mafunzo ya radio au kwenye mtandao wa Internet, bali pia wataweza kuwasiliana uso kwa uso na walimu wa Kichina waliotumwa na serikali ya China. Hivi sasa madarasa 10 yamejengwa au yameanza kujengwa, likiwemo darasa la Confucius huko Nairobi nchini Kenya, darasa la Confucius kwenye shirikisho la urafiki kati ya China na Japan huko Nagano nchini Japan, darasa la Confucius kwenye chuo kikuu cha ualimu cha Russia, na darasa la Confucius huko Ulan Bator nchini Mongolia.

Imefahamika kuwa ili kuwawezesha marafiki wa nchi za nje kujifunza vizuri zaidi lugha ya Kichina kupitia chuo cha Confucius kinachotoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa njia ya radio, chuo hicho kitatengeneza hatua kwa hatua vipindi vya mafunzo kwa kufuata umaalum wa nchi na sehemu tofauti, na kueneza mtihani wa kiwango cha uwezo wa lugha ya Kichina katika darasa la Confucius katika nchi za nje. Mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Wang Gengnian alisema:

"chuo hicho kingependa kufanya juhudi kujenga daraja kwa ajili ya mawasiliano ya utamaduni na lugha kati ya watu wa China na watu wa nchi mbalimbali duniani, ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya tamaduni mbalimbali duniani na ujenzi wa dunia yenye masikilizano."