Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-19 19:46:45    
Binadamu wafanya juhudi kwa pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

cri

Kutokana na maendeleo ya jamii, mazingira ya hali ya hewa duniani yanazidi kuwa mabaya siku hadi siku, hivi sasa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kumekuwa somo kubwa linalowakabili binadamu. Baada ya kufanya mazungumzo magumu ya siku 13, tarehe 15 Desemba, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika nchini Indonesia ulipitisha "Mpango wa Bali" wenye umuhimu wa kufungua ukurasa mpya. Kupitishwa kwa waraka huo kumeonesha msimamo wa makini wa nchi mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, pia kumeonesha hali mbaya ya kuongezeka kwa joto duniani.

Kutokana na kuongezeka kwa joto duniani, milima ya barafu iliyoko kwenye ncha ya kaskazini na nchi ya kusini za dunia inayeyuka kwa kasi zaidi na zaidi. Kwa mfano, urefu wa Milima ya barafu ya Aletsch ya Ulaya inayojulikana duniani ulipungua kwa mita 110 mwaka 2006. Msichana mmoja wa Ufaransa aitwaye Kemeng alisema:

"Napenda sana milima ya barafu, mimi na wazazi wangu tuliwahi kwenda kutembelea milima ya barafu, niliambiwa kuwa ndani ya milima ya barafu kuna maji baridi, lakini kutokana na kuongezeka kwa joto duniani, milima ya barafu imepungua, naona wasiwasi na kuhofia milima ya barafu inayopendeza, hatimaye itatoweka".

Kutokana na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ifikapo mwaka 2080 halijoto kote duniani itaongezeka kwa nyuzi 2 hadi 4, ambapo hali mbaya ya hewa itatokea mara kwa mara, na maisha na mali za watu wengi wasiohesabika zitakabiliwa na tishio. Kwa upande mmoja, kimbunga kwenye ukanda ya tropiki kitatokea mara kwa mara kwenye miji kadha wa kadha barani Asia na barani Latin Amerika; kwa upande mwingine, maafa ya ukame yatatokea katika sehemu nyingine duniani, ambapo mashamba ya sehemu mbalimbali za Afrika na Ulaya yatakauka na kutoweza kulimika. Na migogoro itakayosababishwa na hali ya kugombea maliasili ya maji huenda itatokea mara nyingi zaidi.

Kutokana na hali hiyo, serikali za nchi mbalimbali zimetambua hali mbaya itakayoweza kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, hivyo zimeanza kuchukua hatua. Kutoka Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na Umoja wa Ulaya hadi mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8, kutoka Mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki hadi Mkutano wa wakuu wa nchi za Asia ya mashariki, mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa mada muhimu ya mikutano hiyo ya kimataifa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alipojibu maswali ya waandishi wa habari mwezi Novemba katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa alisema:

"Hali ya kuongezeka joto duniani imekuwa hali halisi, wanasayansi wametambua wazi hali mbaya ya suala lenyewe. Hatuna haja ya kueleza zaidi kuhusu suala hilo, kwani ushahidi umekuwa wa kutosha, lazima tuchukue hatua bila kusitasita, inatubidi tuchukue hatua kuanzia sasa".

China imetoa mchango halisi kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jibao alipotoa hotuba mwishoni mwa mwezi Novemba kwenye Mkutano wa 3 wa wakuu wa nchi za Asia ya mashariki alisema:

"China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa ya watu, tunapaswa kueleza wazi kanuni kuhusu jukumu la pamoja na lenye tofauti. China inakabiliana kwa makini na mabadiliko ya hali ya hewa, kwani tunaona jukumu hili linahusiana na binadamu wote".

Rais Susilo wa Indonesia alipofafanua "Jukumu la pamoja na lenye tofauti" kwenye Mkutano wa Bali alizitaka nchi zilizoendelea zitekeleze jukumu la kuzuia hali ya kuongezeka kwa joto kote duniani, alisema nchi zilizoendelea zinapaswa kubeba jukumu la kihistoria kwa ajili ya kukabiliana na hali ya kuongezeka kwa joto duniani, nchi hizo zimetambua kuwa lazima zifanye juhudi zaidi katika kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, na pia zinatakiwa kufanya ushirikiano zaidi na nchi zinazoendelea.

Lakini "Mpango wa Bali" ni matokeo ya juhudi za usuluhishi kati ya nchi zilizohudhuria Mkutano wa Bali, ambao haukuweza kuweka bayana malengo ya kupunguza hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani baada ya mwaka 2010. Hivyo nchi mbalimbali duniani zinatakiwa kufanya juhudi kubwa na kufanya ushirikiano halisi ili kupata ufanisi.