Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-19 20:20:02    
Mapishi ya ngisi na liki

cri

Mahitaji:

Liki gramu 20, pilipili mboga gramu 20, pilipili hoho gramu 20, ngisi gramu 50, chumvi kijiko kimoja, sosi ya chaza vijiko viwili, sosi ya mchuzi kijiko kimoja, vipande vya tangawizi na vitunguu saumu

Njia:

1. washa moto, halafu chemsha maji weka vipande vya ngisi kwenye maji korogakoroga, na vipakue.

2. kata liki iwe vipande, kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande.

3.washa moto tena, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi na vitunguu saumu korogakoroga, tia vipande vya pilipili mboga na pilipili hoho korogakoroga, tia vipande vya liki korogakoroga, mimina sosi ya chaza, sosi ya mchuzi, chumvi, korogakoroga halafu tia vipande vya ngisi korogakoroga kwa haraka, halafu kuipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.