Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-20 21:02:39    
Umoja wa Ulaya ujiondoe kutoka msukosuko wa kutunga katiba

cri
Mwaka 2007 ni mwaka muhimu kwa ujenzi wa Umoja wa Ulaya. Baada ya kufanya mazungumzo magumu ya muda mrefu, tarehe 13 Desemba, viongozi wa nchi mbalimbali za Umoja wa Ulaya walisaini "Mkataba wa Lisbon" utakaotekelezwa badala ya mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya. Kusainiwa kwa mkataba huo mpya kumekomesha hali ya kukwama kwa utungaji wa katiba wa Umoja wa Ulaya iliyodumu kwa miaka miwili, na kutia nguvu ya uhai kwa ujenzi wa Umoja wa Ulaya. Waziri mkuu wa Ureno ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya Bw. Jose Socrates alisema: "Labda watu wa vizazi vya baadaye hawataweza kukumbuka maneno tuliyosema leo, lakini nina uhakika kuwa, tumevumbua historia, na siku hii itakumbukwa kwenye historia.

Kama alivyosema Bw Socrates, tarehe 13 Desemba mwaka 2007 itawekwa kwenye historia ya Umoja wa Ulaya, kwani viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya walisaini "Mkataba wa Lisbon" siku hiyo, na hii imeonesha kuwa Umoja wa Ulaya umepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa umoja huo. Bw. Socrates alisema, mkataba huo utauelekeza Umoja wa Ulaya ushike njia yenye matumaini. Alisema: "Yaliyomo ya Mkataba wa Lisbon ni pamoja na sehemu nzuri kabisa ya mali ya urithi ya ujenzi wa Umoja wa Ulaya, huu si mkataba uliotungwa kwa ajili ya siku zilizopita, bali ni mkataba unaoelekea siku za mbele, na kwa ajili ya kujenga Ulaya yenye mambo ya kisasa na ya ufanisi zaidi, na yenye demokrasia zaidi".

Tokea nusu karne iliyopita, Umoja wa Ulaya umeendelezwa kuwa Umoja wa kiuchumi na kisiasa kutoka jumuiya moja ya uchumi ya kikanda, nchi wanachama wa umoja huo zimeongezeka na kufikia 27 kutoka 6. "Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" uliotangazwa mwaka 2004 ni kwa ajili ya kuhakikisha Umoja wa Ulaya unapanuka na kuendelezwa kwa ufanisi siku hadi siku. Lakini wananchi wa Ufaransa na Uholanzi walikataa mkataba huo mwaka 2005, hali hii ikakwamisha mchakato wa kutunga katiba kwa Umoja wa Ulaya. Mwezi Juni mwaka huu Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika huko Brussels, uliamua kutunga mkataba mpya badala ya Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya. Baada ya kufanya mazungumzo magumu, tarehe 18 Oktoba, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walipitisha "Mkataba wa Lisbon" kwenye Mkutano wa wakuu usio wa rasmi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jose Barroso alisema, mkataba huo utainua sana ufanisi wa uendeshaji wa Umoja wa Ulaya, na kuhakikisha nchi za umoja huo zitasema kwa sauti moja. Alisema: "Mkataba wa Lisbon" utaimarisha uwezo wa Umoja wa Ulaya katika utekelezaji wa mpango na kuongeza uwezo wake wa kutimiza kwa ufanisi malengo yaliyowekwa, na utausaidia Umoja wa Ulaya uwaletee wananchi wengi wa nchi za Umoja wa Ulaya siku nzuri zaidi za mbele".

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa mambo ya Umoja wa Ulaya cha China Bw. Xing Hua anaona kuwa, kusainiwa kwa "Mkataba wa Lisbon" ni mafanikio makubwa uliyopata Umoja wa Ulaya katika ujenzi wake. Alisema: "Mkataba huo umeweka sheria kwa hatua ya mwanzo kuhusu mageuzi ya miundo ya Umoja wa Ulaya na namna ya kuendeshwa katika hali ya kawaida, chini ya hali ambayo umoja huo umekuwa na nchi 27 wanachama. Muhimu zaidi ni kuwa, mambo muhimu kadha wa kadha yaliyomo kwenye mkataba wa katiba wa siku zilizopita bado yamebaki kwenye "Mkataba wa Lisbon", hayo yatasaidia zaidi Umoja wa Ulaya uoneshe umuhimu wake mkubwa katika mambo ya kimataifa na kuufanya umoja huo upate ufanisi zaidi katika mchakato wa kutoa maamuzi".

Lakini kutokana na maoni tofauti ya baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya juu ya taratibu mbili kuhusu kupitisha maamuzi kwa kura nyingi zaidi, hivyo "Mkataba wa Lisbon" uliongeza kanuni kuhusu namna ya kushughulikia au kutofautisha miswada mbalimbali yenye hali maalum wakati wa kupitisha maamuzi. Kuwekwa kwa kanuni hiyo, pia kumeonesha kuwa, mchakato wa utungaji wa katiba ya Umoja wa Mataifa vilevile utakuta vipengele mbalimbali.

Kupitishwa kwa "Mkataba wa Lisbon" kumefungua ukurasa mpya wa Umoja wa Ulaya, lakini kama mkataba huo utaweza kutekelezwa kwa mpango uliowekwa au la, itaamuliwa na wananchi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.