Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-20 14:25:43    
Wabunge na mawaziri wanawake wajadiliana kuhusu suala la kuhimiza maendeleo ya akina mama

cri

Mkutano wa tano wa wabunge na mawaziri wanawake wa Asia ulifungwa tarehe 28 mwezi Novemba mjini Beijing. Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Kuwapa haki za elimu akina mama na watoto ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi na jamii". Kwenye mkutano huo, wajumbe zaidi ya 100 kutoka nchi 22 za sehemu ya Asia na Pasifiki na mashirika ya kimataifa walijadiliana kuhusu kuhimiza maendeleo ya shughuli za utamaduni na elimu kwa akina mama, na kutoa taarifa ya kuhimiza haki za elimu za akina mama.

Baada ya majadiliano kati ya wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo, Taarifa ya Beijing ambayo ina lengo la kuhimiza kazi ya kuwapa akina mama haki ya kupata elimu ilipitishwa. Kiongozi wa ujumbe wa New Zealand Bibi Jill Pettis ambaye alikuwa mwendeshaji na kupitisha taarifa hiyo, ana matumaini kuwa taarifa hiyo inaweza kufanya kazi halisi. Alisema:

"Sasa tunapiga kura kuhusu Taarifa ya Beijing. Nashukuru mchango wenu mkubwa katika kuandaa mswada wa taarifa hiyo, nina matumaini kuwa taarifa hiyo inaweza kutoa mchango katika siku za usoni."

Taarifa inasema, kuongeza fursa ya kupata elimu kunafanya maisha ya akina mama na watoto wa kike yabadilike sana, na kuwahimiza kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya jamii na uchumi. Inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa akina mama na watoto wa kike, na kuwa fursa ya kupata elimu na ajira kwa usawa.

Wakati wa mkutano huo, wajumbe pia walijadiliana kuhusu mada tisa zikiwemo hali ya elimu ya akina mama na watoto wa kike na matatizo yanayopatikana katika maendeleo ya elimu ya akina mama na watoto wa kike, uhusiano kati ya kiwango cha elimu cha wanawake na kiwango cha mapato yao, elimu ni msingi wa kuboresha afya ya uzazi, kupambana na ugonjwa wa ukimwi na kuinua kiwango cha wanawake kushiriki kwenye shughuli za siasa kwa kutumia elimu.

Spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo alipokutana na wajumbe waliohudhuria mkutano huo, alisema,

"Kauli mbiu ya mkutano huo ni nzuri. Inafuatilia sana elimu ya wanawake na watoto, hii ni alama muhimu ya ustaarabu wa nchi moja na maendeleo yake ya jamii. Lengo letu ni kupata ukombozi wa wanawake na usawa kati ya wanawake na wanaume. Lakini kazi muhimu ya serikali na bunge ni kuinua sifa ya wanawake, na suala la msingi kuhusu jambo hilo ni elimu. Tuna imani kuwa mkutano huo bila shaka utahimiza nchi mbalimbali zifuatilie zaidi elimu ya wanawake na watoto, pia ninafurahi kuwa mkutano umetuwezesha tufanye maingiliano mazuri."

Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya elimu ya wanawake na watoto wa kike wa Asia imekuwa inaboreshwa siku hadi siku, lakini kutokana na sababu mbalimbali za historia, utamaduni na mitizamo tofauti, wanawake wako katika hali mbaya kwenye ushindani, inahitaji muda mrefu kutimiza usawa kati ya wanawake na wanaume. Kuboresha hali hii kunahitaji juhudi zinazofanywa na wanawake, pia kunahitaji juhudi za pamoja zinazofanywa na serikali za nchi mbalimbali za Asia.

Katibu mkuu wa shirikisho la kimataifa la uzazi wa mpango Bibi Gill Greer alisema,

"Wanawake wanapaswa kuwa na majivuno na kujiendeleza zaidi, maspika na mawaziri wanawake lazima wawe na imani juu ya madaraka yao, na kufanya juhudi kwa ajili ya haki za wanawake na watoto wa kike. Mustakabali wa maelfu ya watu, mustakabali ya sehemu waliko hata dunia nzima unategemea juhudi zetu katika siku za baadaye."

Mkutano wa wabunge na mawaziri wanawake wa Asia ulioitishwa na Baraza la idadi ya watu na maendeleo la wabunge wa Asia, umefanyika kila mara katika miaka mitano iliyopita na umekuwa jukwaa muhimu la mazungumzo na maingiliano kwa wabunge na mawaziri wa nchi mbalimbali za Asia. Mkutano huo ulifanyika hapa Beijing kutokana na Baraza la idadi ya watu na maendeleo la wabunge wa Asia kutambua maendeleo ya shughuli za wanawake nchini China. Mwishoni mwa mwaka jana, mwenyekiti wa baraza hilo alimwandikia barua ofisa husika wa bunge la umma la China akisema, ana matumaini kuwa mkutano huo utafanyika mjini Beijing kwa sababu China imepiga hatua kubwa katika kuwawezesha wanawake washiriki kwa usawa kwenye shughuli za kisiasa.

Idhaa ya kiswahili 2007-12-20