Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-24 15:18:03    
Utalii kwenye Ziwa Nanwan mkoani Henan

cri

Sehemu ya utalii yenye mandhari nzuri ya ziwa la Nanwan iko umbali wa kilomita 5, kusini magharibi mwa mji wa Xinyang, eneo hilo la maji lina kilomita za mraba 75, ikiwa ni pamoja na ziwa Nanwan na msitu wa taifa wa Nanwan zenye vivutio vya milima, misitu na visiwa.

Sehemu ya ziwa la Nanwan licha ya kuwa na raslimali kubwa ya misitu, visiwa, bandari na mazingira bora ya asili, ina utamaduni maalumu wa Xinyang na utamaduni wa samaki wa Nanwan, ambavyo vinawavutia sana watalii. Naibu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa sehemu ya ziwa Nawan, Bw. Liu Bin alisema,

"Sehemu yetu ya Nanwan ni sehemu ya utalii ya taifa yenye mandhari nzuri ya ngazi ya 4A ikiwa ni pamoja na vivutio vya mradi wa maji na bustani ya msitu wa ngazi ya taifa. Sehemu ya ziwa la Nanwan yenye eneo la kilomita za mraba 75 inasifiwa kuwa ni ziwa la kwanza kwenye sehemu ya kati ya China, ambayo eneo lake ni kubwa mara 12 kuliko ziwa magharibi la mji wa Hangzhou, Xihu. Sehemu hiyo yenye eneo kubwa la maji lina visiwa 61 vyenye maumbo mbalimbali."

Kisiwa kimoja kinachojulikana zaidi ni kisiwa cha ndege. Watalii wanaweza kwenda huko kwa kutumia boti, ambako ni umbali wa kilomita 3 au 4 hivi, kisiwa hicho chenye miti mingi kinaitwa na wenyeji kuwa mlima Bagua. Kwenda mbele kwa kilomita 5 kuelekea upande wa kusini magharibi kutoka kwenye mlima Bagua, ni kisiwa cha ndege cha sehemu ya ziwa Nanwan, wenyeji wa huko wanasema, mwanzoni kabisa kisiwa hicho kiliitwa mlima Paifang, wakati wa mwishoni mwa enzi ya Qing, mwanamke mmoja aliyeitwa Caishi alizaa mtoto mmoja wa kiume, hapo baadaye mume wake alifariki kwa ugonjwa, na ilimbidi Caoshi peke yake amtunze mtoto wake, na hakuolewa tena. Mfalme aliamuru kujengwa kwa Paifang, ambayo ni kama lango kubwa la mawe, ili kumsifu. Toka wakati ule, kisiwa hicho kiliitwa kisiwa cha Paifang, baadaye ndege wengi walihamia huko, na siku hadi siku jina la kisiwa cha Paifang lilibadilika na kuitwa kuwa kisiwa cha ndege.

Watu wakiwa katika kisiwa cha ndege, wanaweza kuwaona ndege na kusikia milio yao kila mahali, kila mwaka kuna ndege wa aina ya Egret kiasi cha laki moja waliohamia kwenye sehemu ya kusini kutoka sehemu ya kaskazini ya China, hukaa huko kwa muda na kuzaliana kwenye kisiwa hicho. Jambo linaloshangaza ni kuwa, ni kwa nini aina hiyo ya ndege wanakaa kwenye kisiwa hicho tu kati ya visiwa 61 vya sehemu ya ziwa la Nanwan? Sababu yake ni kuwa kwenye kisiwa cha ndege kuna miti na mimea mingi, hususan ni aina ya miti ya Teak, ambayo majani yake yanatoa harufu nzuri wanayoipenda ndege wa aina hiyo, hivyo wanakuja kwa wingi kujenga viota vyao kwenye kisiwa hicho. Mbali na hayo, sehemu ile kuna vijito vingi, ambavyo baadhi yake vina maji machache, ni mahali pazuri pa kuweza kupata chakula cha samaki na kamba wadogo kwa ndege hao. Kutokana na kuweko kwa mazingira bora, kila mwaka toka mwezi Machi hadi mwezi Novemba kuna ndege wa Egret kiasi cha laki moja wanaoishi huko.

Watalii wanaotembelea kisiwa cha ndege, hawakosi kwenda kutembelea bustani ya "Niaoyulin", maana yake katika lugha ya Kichina ni msitu wenye milio ya ndege, bustani hiyo yenye eneo la mita za mraba 15,000 ilijengwa mwaka 2004, bustani hiyo ina vivutio vingi, ambavyo ni pamoja na maporomoko ya maji ya kutoka sehemu ya juu ya mlima, kijito cha bata wenye upendo wa kichina, ziwa la bata maji, kiwanja cha njiwa na jumba la michezo ya ndege, kwenye bustani hiyo kuna aina zaidi ya 300 za ndege, ambao idadi yao inazidi 1,000.

Kwenye bustani hiyo unaweza kuwaona bata wenye upendo wa kichina wakiogelea, bata maji wenye shingo ndefu wakilia pamoja na ndege adimu wakubwa wenye manyoya maridadi na kifua cha rangi nyekundu na ndege adimu wenye rangi nyeupe kichwani na mkia mrefu. Kwenye jumba la michezo ya ndege, kuna ndege wa Liao Columbia wanaosema maneno ya "karibu, karibu!" kwa watalii, kasuku wanaopiga kinanda na kucheza, na ndege wanaoweza kutambua noti za fedha na kufanya hesabu, michezo yao inashangiliwa na watalii mara kwa mara. Kwenye upande wa kusini mashariki wa msitu wenye milio ya ndege pia kuna sehemu moja yenye ndege wengi. Ukinyanyua kichwa na kuangalia juu, utaona ndege chungu nzima kwenye anga, miti na maji, ambao wengi wao hujui ni wa aina gani. Kwenye bustani hiyo, watu wanaweza kuona bata wenye upendo wa kichina mtalii mmoja kutoka Beijing aliyefuatilia ndege kwenye kisiwa hicho, Bibi Li Ping alisema,

"Kwenye kisiwa hicho kila mwaka kuna ndege wengi zaidi, wengi wa ndege hao sijui ni wa aina gani, baadhi ya ndege, hata unashindwa kuwaona kwenye zizi la wanyama, ni ajabu sana."

Baada ya kuondoka kutoka kwenye kisiwa cha ndege, baada ya muda mfupi utafika kwenye kisiwa cha kima. Tuliona ndege wengi wakicheza kwenye matawi ya miti, manyasi na mawe. Wengine walikaa chini wakiwa wamekunja miguu wakiangalia huku na huku, wengi wao waliweka watoto wao vifuani mwao kwa upendo, baadhi yao walikuwa wakipigana kwa kucheza, na wengine wakikamata chawa na kujikuna. Baadhi ya kima wasio na woga, wakiwaona watalii waliwasogelea na kukodolea macho kwenye chakula walichokuwa nacho mikononi, mtu akitupa karanga chini, kima hawana wasiwasi wanaenda kugombea, mtalii mmoja alifungua kifuniko cha chupa ya maji na kuiweka chupa chini, kulikuwa na kima mmoja aliyekwenda haraka kuichukua na kunywa maji bila woga. Mwongoza watalii, Bi Ye alisema,

"Kima hao walihamishiwa hapa kutoka milima Taihang, hawa ni wa kundi moja na wana kiongozi wao. Kiongozi wa kundi la kima, ana madaraka na kupata chakula kwanza, anatuma kima wengine kufanya doria au kwenda kutafuta chakula, licha ya hayo ana haki ya kuwachukua kima jike vijana kuwa wake zake, ambao kima wengine hawaruhusiwi kuwa pamoja nao."

Kima waliochezacheza waliwafurahisha watalii, watalii wengi walikuwa hawataki kuondoka haraka. Mfugaji wa kima hao, Bibi Wang Jianping alisema,

"Kwetu hapa kuna bwawa la maji la Nanwan, mazingira ya hapa penye miti na mimea mingi panafaa sana kwa maisha ya kima. Hapa kuna miti mingi inayozaa matunda ya aina mbalimbali yanayopendwa na kima .

Idhaa ya kiswahili 2007-12-24