Alasiri ya tarehe 24 kabla ya sikukuu ya Krismasi, askari wa rejimenti ya pili ya jeshi la Marekani nchini Iraq walijizatiti na kuwa tayari kuondoka kambini. Lakini hawakwenda kwenye sherehe ya Krismasi kama kawaida yao, bali walijipenyeza ndani ya madereya na kwenda kufanya doria mjini Baghdad.
Hii ni sikukuu yao ya tano ya Krismasi nchini Iraq. Maafisa wa jeshi la Marekani wanaelewa kwamba kila sikukuu ya Krismasi inapofika, ni lazima kuwatuma askari kufanya doria. Kufanya hivyo sio kwa ajili ya kulinda usalama bali ni kwa ajili ya kuwafanya askari wasiwakumbuke wanafamilia wao na kuhakikisha ukakamavu wao wa kiaskari.
Katika sikukuu ya Krismasi, kwenye kambi za jeshi la Marekani huandaliwa chakula kinono cha mchana na cha usiku, na ndani ya kambi zinajaa zawadi za aina mbalimbali zilizoletwa kutoka nchini Marekani na kambi hupambwa kwa mazingira mazuri ya Krismasi. Lakini wakati huo hakuna mtu anayethubutu kusema "Heri ya Krismasi!" kwa mwenzake.
Afisa Roy amekuwepo kwenye Jeshi la Marekani kwa miaka 23. Mwaka huu akiwa pamoja na askari wake mia moja anapitisha sikukuu yake ya tatu ya Krismasi nchini Iraq. Bw. Roy alisema, "Najua kwamba wakati huu inafaa niwasalimu kwa kusema 'Heri ya Krismasi!' Lakini nikisema hivyo mara nitawakumbusha hali yao ya mbali na nyumbani kwao na furaha yao ambayo wangeipata katika siku hiyo."
Wakati ulipokaribia mkesha wa Krismasi, padri mmoja alikuwa akishughulikia kuwagawia zawadi askari. Alisema askari hao vijana wanapopata zawadi za wanafamilia wao, huwa wanapiga kelele kwa furaha na kusema, "Ah, baba na mama wananikumbuka." Kisha wanakimbia kwenye kambi yao na kukaa kwa upweke.
Kwa daktari mwenye umri wa miaka 20 Bw. Georncy huu ni mwaka wa pili kwake kupitisha sikukuu ya Krismasi nchini Iraq. Mwaka huu amepata mwanasesere wa swala, huyu ni mwanasesere anayempenda sana kwa sababu kichwani kuna kofia ndogo ya jeshi la Marekani. Sasa baada ya yeye kukua vile vile amevaa kofia ya jeshi la Marekani. Alisema mwanasesere huyo ni rafiki yake mkubwa, mwaka huu anaweza tu kusherehekea Krismasi pamoja na mwanasesere huyo."
"Lakini natamani kukaa na wanafamilia wangu" Bw. Georcy aliendelea, "Nilipokuwa nyumbani nilikuwa hutwika mwanasesere wa swala kichwani na kuwachekesha wazazi wangu, natamani nipate tena siku kama hiyo." Bw. Georcy aliposema hayo macho yake yalikuwa mwekundu.
Maofisa wakubwa wa jeshi la Marekani walisema, katika miaka ya hivi karibuni matukio ya milipuko yamepungua, askari wa Marekani pia wamekuwa na moyo mwepesi kidogo. Tovuti ya jeshi la Marekani ilitangaza kwamba mwezi Novemba askari 40 wa Marekani waliuawa nchini Iraq, mwezi Desemba askari 17 tu waliuawa nchini humo. Jeshi la Marekani linaona habari hiyo ni nzuri kwa sababu idadi ya askari waliouawa imepungua, na kusema mwezi wa Desemba ni mwezi salama kabisa tokea vita vya Iraq kuzuka, bila shaka furaha yao inapatikana kutokana na kulinganishwa idadi ya askari 131 waliouawa mwezi wa Mei.
Mwaka huu katika sikukuu ya Krismasi kikosi cha Bw. Roy pia kilipata zawadi moja isiyo ya kawaida, zawadi hiyo ilitumwa na rafiki wa askari mmoja aliyeuawa nchini Iraq, askari huyo aliuawa na wanamgambo mwanzoni mwa mwaka huu. Wanafamilia wa askari huyo walihuzunika sana wakati wanapopitisha siku ya kwanza ya Krismasi baada ya yeye kuuawa. Rafiki anawakilisha marehemu kuwatakia heri na salama.
Katika siku ya Krismasi ya mwaka 2007 afisa Roy alisema, "Lengo lengu ni kujitahidi niwezavyo kuhakikisha askari wangu wanarudi nyumbani wakiwa hai."
Idhaa ya kiswahili 2007-12-24
|